Ona kilichompata huyu jamaa

Ona kilichompata huyu jamaa

Kurunzi

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
10,175
Reaction score
11,572
Ni miaka michache kidogo imepita tukiwa chuo, mwanachuo mwenzetu rafiki yetu, alipata mkasa mbaya kabisa.

Siku moja dogo mmoja alimletea pc ili amsadie kuiformat, kumbuka tuliosomea masomo ya electronics tumeishi sana kwa hizi mishe.

Kabla ya kuiformat huyu mwamba aliona kuna docoments muhimu sana kwenye hiyo pc, aliamua kuzi copy kwenye flash yake.

Siku zikawa kidogo zimepita, siku moja mwamba aliamka yupo tee mfukoni, hali tete akamua kujilipua unajua tena maisha ya chuo.

Akaona isiwe taabu, alienda cafe akapitia zile documents ilikuwa kama report ya reseach fulani hivi, kulikuwa na mawasiliano ya simu ya mwenye hiyo report, alikuwa mwanamke, alimpigia simu na kumueleza alikuwa na document zake, alimwambia wakutane ampe.

Baadaye waliendelea kuchat kwa sms ili kupanga mahali pa kukutana ili ampe document zake, mwamba alijua huyo mama atamtoa japo kidogo, lakini pia atamuuzia hiyo flash apate vijisenti vya kujikimu unajua tena maisha ya chuo.

Mipango ilifanyika ili wakutane maeneo ya Mwenge, kweli walikutana kwenye harakati za kuanza kumuonesha zile documents kwenye pc ya yule mama dah polisi hawa hapo, loh wakamwambia yupo chini ya ulinzi kuanzia sasa.

Walimchukuwa mpaka central police, alihojiwa zaidi ya masaa 4, jamaa alihojiwa kwa kesi ya mauaji, kumbe ile pc dogo aliyompelekea ili aiformat ilikuwa imeibwa kwenye ofisi moja, majambazi waliingia usiku na kuiba vitu walimpiga mlinzi wakamuumiza vibaya na baadaye alipoteza maisha.

Jamaa alitahayari sana, hakuamini anayoyasikia, mbaya zaidi hata yule dogo hamjui kwani alielekezwa na yule jamaa aliyemuelekeza alikamatwa baada ya kumhoji akasema hamjui.

Jamaa alikaa ndani miaka 2.3, tunashukuru jamaa waliohusika na lile tukio walikamatwa wakawa ndiyo pona yake na jamaa mwingine, hata hivyo aliendelea kusota ndani.

Ilibidi ifanyike mipango ya kumtoa sitaisema ila jamaa ilimbidi aende moja ya nchi ya Kusini mwa Afrika, ambako alikaa miaka 12.

Ila kwa sasa amerudi yupo nchini, anapambana na mishe zake.
 
Sijui ni tatizo la kiswahili kuwa kigumu sana ama ni nini maana kwa namna ulivyoandika ni kama mwanafunzi wa shule ya msingi ambaye bado hajajua vizuri kusoma na kuandika. Umeeleweka japo kwa mbinde
 
Kila jambo lazima ufikirie sana hasa katika usalama wako kabla ya kuamua kufanya maamuzi, usiwaze masilahi tu kuna mambo makubwa nyuma yake
 
kuna jamaa magomeni alinipigia story kama hii...yeye ananunuaga vitu vya deal lkn mpaka akujue, sasa bana enzi hizo akanunua ipad na laptop sijui na nn waliomuuzia waliletwa na jamaa mwingine kama dalali hivi....

amekaa kama wiki tatu hv halafu vitu bado anavyo yule dalali akampigia simu kumuuliza kama jamaa vitu anavyo jamaa akasema hajaviuza bado anavyo...

jamaa kakaa mida kidogo ukaja mtiti wa maaskari balaa, wakamchota jamaa, dalali haooo wakaondoka!

Jamaa ananiambia kumbe vitu viliporwa kwa mzungu,wakati wanampora mzungu akakomaa na begi..jamaa wako kwenye gari mzungu chini, walimburuza balaa wakaondoka na begi huku nyuma mzungu..akaenda hospitali akafa....msala ukaanza...

wale wezi sijui ilikuaje wakajua mmoja akapotea mwingine akakimbilia south msala wakabaki nao masela

jamaa ananiambia alikaa jela miaka 2.5 anasota kesi ya mauaji, sijui na nn na nn..!

kilichomuokoa jamaa ni kwamba kuna sister ake alikua anakaa arusha akaipata hiyo ishu, sister kumbe alisoma na wakili mmoja matata sana hapa dar sekondari au primary...yule wakili ndo akaingilia kati...

dogo akachomoka,yule wakili hakuchaji hata mia...!

jamaa mpaka leo haamini hata kidogo! ila jamaa yuko poa ana hela yake ya kutosha tu..anapiga mishe zake hapo mapipa fresh tu!

vitu vya mkononi ni majanga
!
 
Ni miaka michache kidogo imepita tukiwa chuo, mwanachuo mwenzetu rafiki yetu, alipata mkasa mbaya kabisa.

