GE2025 Olivia Chagula: Rais Samia ametuhakikishia Usalama twende tukatiki

GE2025 Olivia Chagula: Rais Samia ametuhakikishia Usalama twende tukatiki

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Aliyekuwa mgombea ubunge wa viti maalumu kupitia Umoja wa Wazazi wa CCM, Olivia Chagula, amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 kushiriki uchaguzi mkuu kwa kupiga kura bila hofu akisisitiza kuwa usalama umehakikishwa kama alivyoeleza Amiri Jeshi Mkuu, Rais Samia Suluhu Hassan, katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana Oktoba 21, katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam

Chagula amesema, “Kama Dkt. Samia alivyosema, yeye ndiye Rais wa nchi (na Amiri Jeshi Mkuu), hivyo wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wajitokeze kwa wingi Oktoba 29, kwani usalama upo wa kutosha.”

Aidha, amesifu jitihada mbalimbali zinazotekelezwa na Dkt. Samia kupitia Ilani ya CCM, na amewataka Watanzania wenye nia ya kuandamana wasithubutu kufanya hivyo, kwani muda huu ni wa amani na maendeleo, si wa kushaabikia machafuko

Akizungumza Pktoba 21, 2025 na wakazi Dar es Salaam, Rais Samia ambaye pia ni Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), aliwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29 huku akieleza kuwa vyombo vya usalama nchini vimejipanga kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa amani na utulivu

Alisisitiza kuwa maandamano yatakayokuwepo ni ya watu kupiga kura pekee na si mengineyo



Chanzo: TBC DIGITAL
 
Kwa lavel ya urais sijaona mgombea anayetoshea kuwa rais....wote akili ndogo hasa huyo daktari wa mchongo, so sitapiga!.

Salum Mwl toka kampeni zimeanza hajawahi kuthubutu kumkosoa chura kiziwi jukwaani hata mara moja jukwaani...chaumma ni tawi la ccm!.
 
Back
Top Bottom