WISE BOY
JF-Expert Member
- Dec 26, 2011
- 782
- 244
Kwanza kabisa natoa angalizo kuwa mada hii haina malengo yoyote ya kukasfu wala kuchafua mtu yeyote..
Leo nikiwa nasafiri pembeni yangu walikaa wadada wawili waliojiweka kisasa na vimini vinavyo wanyima uhuru wa kukaa.
Kina dada walikua na mtoto mdogo wa umri kma wa miaka miwili hv, baada ya safari ndefu mtoto yule akajisaidia haja kubwa ndani ya pampas lkn harufu ilijaa gari zima.
Muda mtoto anajisaidia gari ilikua imesimama na abiria wameshuka, lkn kina dada hao hawakuutumia muda huo kumbadili mtoto bali waliendelea na mambo yao huku wakimshika mtoto kama "kinyaa flani", mtoto akilia bila msaada.
Kilocho nikera zaidi ni kitendo cha kusubiri abiria wote wamepanda ndipo wakaanza kumbadili mtoto, hiyo harufu sasa... Na watu wanakula take away zao...
Lkn waliniacha hoi zaidi pale walipomaliza kumbadili mtoto na kutupa ile pampas yenye kinyesi kwenye moja ya dustbin zilizo ndani ya gari, harufu yote ndani na wao wala hata hawashtuki...
Dada zangu, nawaombeni mjaribu kujifunza kuwa "Mama" pindi mnapozaa watoto, na pia mjitahidi katika suala la usafi.
Samahani kwa kuwachosha na maelezo marefu...