Ole ole kwangu na nchi yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ole ole kwangu na nchi yangu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bakuza, Jun 25, 2011.

 1. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 488
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  NASEMA OLE OLE KWANGU NA NCHI YANGU

  Sina hakika kama kweli ,mimi ndimi kiongozi hasa mchaguliwa wa Wawadanganyika,kama ndiye basi ole wangu na kama siye basi ole wangu zaidi maana yawezekana nimeingia kimagumashi nikitumia mainteligensia wa uchakachuzi wa matokeo na vyombo vya kibabe.
  Ole wangu ninayechekelea kuona vyombo vyangu vya kibabe na mainteligensia wangu wakihujumu uhai wa walalahoi watoto wa masikini na kuwaita wavamizi na majambazi wakubwa kwa sababu ya umasikini wao na kulinda maslai ya wachache/mafisadi.
  Ole wangu mimi niliyeacha misingi ya utawala bora na usawa aliyoacha Mwalimu japo amekuwa mwalimu wangu miaka mingi na kuwa na tamaa ya mali iliyopindukia.
  Ole wangu niliyeacha kuwawajibisha mafisadi na watumia madaraka vibaya kwa sababu ni maswahiba zangu.
  Ole wangu maana sikuwajari wavuja jasho wa nchi hii wanavyoumizwa na mfumuko wa bei uliokithiri wa vyakula,mafuta,huduma zajamii na bidhaa nyinginezo zote.Huku nikiwakejeri eti “wapiga kelele wapinzani hao hawana sera”
  Ole wangu mimi niliyewadangaya Wadanganyika kwa ahadi rukuki ambazo hazitekerezeki.
  Ole tena nasema Ole wangu nisivyohangaikia wagojwa mahosipitalini ili wapate huduma bora,na kuacha kuwalaza chini.NInachofanya ni kubariki posho za vigogo wa serikali na wabuge nami nikiongeza safari nyingi ugaibuni kwenda kuleta wakoloni wengine maana sisi ukoloni wetu hautoshi kwa ngozi zetu nyeusi.
  Ole wngu mimi ona wale hawajui watapata wapi mlo wa leo wala kesho,na wengine wale pale wanaumwa hawana pesa ya kuchangia matibabu,hata hawa hapa hawajui watasomaje japo elimu ya kata wanayopata kata za mbali bila nauli za kwenda huko.
  Ole mimi ninayefarakanisha walalahoi na walinzi wa usalama wao na wao na marapurapu (mali) yao.
  Ole wangu niliyehaidi kuuondoa umasikini na kuleta maisha bora huku sijui kwa nini wao na nchi yao ni masikini.Huku mimi na wenzangu/maswahiba zangu tukiwa na utajiri uliopindukia,sijui naota lakini nadhani niko sijalala labda kama waweza ota ukiwa macho.
  Ole,Ole,niliyetoa ahadi ya ajira rukuki ,na nikafanikiwa kuongeza wapiga debe,wabwia unga,wavuta bangi na mgambo wa jiji,ambao kazi yao ni kunyanyasa wafanyabiashara wadogowadogo mali zao kwa mbwembwe nikiwaita wamachinga.
  Ole wangu kwa kutowashugulikia waleta unga wakubwa japo majina kama sikosei niliyapata kutoka kwa wenye uchungu na nchi ya Wadanganyika,si hao tu na mafisadi sitaki kusikia kelele maana wakiumizwa wao name naweza kufikiwa ikawa balaa.
  Ole kuu kwa kutotimiza kiapo cha katiba niliyohaidi kuilinda na kuitekeleza,sasa nataka kuunda ya kwangu itakayolinda maslahi yangu,maswahiba zangu na zaidi chama changu kinachoniweka na kunipa mwanya huo.Wadanganyika mtakoma miaka iliyobaki.Ila sijui naona kidogo kidogo wanasutuka sababu ya huyu muelimishaji anaitwa sijui dokta maslaa,simpendi huyu anataka kuharibu tonge langu
  Ole wangu maana pesa ya DEC hawataipata ng’o,hata ile waliyorejesha waoga wachache katika fuko la EPA sirejeshi nitawazuga tu mpaka naondoka kitini.
  Mungu nihukumu kwa hayo ila Wadanganyika wahukumiwe zaidi maana wana macho hawaoni wana masikio lakini hawasikii wameifanya mioyo yao kuwa migumu japo ukweli wanaelezwa hawataki kuelewa.
  JK.NYERERE RUDI UONE KILIO HIKI TUNALIA WATANZANIA
  Natoa chozi la simanzi ninapoipitia katiba ya kwanza ya CCM baada ya kuvujwa TANU na ASP katika mkutano mkuu wa tarehe 21/01/1977 mjini Dar es salaam.Ulihudhuriwa na wajumbe wa vyama hivyo pamoja na Ndugu Julius Kambarage Nyerere Raisi wa TANU na Ndugu Aboud Jumbe Raisi wa ASP,ambao kwa pamoja waliamua na kutamka rasmi kuvunjwa kwa TANU na ASP na kuundwa kwa CCM ifikapo tarehe 05/Feb 1977.
  Nikienda kipengele “c” cha azimio hilo chozi linanilenga lenga kuililia Tanzania.Nanukuu “Tumeamua kwa pamoja kuunda chama kipya cha kuendeleza mapinduzi ya kijamaa nchini Tanzania na mapambano ya ukombozi wa afrika juu ya misingi iliyojengwa na TANU na ASP.Chama tunachokiunda tunataka kiwe chombo madhubuti katika muundo wake na hasa katika fikra zake na vitendo vyake vya kimapinduzi vya kufutilia mbali aina zote za unyonyaji nchini ,na kufutilia mbali aina zote za unyonyaji nchini na kupambana na jaribio lolote lile la mtu kumwonea mtu au shirika au chombo cha nchi kuonea na kudharirisha wananchi,kudhoofika uchumi,au kuzorotesha maendeleo ya Taifa.Chama tunachokiunda tunataka kishike barabara hatamu za uongozi wa shughul zote za umma kwa maslahi ya wakulima na wafanyakazi wa Taifa letu”

  Na ukiangalia malengo namba 8 mpaka 16 ya kuanzishwa kwa CCM utachoka ukilinganisha na leo hii nchi inavyopotea.
   
Loading...