madeinmusoma
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 326
- 391
Alipaata kuwepo bwana mmoja wa kuitwa Matonya David Paulo, mzaliwa wa kijiji cha Mpamatwa wilayani Bahi,Mkoa wa Dodoma. Aliishi Dar es Salaam kwa mara ya kwanza mwaka 1961.
Alikua maarufu sana hapa nchini kwa ajili ya kazi yake ya kuombaomba. Ilifika hatua hadi watu walikua wanataniana hasa wale wenye tabia za kuomba kuomba kwa kuitana Matonya.
Aliwahi kupingana na aliekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mzee Yusuf Makamba kuhusu kurudi kwao Bahi na kudai yeye ni mtoto wa mjini hivyo Makamba asingemuweza. Ilifikia hatua alipachikwa jina la utani kuwa yeye ni 'kiboko ya Makamba'. Hadi ndugu Professor Jay alimuimba kwenye mashairi ya wimbo wake Bongo Dar es Salaam akiwa amemshirikisha mwanadada LadyJaydee.
'Upinzani bongo haupo
Simba na Yanga,
Matonya na Makamba,
Site na wamachinga'.
Kutokana na mivutano iliyokuwepo kipindi hicho kati ya mzee Matonya na Mzee Makamba. Huku tena askari wa jiji maarufu 'City' japo wengi walikua wanatamka 'site' upande wao nao kilichimbika sana na wamachinga na mama Ntilie. Mixer kumwagiana majungu ya makulaji huku kukimbizana mpera mpera na bidhaa mikononi.
Hata hivyo mzee Matonya alifariki mwaka 2012 inasemekana akiwa masikini wa kutupwa, zaidi alijivunia miaka yake 90 aliyofariki nayo.