jiwe angavu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 19,058
- 35,838
Habari za asubuhi wakuu.
Naomba niende moja kwa moja kwenye dukuduku langu.
Katika kufuatilia na kufanya michakato mbalimbali katika uombaji wa mkopo nimekumbana na changamoto nyingi ambazo naamini wengi wetu waliofanya huu mchakato wamekutana nazo.
Kupitia mfumo mpya wa uombaji mkopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa njia ya mtandao (OLAMS), kuna changamoto nyingi zilizojitokeza katika kufanikisha mchakato huu kwa urahisi na kwa wakati, baadhi ya changamoto ambazo naamini wengi wetu wamekumbana nazo na wanaendelea kukumbana nazo ni kama zifuatazo.
Hivyo kupelekea wengi kushindwa kutuma maombi yao kwa wakati, sidhani kama ni lengo la serikali kuwasumbua na kuwahangaisha hangaisha wananchi wake hasa vijana wanaohitaji kujipatia elimu ya juu ili waweze kutimiza malengo yao kielimu.
hivyo kama nilengo la serikali kupitia bodi ya mikopo kuwawezesha viijana wa kitanzania kufikia malengo yao ya kusoma elimu ya juu,ni vyema suala la kuongezewa muda wa kuomba mkopo ungeongezwa ili kuwawezesha wengi kukamilisha huu mchakato kwa wakati kutokana na usumbufu mwingi uliojitokeza kupitia mfumo mpya wa OLAMS.
nawatakieni utekelezaji mwema wa majukumu yenu.
waziri wa elimu
Katibu mkuu wizara ya elimu
Mkurugenzi bodi ya mikopo

- Mtandao kuwa chini(networks Problems), hii ni changamoto kubwa sana, kuna kipindi cha siku mbili ama tatu mtandao wa website ya bodi na ule wa OLAMS haukupatikana kabisa.
- Ucheleweshwaji wa kupewa control number kwa jili ya malipo, hii kuna baadhi ya watu imewachukua zaidi ya wiki 2 hadi tatu tangu wafanye ombi la kuomba control number.
- Kushindwa kuprint au ku-apload forms kwa ajili ya kuzifanyia kazi au kuzituima kwenye mfumo.
- Kushindwa kufanya marekebisho endapo kwa namna moja ama nyingine mwombaji kakosea kujaza taarifa zake kwa usahihi.