Ombi Maalumu: Katiba Mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ombi Maalumu: Katiba Mpya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mchaga, May 24, 2012.

 1. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wakuu naomba kuwasilisha kwenu hoja yangu ya kuomba tuanzishe thread maalumu ya kujadili na kuchambua Katiba yetu wakati tukianza mchakato wa kuwa na Katiba Mpya.

  Nadhani itakuwa vyema kwa sababu zifuatazo:

  1. Kuwasadia Kamati iliyoteuliwa kupata maoni kupitia Mitandao ya Jamuu na JF ni mojawapo (tusidharau nguvu ya hizi new media)

  2. Kwa kupitia JF wengi watakuwa huru kuweka maoni yao

  3. Baadhi ya wajumbe wa katiba mpya ni wanachama hapa hivyo itasaidia sana kuwapa mawazo na michango mbalimbali ya namna bora ya kukamilisha kazi hii

  4. Kupitia JF na sisi wananchama tulio mbali tutaweza kuwakilisha mawazo yetu japo itakuwa si katika vikao rasmi lakini baadhi ya mawazo yanaweza kuchukuliwa na kuwasilishwa katika vikao rasmi

  Namuomba Moderator na wadau wengine waone kama itakuwa vyema kuwa na wazo hili na kulifanyia kazi au kuboresha namna bora zaidi ya kuwa na special thread.

  Naomba kuwasilisha kwenu.

  Asante.
   
 2. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Mchaga mbona katika hii page ya Jukwaa la Siasa kuna sub-forum ya KATIBA MPYA?

  Pitia hapo kwani kuna michango mingi tu ya wanachama JF ambayo ni mizuri na wewe pia utoe maoni yako hapo ili sote tuelimike.


  NIMEAMINI KUWA TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA.
  MIZAMBWA
  NABII MTARAJWIA!!!
   
Loading...