Msolopagazi
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 663
- 153
Ombi kwa vyama vya wafanyakazi kesho ikiwa ni siku muhimu kwa wafanyakazi ni bora na watakuwa wamefanya jambo la maana na la kukumbukwa kwa kumuomba muheshimiwa rais
John Pombe Magufuli kuruhusu fao la kujitoa kwani sekta nyingi almost zote zimedorora sana hasa za binafsi kupelekea kupunguza wafanyakazi wao hivyo ni muhimu watu wakachukua michango
yao na kwenda kujiajiri kwani maisha ni magumu sana uraiani.
Pili kipindi hiki kimekuwa kigumu sana kupata ajira kwani watu wanaotafuta kazi niwengi kuliko walio na kazi imagine hawa elfu 9000 waliochishwa juzi nao pia wanaingia katika soko la kutafuta ajira ili waweze kujikimu na maisha baada ya kuachishwa serikalini.
Tatu kodi tunazokatwa wafanya kazi kwa mwezi ni kubwa sana ikilinganishwa na sekta zingine kama biashara na tunalipa bila delay au shuruti kwani zinakatwa juu kwa juu tofauti na mtu anaye fanya biashara au kilimo ambaye mpaka afuatwe pia ikumbukwe katika mafao ni mchango baina ya mfanyakazi na anaongezewa na mwajiri wake hakuna hata senti kutoka serikalini wala ruzuku kwa hiyo serikali ingetuachia sisi wafanyakazi wenyewe tukajipangia matumizi yetu badala ya serikali kutuingilia.
nne mimi binafsi niko kwenye sekta ya madini mazingira ya kazi ni magumu sana kwa hali ya kawaida huwezi kufanya kazi hadi kufikisha miaka 60 serikali iangalie takwimu za OSHA tangu migodi ianze kuna watanzania wengi sana wameathirika kutokana na uchimbaji wa madini hasa migongo sababu heavy duty mashine hazina shock up ni kiuno chako ndiyo spring masikio sababu ya kelele pia mapafu na magonjwa kama silicosis kwa sababu ya vumbi hivyo mtu kufanya kazi ya mining kwa zaidi ya miaka kumi kama mwalimu au nesi au afisa ugani ni uongo kwa haya machache chonde chonde ndugu zanguni naomba mtufikishie kilio chetu au nasikia mkulu mwenyewe anapita pita kwenye mtandao tunaomba mtusaidie wanyonge mliopa mtatusaidia. Asante