Ole Mushi: Kilichowachelewesha wana wa Israel kufika nchi ya ahadi ni kutokusikilizana

DIZZO MTAWALA

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
240
767
Na Thadei Ole Mushi.

Kilichowachelewesha wana wa Israel kufika nchi ya ahadi toka utumwani ni masikilizano tu. Kutoka Misri hadi Israel hazifiki KM 700. Lakini walitumia muda wa miaka 40 kufika Israeli. Musa alienda kuwaokoa akiwa kijana kabisa lakini alizeekea njiani na kufa kabla hajafika Israel. Kama walikuwa wanasikilizana wangetumia hata nusu ya mwaka wangefika. Lakini walikuwa wanafika mahali wanaanza kulaumiana,kugombana na hata kumkufuru Mungu kwa matendo yao.

NATAKA KUZUMGUMZA NN?

Nimesoma alichoandika Mh Hamidu Bobali Mbunge wa Mchinga kuhusu Korosho na manunuzi yake huko kusini naona Kiza. Ameandika :-

"Maumivu tunayoyapata wakulima wa korosho ni makubwa yasiyo na kifani na maelezo.....

Jimboni kwangu Mchinga hakuna mkulima wa korosho hata mmoja alielipwa pesa kiasi chochote kile....

Korosho zilizopo Maghalani kwetu ambazo hazijasafirishwa ni nyingi kuliko zilizosafirishwa kufikishwa ghala kuu kusubiri tathimin na zoezi la kukagua mashamba....

" Ewe Mola , Mimi mbunge wa wananchi wa Jimbo hili, nainua mikono juu na kwa sauti ya unyenyekevu kukukabidhi kilio cha wapiga kura wangu."..

Hali ya maisha ni ngumu kuliko maelezo.."

Mwisho wa Kunukuu.... Kama ni kweli hali ipo hivi lazma tukubali kuna mahali hatukusikilizana. Kuanzia bungeni hadi njee ya Bunge. Hiki ndicho kilichowachelewesha wana wa Israel Kufika haraka Misri.

Kutokusikilizana kunatucheleweshea sana kufika kwenye maendeleo. Laiti kama tungesikilizana kuanzia ndani ya Bunge sasa hivi Korosho zingekuwa zimeshaisha huko kusini na watu wanaendelea na maisha yao.

#Tuzungumzie na hili...Kuna middle man ambao walikuwa wamejihusisha na biashara ya Korosho hawa hawana mashamba ni kama wale wanaokwenda kununua Mikungu ya Ndizi kule Kilimanjaro na kuileta hapa Buguruni kwenye mnada hawana mashamba ila wao ni kiungo kati ya Mkulima na Mlaji. Ni makundi matatu yanayotegemeana na wote ni watanzania huko kusini nasikia kama huna Shamba ni sawa na kwamba huna Korosho. Kuna watu walikopa kwa ajili ya biashara hii hawa wanaenda kufilisika muda si Mrefu tunaendelea kutengeneza watu tegemezi kwenye jamii kuliko kuzalisha wanaotegemewa.

#TUNACHOKIFANYA.

Kuna kanuni huwa inasema wagawanye halafu waongoze (Divide and Rule). Hii kanuni awamu hii tumeiacha au aidha hatujui kuitumia. Angalieni haya jifungieni hapo Lumumba mtafakari maneno haya:-

1. Kwa sasa hivi kupitia sheria zinazotungwa na bunge na kutokusikilizana kwetu waandishi wote ukiachana na jamvi la Habari na Tanzanaite wanasikilizana na wapo against sisi ccm fuatilieni mtaliona. Tuliwaunganisha bila kujua.

2. Watumishi wa Serikali kutokupandishwa mishahara pamoja na kanuni mpya ya Mafao imeshawaunganisha wafanyakazi wote. Hatutaki kuwasikiliza........huko mbeya Uyole kuna afisa toka kwenye mifuko yetu ya Hifadhi alienda kuwapa semina ya kikokotoleo kilichompata anajua mwenyewe..... Watu wana hasira sana.

3. Tumewaunganisha tuliowatumbua katika nafasi mbalimbali.

4. Tunmewaunganisha wakulima mkulima wa Korosho Analia na wa Mbaazi Analia. Hawa wa Mbaazi tuliwaambia wazile sijui kama wameshazimaliza.

5. Tumewaunganisha wapinzani wetu kisiasa kwa sheria Zetu na Operation Zetu. Vyama karibia vyote vinaongea Lugha Moja

6. Tumewaunganisha vijana wanaohitimu fani mbalimbali kwenye vyuo vyetu. Zamani wale waliokuwa wanamaliza ualimu walikuwa wanatusaidia kuneutralize hali ya mambo huko mtaani. Sasa hivi wote wanazurura na bahasha awe ni mwalimu au ni aliyesomea political science.

7. Mwaka Jana tulivurugana na madhehebu yetu haswa kwasababu ya nyaraka zilizoandikwa. Tuliwaunganisha wote KKKT,RC na madhehebu mengine wakawa wanaongea Lugha moja.

8. Kuna wale wa vyeti fake.... Nao wameshatangulia kwenye Behewa muda mrefu wanaendelea kusubiri wengine wanaoungashwa na kupewa kifurushi chao cha kujiunga.

9. Pale Kimata tuliwabomolea nyumba lakini kule mwanza tukawaambia kwa kuwa mlitupigia kura hatutazibomoa. Hawa wa Kumara na maeneo mengine wakajua ni chuki dhidi yao wala si Sheria nao wameshapanda kwenye behewa.

10. Kuna waliokosa mikopo navyuoni hawa wanalia kilio kimoja na wanaolazimishwa kukatwa asilimia 15 badala ya nane......

Mambo ni Mengi mno...... Makundi yote Haya tunayoyaunganisha yanapanda Behewa moja yote yanaongea Lugha Moja against chama changu. Ukiniambia tunafikiria nini nitakuambia Sijui.

Katika hali kama hii juhudi za Maendeleo ya #VITU ya Serikali hayawezi kuonekana. Mkulima wa Korosho sasa hivi huwezi kwenda kumwadithia maswala ya SGR au ndege akakuelewa vivyo hivyo kwa makundi mengine.

Tumesahau ustawi wa Jamii.....

Hii ndio Miaka 40 ya wana wa Israel kutoka utumwani, tuna Miaka zaidi ya 50 ya Uhuru tunakwenda mbele tunarudi nyuma kwa sababu ya kukosa masikilizano. Miaka 50 iliyopita hizi ndege zilikuwepo, Reli zilikuwepo, viwanda vilikuwepo, nk.

Kutokana na kukosekana kwa masikilizano tupo kama tumepata Uhuru Jana. Awamu itakayokuja sintoshangaa wakianza na mambo Mengine na haya yaliyotengenezwa miaka hii yakatupwa na kuishilia kabisa.

Ole Mushi.
0712792602
 
Jiwe ni sikio la kufa. Serikali yake imejaa unyang'anyi uliopindukia. Kila kundi katika jamii linalalamika, si watumishi, wafanyabiashara na hata wakulima. Kila unapokwenda ni malalamiko dhidi yake. Furaha imetoweka machoni kwa watanzania walio wengi. Uongozi umemshinda mazimaaa! Huyu si mtu wa kutawala vipindi viwili. CCM msaidieni kwa kumweka pembeni kwenye kura za maoni 2020, angalau mumshikishe kijiti Mh. Membe. Jiwe amezidi na anaendelea kuharibu. Hatufaiiiiiiiiiii na hana hadhi ya kuwa mkuu wa kaya.
 
Back
Top Bottom