Mazingira
JF-Expert Member
- May 31, 2009
- 1,833
- 301
Mheshimiwa rais kama ambayo huwa unatoa msamaha kwa wafungwa, tunaomba utoe msamaha kwa watu waliosafiri nje ya katika miezi ya Novemba na Disemba 2015. Wako waliosafiri kabla ya tangazo halijawekwa vizuri. Wengine walidhani ni watumishi wa serikali kuu peke yake na wengine walidhani ni safari zinazotumia pesa za serikali tu peke yake. Kwahiyo kuna wengine walisafiri kwa ajili ya mafunzo ya muda mfupi na yalikuwa yamelipiwa kwa asilimia 100 na wafadhili na mafunzo hayo yamewaongezea ujuzi wa kulitumikia taifa kwa ufanisi zaidi lakini hivi sasa wanaandamwa na watawala kwenye ofisi zao au wizara mama kiasi kwamba wanaonekana kama ni wahalifu wa kupindukia. Kwa sasa hata kazi wameshindwa kufanya maana kila siku ni bughudha tu kwao na wanatishiwa sana na hawa watawala. Tunakuomba mheshimiwa rais uwasamehe ili waendelee kulijenga taifa na utoe onyo kali kwa atakayesafiri nje bila kibali. Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa msamaha wako. Asante.