Siku moja dogo mmoja alimletea pc ili amsadie kuiformat, kumbuka tuliosomea masomo ya electronics tumeishi sana kwa hizi mishe.

Kabla ya kuiformat huyu mwamba aliona kuna docoments muhimu sana kwenye hiyo pc, aliamua kuzi copy kwenye flash yake.

Siku zikawa kidogo zimepita, siku moja mwamba liamka yupo tee mfukoni, hali tete akamua kujilipua unajua tena maisha ya chuo.

Akaona isiwe taabu, alienda cafe akapitia zile documents ilikuwa kama report ya reseach fulani hivi, kulikuwa na mawasiliano ya simu ya mwenye hiyo report,alikuwa mwanamke, alimpigia simu na kumueleza alikuwa na document zake, alimwambia wakutane ampe.

Baadaye waliendelea kuchat kwa sms ili kupanga mahali pa kukutana ili ampe document zake, mwamba alijua huyo mama atamtoa japo kidogo, lakini pia atamuuzia hiyo flash apate vijisenti vya kujikimu unajua tena maisha ya chuo.

Mipango ilifanyika ili wakutane maeneo ya Mwenge, kweli walikutana kwenye harakati za kuanza kumuonesha zile documents kwenye pc ya yule mama dah polisi hawa hapo, loh wakamwambia yupo chini ya ulinzi kuanzia sasa.

Walimchukuwa mpaka central police, alihojiwa zaidi ya masaa 4, jamaa alihojiwa kwa kesi ya mauaji, kumbe ile pc dogo aliyompelekea ili aiformat ilikuwa imeibwa kwenye ofisi moja, majambazi waliingia usiku na kuiba vitu walimpiga mlinzi wakamuumiza vibaya na baadaye alipoteza maisha.

Jamaa alitaayari sana, hakuamini anayoyasikia, mbaya zaidi hata yule dogo hamjui kwani alielekezwa na yule jamaa aliyemuelekeza alikamatwa baada ya kumhoji akasema hamjui.

Jamaa alikaa ndani miaaka 2.3, tunashukuru jamaa waliohusika na lile tukio walikamatwa wakawa ndiyo pona yake na jamaa mwingine, hata hivyo aliendelea kusota ndani.

Ilibidi ifanyike mipango ya kumtoa sitaisema ila jamaa ilimbidi aende moja ya nchi ya Kusini mwa Afrika, ambako alikaa miaka 12.

Ila kwa sasa amerudi yupo nchini, anapambana na mishe zake.
Umesema alikwenda Afrika kusini au ndio unamzungumzia MC muga
 
Miongoni mwa sababu nilizoacha hizi ishu na kubypass frp
Mimi niliacha kununua mali za mkononi sijui simu used, laptop used unless nakufahamu na niliona toka umeinunua ikiwa mpya, otherwise iwe ni iPad au iPhone utoe iCloud niweke yangu.

Kuna jamaa kariakoo alikuwa na frem anauza pc used, alipataga msala wa kuuziwa PC used kumbe bwana shamba kauawa huko pc imepigwa. Alisota sana ndani honga sana na kufilisika juu
 
Mshkaji wangu alikua na Samsung note 4 akakutana na mshkaji wake akamuambia tubadilishane nikupe note 5 kisa kapenda rangi ya note 4. Isipokua note 5 ina frp akawasiliana na mimi nikamuambia tutaclear aichukue tu.

Ikaja tukabypass vizuri tu. Baada ya pale akamuuzi mtu kupatana ile simu.

Muda ukapita siku hiyo kafuatwa na askari wamemkamata mpaka O bay, O bay akamkuta yule jamaa aliyesema wabadilishane akamkuta na jamaa aliyemuuzia huko kupatana.

Turns out simu ni ya mkandarasi mchina aliibiwa Chato pamoja na laptop na vitu vingine. Yeye alibadilishana simu na huyo jamaa Dom ila wote wakakutana Dar, O bay.

Simalizii kilichotokea.
 
Moral of the story ni kwamba 'Tamaa Haifai,' si ndiyo? Jamaa alitaka ajiongeza ili apate hela akajisifie kwa wenzake kuwa ni mjanja wa kimaisha.
 
kipindi cha zamani sana kuna manyamera walimuua mdosi ila kwa kutumwa basi baada ya mauaji ilikuwa hamna kuiba kitu bali kuishia.mmoja wao akaingiza tamaa baada ya kuona redio kali matata ikabidi atoke nayo.kwa ushamba wake kila akijaribu kuiwasha inamshinda akaona aipeleke kwa fundi lamda mbovu.fundi nae alivyokuwa zumbukuku akashindwa kuiwasha ikabidi aifungue hapo jamaa alieipeleka akaambiwa arudi kesho.fundi kufungua akakuta picha ya mdosi ndani ya redio na taarifa zilikuwepo kuhusu hayo mauaji.jamaa alivyofata redio tuu wakamdaka
 
Ishi kulingana na uwezo wko.Mengine yaweza kukutoa roho
 
Back
Top Bottom