Mathanzua
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 17,035
- 22,713
Mimi ni mwanachama wa CCM.Kwa muda mrefu nimekuwa nakerwa mno na mambo yaliyokuwa yanaendelea katika nchi yetu, kiasi kwamba ilifika wakati ikaonekana kana kwamba wananchi wa Tanzania hawana mtetezi kabisa.Kila mtu atakubaliana na mimi kwamba wananchi wa Tanzania sasa wamepata mtetezi wa kweli, Rais Dr.John Pombe Magufuli.Ushindi dhidi ya kampuni ya Barrick Gold, ambapo kampuni hiyo imekubali kuilipa Tanzania haki yake yote,si wake binafsi ila ni wa Watanzania wote,hata na wale ambao walikuwa wanasema "tutakunywa shubiri."Huu ni ushindi wa kihistoria,na Rais wetu anastahili pongezi kwa kazi nzuri aliyoifanya.
Kwa ushindi huu wa awali, tunakiomba Chama kuandaa maandamano nchi nzima ya kumuunga mkono Rais katika vita hii ngumu ya kiuchumi aliyoinzisha.Maandamano haya yawe ya Watanzania wote,bila kujali itikadi zetu za kisiasa. Nia ni kumpongeza, kumpa hamasa,ujasiri na mandate ya kuendeleza vita hii ngumu.
Mungu ibariki Tanzania.