Ombi maalum kwa sumatra

Ombi maalum kwa sumatra

kindikwili

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2016
Posts
1,862
Reaction score
2,876
Kwanza niwapongeze wafanya kazi wote wa SUMATRA kwa kazi kubwa mnayoifanya kuhakikisha sekta ya usafiri na usafirishaji nchini unasonga mbele na wananchi wanapata huduma bora. Pongezi hizi naomba ziwatie nguvu na kuwapa motisha zaidi kwani tunatambua kazi yenu na umuhimu wenu katika ujenzi wa taifa hili

Lengo la mada tajwa hapo juu ni kuwaomba kuchunguza , kupima na baadaye kuridhia kama mtaona inafaa kuongeza magari kwenye barabara ya MANDELA hasa kwa magari ya kwenda MAKUMBUSHO. Kwakweli magari yanayokwenda makumbusho yakitokea Segerea, Temeke, Buguruni na Gongo la mboto ni machache sana ukilinganisha na wingi wa watu hasa wakati wa asubuhi na jioni. Wananchi wanaopandia njiani mfano vituo kama Tabata reli, TOT, Mwananchi, Gereji, External, Mabibo hostel na River side wanapata shida sana ya usafiri kiasi kwamba wengi wanachelewa kufika kwenye maeneo yao ya kazi kwasababu magari yanakuja yameshona kweli. Huu muda ambao raia walio tayari kwenda makazini wakiwa na nauli zao wanapoteza ingetosha kufanya kazi nyingine huko waendako.

Sitaki kuwachosha maana tayari ombi langu limefika na mtalifanyia kazi kwa wakati ufaao, lakini pia naomba muangalie namna ya wafanyabishara wanaotaka kujiingiza kwenye usafiri wa jiji waanze kuleta magari makubwa kama Hitcher, au yale yenye mfano wa mwendo kasi. Kwasabau yale magari yanaweza kubeba coaster hizi za kawaida 2 hivyo tutapunguza idadi ya magari lakini pia tutawahakikishia wananchi usafiri mzuri.

Pongezi sana kwa kurahisisha usafiri wa buguruni, temeke, na ukanda huo kwenda mbezi ya kimara maana magari ni mengi hadi raha.
Wenu katika ujenzi wa nchi.

Kindikwili

Masasi kwasasa Dsm
 
Sumatra hawana shida na hilo, ila wamiliki ndio hawaombi hizo njia. Waombe wamiliki waombe au utaponunua basi lako utaomba hiyo ruti
 
Back
Top Bottom