Ombi la Zitto Kabwe kwa Rais Samia

Ntozi

JF-Expert Member
Feb 1, 2021
226
299
Kauli ya Zitto Kwa Rais juu ya kumsamehe mwenzao ambae hakuwepo mkutanoni Kwa changamoto za kisheria,ni kauli ya kiutu inayolenga pia kujenga mshikamano wa Amani Kwa sasa na siku zijazo.

Lakini wengine wanajiuliza kwamba Zitto Kwa nafasi yake, angeweza kuonana na Rais huko Ikulu na kumwomba juu ya hilo.

Ukizingatia kuwa chama anachokiongoza kinaunda serikali ya umoja wa kitaifa huko Zanzibar, haiwezi kuwa ngumu kwake kuonana na mama na kushauriana nae juu ya hilo la mwenzao.sasa haya matamko ya majukwaani, yanaongeza tu mijadala Kwa sababu kila mtu anakuja na maoni yake kiasi cha kufifisha uzito wa hoja nzuri Sana ya mh.Zitto Kwa mh.Rais.

Vyama vya siasa vya upinzani, vinatakiwa kuwa na umoja na kauli moja isiyotia Shaka juu jambo lolote ambalo vinaona haliko sawa Kwa ustawi wa demokrasia yetu changa.
 
Ombi hilo hilo la Zitto la kutaka Mbowe aachiwe lilishafanywa na watu wengi akiwemo Mnyika kupeleka Maombi TCD na kwa Mangula.

Mjadala unakuja kisa Zitto kaomba mbele ya Rais na Rais katoa kauli yenye uelekeo na hilo watu wasiomtakia Mema Zitto hawalipendi walitamani nafasi hiyo itoke vinywani mwao
 
huyo snitch alitumwa nani kuomba huo msamaha? na msamaha wa kosa gani alilo fanya mbowe?
 
Tatizo la chadema walitaka waende wao peke yao zitto wanamuona kama adui yao kuliko ccm hawa kuwelewa ni vigumu sana
 
Ile ni planned. Kwa kuwa ZZK aliamua kuhudhuria mkutano huo ilikuwa lazima afanye jambo kuonesha CDM wamekosea kususa.
 
Kesi yenyewe ya michongo halafu mtu anapigiwa magoti kwa msamaha, Nchi inajilaani kwa madhambi ya viongozi.
 
Nakubaliana na Mh. Zitto, ameongea kiungwana na kwa heshima. Sawa, kauli yake, kimantiki ya sheria inaleta tafsiri hasi,kwamba Mbowe amekosa sasa msamaha unahitajika. Ukiacha tafsiri hizo za kitaalamu, kienyeji ni sawa, na ilikua lazima kuanzisha maridhiano ili kuliponya taifa.
 
Lisu kalopoka huko DW kama kuheshimu mawazo ya watu hamuwezi hivi mkijakupewa hii nchi si tutakula bakora wananchi? kwakweli mnatutisha sana nyie watu.
 
We kaandae mkutano kwa jina la wadau wa demokrasia, wewe fanya kama unaomba mwenzenu aachiwe huru, mimi nitatoa kauli ya kimazingira halafu baada ya siku si nyingi yule mwingine atasema sioni haja ya kuendelea na hii kesi, halafu mabeberu wataachia mpunga walioubana, halafu lile bunge lao litakuwa haliongelei serikali yetu.
 
huyo snitch alitumwa nani kuomba huo msamaha? na msamaha wa kosa gani alilo fanya mbowe?
Chadema mwacheni Mbowe atoke gerezani akaungane na familia yake, hashtag zenu haziwezi kumsaidia chochote Mbowe
 
We kaandae mkutano kwa jina la wadau wa demokrasia, wewe fanya kama unaomba mwenzenu aachiwe huru, mimi nitatoa kauli ya kimazingira halafu baada ya siku si nyingi yule mwingine atasema sioni haja ya kuendelea na hii kesi, halafu mabeberu wataachia mpunga walioubana, halafu lile bunge lao litakuwa haliongelei serikali yetu.
Huo ndo ukweli wenyewe.
 
Chadema tatizo Lao ni kujiona Wana nguvu kuliko uhalisia...ndo maana Magufuli aliwafuta kabisa ingawa kwa mbinu chafu..

Bado hawajifunzi kabisa..
Siasa maanake ni mazungumzo na kwenye mazungumzo 'compromise ' ni kawaida..

Ukitaka kushikilia misimamo yako as if unayo hiyo power ..ni utoto..
Sasa Zitto ndo kageuka adui wao...
Wako tayari Mbowe asote hata miaka mitano ndani mradi wajifanye Wana 'misimamo'
Wakati juzi Tu walikuwa na Lowasa na Sumaye meza moja
 
Kauli ya Zito Kwa Rais juu ya kumsamehe mwenzao ambae hakuwepo mkutanoni Kwa changamoto za kisheria,ni kauli ya kiutu inayolenga pia kujenga mshikamano wa Amani Kwa sasa na siku zijazo.
Lakini wengine wanajiuliza kwamba Zito Kwa nafasi yake,angeweza kuonana na Rais huko Ikulu na kumwomba juu ya hilo.Ukizingatia kuwa chama anachokiongoza kinaunda serikali ya umoja wa kitaifa huko Zanzibar,haiwezi kuwa ngumu kwake kuonana na mama na kushauriana nae juu ya hilo la mwenzao.sasa haya matamko ya majukwaani,yanaongeza tu mijadala Kwa sababu kila mtu anakuja na maoni yake kiasi cha kufifisha uzito wa hoja nzuri Sana ya mh.Zito Kwa mh.Rais.
Vyama vya siasa vya upinzani, vinatakiwa kuwa na umoja na kauli moja isiyotia Shaka juu jambo lolote ambalo vinaona haliko sawa Kwa ustawi wa demokrasia yetu changa.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Mtu huna kosa, hujawahi kutenda kosa, unaombaje kusamehewa ?

Kauli nyingine ni za kipumbavu sana
 
Back
Top Bottom