marveljt
JF-Expert Member
- Jan 11, 2017
- 1,503
- 1,479
Wandugu nimeitoa mahali
Kwa miezi kadhaa sasa nimekuwa nikipata jumbe zihusuzo nchi yetu TANZANIA. Na baadhi nimezisema kanisani na tumeanza kuomba.
Niliahidi kuelezea vizuri kama BWANA akinipa kibali.
Na sasa BWANA amenipa kibali na ameniagiza kuwaambia watanzania.
Nitafanya kama nilivyoamriwa.
*Tanzania inakwenda kupitia kipindi kigumu, watu watakuwa na kipindi cha kukosa PESA, kutakuwa na njaa na wengi watakufa.
Matukio ya ujambazi na wizi yataongezeka, nchi itaharibika kwasababu ya njaa.
*Kisha nikaona vita kama vita ya ndani kwa ndani, na askari wengi wanakufa na hao askari wana mavazi yamepigwa chapa TANZANIA.
Na walikuwa wakishambuliwa wao pamoja na familia zao.
Na nikaona watu wanawavamia watu wameshika silaha na kuchukua pesa za watu wengine; watu matajiri, watu maarufu na ikiwemo viongozi wa serikali wanavamiwa na wengine wanatekwa. Nikamuita Mungu juu ya jambo hili nikaomba. Kisha__
BWANA akaniambia waambie watanzania waiombee nchi; andika mambo haya na uwafikishie ujumbe.
Watu wale watakaoomba ndio watakao nusurika ila yeyote atakayepuuzia jambo hili litamkuta.
Mungu akaniambia kuwa yeye ndiye aliyeifanya Tanzania kuwa nchi ya Amani. Hata wasiopenda Amani walipoingia Tanzania walikaa Kwa Amani. Yeye Mungu ndiye aliyezuia uharibifu usiipate Tanzania lakini kwasababu ya mambo yanayotendeka sasa, yanayoiharibu nchi; yeye Mungu atauachilia uharibifu.
**Mimi ndimi BWANA, nimeumba mbingu na ardhi; nimeumba nchi kavu na bahari na mimi ndiye nitakayeiharibu.
Nitaliharibu Taifa la Tanzania kwa kuwa limenitenda dhambi kwa kuwa maovu yamezidi.
Ila nitawabakisha wale wanichao na wenye kunijia mimi.
Asema BWANA Mungu**
Prophet Emmanuel MC.