Ole wako usipojali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ole wako usipojali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by zaleo, Sep 23, 2012.

 1. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Kutoka Yahoo friends. Nimeinasa ikizunguka.

  NIMEWATUMIA TAARIFA HII, ILI PAMOJA NA UKARIMU NA UPENDO TULIONAO TUWE MAKINI NA WADADISI!!!!  [TABLE]
  [TR]
  [TD]JUMAPILI ILIYOPITA NDUGU MMOJA ALIKUWA KWENYE DALADALA AKITOKEA UBUNGO KWENDA TEGETA.BASI LILIPOFIKA MWENGE ABIRIA WALIONGEZEKA NA WENGINE WAKAWA WAMESIMAMA,KATI YA WALIOSIMAMA ALIKUWAPO MZEE MMOJA ALIYEKUWA NA HAND BAG KAMA TUNAZOBEBEA LAPTOP HIVI, YULE MZEE ALIMUOMBA MJOMBA WANGU AMSAIDIE KUMSHIKIA BAG LAKE KWA KUWA YEYE ALIKOSA SITI, BILA YA KUSITA AKAAMUA MUMSAIDIA KALE KA BAG" BAADA YA VITUO VIWILI YULE JAMAA MWENYE KA BAG; ALITEREMKA BILA MJOMBA WANGU KUMUONA NA YEYE HAKUWA NA WASIWASI KWA KUWA ALIJUA MWENYE MZIGO AKITAKA KUSHUKA ATAUCHUKUA TU MZIGO WAKE.

  KABLA GARI HAIJAFIKA KITUO CHA TATU ILISIMAMISHWA NA WATU WALIOJITAMBULISHA KWAMBA WAO NI ASKARI POLISI WAPELELEZI KWAMBA KUNA KITU WANAPELELEZA,WAKAWAAMURU ABIRIA WOTE WATEREMKE KWENYE GARI,WALIFANYA HIVYO MMOJA WA WALE POLISI, WALIMFUATA MJOMBA WANGU NA KUMUULIZA 'NA WEWE KWENYE BAG LAKO KUNA NINI? AKAWAJIBU BAGI SIYO LANGU KWA HIYO SIWEZI JUA NDANI KUNA NINI!! WAKAMUULIZA TENA, MWENYEWE YUKO WAPI TUONESHE" AKAANGALIA KATI YA WALE ABIRIA WENZAKE HAKUMUONA.

  WAKASEMA FUNGUA TUONE KUNA NINI NDANI, WALIPOFUNGUA WAKAKUTA KUNA SILAHA AINA YA PISTO.ALIPOJARIBU KUJITETEA WAKAMWAMBIA TWENDE KITUONI UTAENDA KUJIELEZA HUKO. BASI LIKARUHUSIWA NA YEYE WAKAMPELEKA POLISI, WAKIWA NJIA WAKAMWAMBIA KAMA ANATAKA WAMWACHIE ATOE LAKI NANE 800,000/= VINGINEVYO WATAMUUNGANISHA KATIKA KESI YA WIZI WA KUTUMIA SILAHA,AKAWAAMBIA SINA HIZO PESA NA SIWEZI KUTOA MPAKA SASA BADO YUPO NDANI.HII INATUKUMBUSHA KWAMBA NI KWELI TUNAPENDA KUWASAIDIA WATU ILA TUWE MAKINI NA MISAADA TUNAYOITOA. MZEE ALIKUWA NA NIA NJEMA KABISA YA KUTOA MSAADA ILA MSAADA UMEMGHARIMU MAISHA. Mwisho napenda kuwatahadharisha watu wote tuwe makini na watu tusiowajua,

  MTUMIE NA MWINGINE UJUMBE HUU

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2012
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Asante kutukumbusha tena.
   
 3. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Asante kwa taarifa. Uhuni huu pia unatumika kusafirisha maawa ya kulevya. Usikubali mtu akuombe umshikie /umsaidie mzigo, mfuko etc, hasa mnapotaka kupita uhamiaji. kama kuna madawa ya kulevya anakusakizia wewe. Ukishikwa, anakuruka. Ukipita anachukua mzigo wake. Tuwe macho na ukarimu.
   
 4. m

  mkupuo JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Asante mkuu kwa kutujuza. Sisi wa mikoani uzi huu ni muhimu sana.
   
 5. E

  Emmanuel_mtui Member

  #5
  Sep 23, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni vyema ulivyotujuza maana, haya mambo ni makubwa,
   
 6. W

  Wellwell Member

  #6
  Sep 23, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ohh!!! maskini mjomba!!! huruma imemgharimu jamani. Yawezekana hizo pesa hana kweli. Anyway, mola wake atamsaidia kwani alikuwa mtu mzuri tu.

  Asante kwa kutujuza makubwa haya ya walimwengu!!!
   
 7. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Ina maana polisi walijua kabisa kuwa basi la Ubungo - Tegeta kuna mtu alikua na silaha, kwa nini tokea nikae Dar muda wote hata kama nimezaliwa Katavi sijawai kuona kisa cha namna hiyo.In short kama kisa hicho ni cha ukweli huyo aliekuwa na bastola alikuwa mjinga sana kwa nini asingeshukia hata kituo cha pili kutoka Mwenge akachukua hata bajaji ama boda boda.Anyway hata kama napinga kiaina lakini ujumbe nimeupata ntakuwa makini
   
 8. K

  Kiduku JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 480
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huo ni mchongo wa hawa polisi wa tz
   
Loading...