Ombi kwa madaktari: Mgomo uendelee! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ombi kwa madaktari: Mgomo uendelee!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mafuchila, Feb 9, 2012.

 1. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2012
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Labda nitoe rai kwa madaktari, wengi tumeuunga mkono mgomo wao sio kwa sababu walikuwa wanataka nyongeza ya posho au kushinikiza watu fulani wajiuzulu. Dai la msingi la madaktari ambalo ndilo msingi wa uungwaji wao mkono na taifa zima lililalia kwenye ukweli kwamba walikuwa wakidai SERIKALI ITOE TAMKO JUU YA HATIMA YA AFYA YA MTANZANIA, KWANI UWEZO INAO WA KUTOA MADAWA; VITANDA NA KUBORESHA HOSPITALI ZETU pamoja na mazingira yao ya kazi.
  Dai hilo hapo juu lilipata uungaji mkono kutokana na ukweli kuwa Watanzania wanaokufa mahospitalini kwa magonjwa ya kutibika na ukosefu wa madawa ni mamia kwa maelfu. Naamini na bado nitaendelea kuamini mgomo sio chanzo cha vifo vya wagonjwa wetu bali ni mazingira duni ya huduma mahospitalini, hivyo hata mkirudi hamwezi kuokoa maisha yetu kama madai yenu ni ya kweli kuwa Muhimbili hakuna hata nyuzi za kushonea wagonjwa!!
  Vyovyote itakavyokuwa, kama madaktari wetu mtafikia maafikiano yoyote yale na serikali yasiyohusisha dai hilo hapo juu ambalo limetugusa wengi, sina hakika kama mtapata uungaji mkono mlioupata sasa hivi.
  OMBI: Kwa **** maisha yenu magumu kikazi na kuzorota kwa afya ya Mtanzania imetokana na ufisadi wa kupindukia, rushwa kulindana na kuzorota kwa maadili ya Uongozi, na matumizi ya anasa ya kupindukia ya viongozi wetu, nawaomba nipo chini ya miguu yenu mfanye haya yafuatayo:
  1. Muilazimishe serikali itangaze staili mbali mbali za malipo na viwango wa mishahara na malipo yote kwa waajiriwa wa serikali.
  2. Serikali iviwajibishe vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutufikisha hapa tuli, kwa kuwafanya raia wema kuishi maisha ya woga huku wakiwalinda Mafisadi kwa gharama za walipa kodi.
  3. Serikali itangaze na kuwachukulia hatua za kuwakamata na kuwafilisi mara moja wale wote waliohusika na kashfa kubwa za pesa na mikataba badhilifu ambavyo ndio vyanzo vya maumivu yetu watanzania wote bila kujali itikadi.
  4. Serikali itangaze mara moja mpango mkakati wa kutenganisha siasa na kuanza kuheshimu ushauri na uamuzi wa wataalam wetu ambao ndio waajiriwa wa serikali yetu.

  Ni matumaini yangu kama majadiliano ya mgomo wenu utaangalia mambo haya, basi bila shaka tutapata suluhisho la kudumu la matatizo yetu. Iwapo mtakubaliana na serikali kwa hatua za kuwaongezea vielfu kadhaa na kufukuza watu wachache hapo wizarani, mtakuwa mmejiahibisha mbele ya jamii na hamtaaminika tena!
  Watanzania wengi vifo vyetu vinawahishwa na MAFISADI na WANASIASA UCHWARA na kweli vifo hivi tumeshavizoea, Tunataka KUVIKOMESHA vifo hivi, Vifo tunavyosababishiwa na BINADAMU wenzetu kwa ajili ya kugharamia maisha yao ya ANASA.
   
 2. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2012
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  ndugu yangu, acha tu warudi watutibu wakati mengine yanajadiliwa

  Usiombe kukosa huduma ya matibabu ndugu
   
 3. MachoMakavu

  MachoMakavu JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kugoma bila kuwa realistic ni umbumbumbu uliopindukia!

  Kilio chao kimefika, wananchi pamoja na kuumizwa na mgomo huu tumewaunga mkono, mwisho serikali imesarim amri!

  Bado waendelee na mgomo?
   
 4. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  wananchi tunawashukuru kwa support yenu,it was the factor propelling our movement..bila nyinyi tungefyata mkia.big up sana watanzania kwa kuamka na kufanya maamuzi kwa kile mnachokiona ni sahihi na sio kwa kumsikiliza kiongozi ambaye anapotosha jamii
   
 5. S

  Shansila Senior Member

  #5
  Feb 9, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr,madai yenu yalikuwa yapi,mangapi?yametekelezwa mangapi na mangapi yako pending na mbona mmechomoa mapema huku mkiwaacha wanaharakati rumande?
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Ndugu warudi tu kuna mgonjwa alinitoa machozi yule alyekuwa amelala akadondoka chini na kujirudisha kwenye godoro hawezi
  Thanks god ijawa doctor wala nesi ..
   
 7. m

  massai JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  J.k.mwenyewe mwizi.alafu mnataka ashike wezi, labda ashike ulimboka na mama nkya hapo yuko fasta konoma,simmeona leo alivyofanya
   
Loading...