Nimejiandikishia Kagera lkn kituo changu cha kazi ni Kigoma hii ina maana ya kwamba hata siku ya uchaguzi nitakuwa Kigoma
Katoe taarifa kwa mkurugenzi wako wa uchaguzi, yaani mkurugenzi wa wilaya huko kigoma. Yeye ataandika barua kwenda kwa tume aki quote namba yako ya kadi, kituo ulichojiandikishia na kituo kipya utakacho pigia kura. Halafu tume itabadilisha na utapiga kura. Usi panic
Jamani naombeeni msaada juu ya hili. Hili zoezi la kujiandikisha kupiga kura limenikuta nje ya mkoa wangu maana nilisafiri kikazi nikaja mkoani Kagera. Sasa kule kwetu zoezi linaendelea sawa na hapa Kagera.
Sasa tumeshauliwa eti tukajiandikishe popote pale hivi vitambulisho vitatuwezesha kupiga kura eneo lolote lile Tz.
Sasa baada ya kwenda kujiandikisha huku nilipo watu wananiambia eti kura yangu imeshapotea sitaweza kupiga kura nikiwa nje ya mkoa/kituo nilichojiandikishia.
Sasa nawaza hapa si ndio nishapoteza haki yangu? Maana mm sina shida na kitambuslisho vitambulisho ninavyo vingi nachotaka haki ya kupiga kura.
Halafu walichonishangaza ni kwamba unaandikwa bila kukuuliza document yoyote hii inamaanisha wahamiaji haramu ni rahisi sana kujichomeka hapa.
Ushauri katika hili wataalamu vp nitapiga kura kweli?
Ndugu zangu nimejiandikisha na katika kujiandikisha huko nilimuuliza muandikishaji juu ya uchaguzi kunikutia mahali ambapo sijajiandikishia amenijibu hivi
Unaweza kumchagua rais popote pale utakapokuwepo Tanzania lakini Mbunge na Diwani hutaweza lazima urudi pale ulipojiandikishia ukitaka kuchagua mbunge na diwani' lakini kwa rais ni popote utakapokuwepo
Kajiandikishe kwako mkuu hawana uwezo wa kujua duplicate!
Wanadanganyika sana tu!
Ofcn tulikuwa tunabisha, dogo mmoja kajitosa, mpaka ninavyokwambia anavitambulisho viwili tayar, alichofanya ni kubadilisha vituo tu!
Kwa BVR tutachemka sana tumekurupuka
Tatizo lenu mnaleta siasa kwenye kila jamboNaona kama hili ni wazo zuri tatizo nitamkuta ofisini au atanisikiliza kweli kabla sijatolewa nduki na PS wake
Nimejiandikishia Kagera lkn kituo changu cha kazi ni Kigoma hii ina maana ya kwamba hata siku ya uchaguzi nitakuwa Kigoma
Msihangaike kutakuwa na kipindi maalum cha uboreshaji daftari kabla ya uchaguzi. Utakwenda kwa msimamizi wa uchaguzi na utabadilishiwa kituo tena sasa ni rahisi kwa kuwa maelezo yote yako kwenye kadi ya kura. Tume ilikwisha kutoa Maelezo haya.
Mna jidanganya tu, halavyo watu wengine ni wagumu sana kuelewa , hizo kiti zinakuwa na local information
Na unaweza kujiandikisha hata mara 10 kwenye vituo tofaut , pala watakapo jiunganisha na vituo vyote kenye data base lazima utaoneka tu na hapo ndio kimbembe kitatokea