Ombi kwa Rais: Tupunguzie ukubwa wa bunge!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
94,035
164,306
BBunge la JMT ni kubwa mno hali inayofanya likose tija.Kwa kuwa idadi ya majimbo haitamkwi na katiba, namuomba Rais atupunguzie idadi ya wabunge kwa kutumia utaratibu atakaoona unafaa.Alifanya hivi kama Chairman wa CCM kwenye Nec na CC ikawezekana, sasa atusaidie na huku bungeni.Ni vile tu Rais wetu ni mtu wa kuchukua maamuzi vinginevyo kwa kulitegemea bunge sidhani kama Atcl ingekuwa inamiliki ndege leo hii mtakumbuka habari ya gati 13 na 14 pale bandarini.Fikiria wabunge zaidi ya 350 wanakaa Dodoma kwa miezi 3plus kujadili bajeti ya mwaka mmoja tu wakitumia mabilioni ya kodi za walalahoi.Chondechonde Rais Magufuli tuangalie walipakodi wako kwa jicho la huruma.Kama kule CCM imewezekana sidhani kama bungeni itashindikana ukizingatia ukweli kwamba kimaslahi bunge liko chini ya ofisi ya Waziri Mkuu.Mods tafadhali naomba msiunganishe uzi wananchi tujadili.Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom