Ole Millya kuvuliwa uanachama CCM

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054
Na Said Njuki, Arusha

MGOGORO ndani ya CCM Mkoa wa Arusha umeshika kasi mpya baada ya Kamati ya Usalama na Maadili na Kamati ya Siasa za chama hicho mkoa kudaiwa kumvua uanachama Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) Mkoa, Bw. James Ole Millya.

Pia vijana wengine watano wa umoja huo wanaodaiwa kuwa vinara wa mgogoro nao watakumbwa na rungu hilo baada ya kamati hizo kutoa mapendekezo ya kufukuzwa uanachama kwa kitendo chao cha kushadadia kuondoka kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Bi. Mary Chatanda.

Habari kutoka ndani ya vikao hivyo ambazo zimethibithswa na baadhi ya viongozi wa chama hicho kwa sharti la kutotajwa majina, zimedai Kamati hiyo iliyoketi mwishoni mwa wiki ilitoa mapendekezo yake kuwa Mwenyekiti huyo anayedaiwa kuwa kinara wa mgogoro huo pamoja na vijana hao avuliwe madaraka.

Vyanzo hivyo vilidai kuwa kikao cha kamati hiyo pia kilihudhuriwa pia na wajumbe kutoka Kamati ya Maadili ya Taifa ikiongozwa na Kanali Mhando na wajumbe wawili kutoka UVCCM Taifa ambao ni Bw. Seif Malinda na Mzee Mipoko kilichokaa kuanzia asubuhi hadi usiku wa manane.

Mapendekezo hayo baada ya kuridhiwa na wajumbe hao yalifikishwa katika Kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa, kilichofanyika siku moja baadaye na kuridhia mapendekezo hayo, hivyo kusubiri kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa kinachotarajiwa kukutana Jumamosi wiki hii kwa ajili ya maamuzi zaidi.

Vyanzo hivyo vimewataja majina ya vijana watano kati ya 11 waliohojiwa siku hiyo, kufuatina mgogoro unaotokana na falsafa mpya ya CCM ya kujivua gamba ambapo makada waandamizi wa chama hicho, aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, Mbunge wa Igunga, Bw. Rostam Aziz na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Bw. Andrew Chenge wanashinikizwa kuachia ngazi zao.

Baadhi ya sababu zilizoelezwa za kuwajibika kwa Bw. Milly Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Bi. Mary Chatanda.

Wadadisi wa mambo ya siasa mkoani hapa wameeleza ya kuwa iwapo hatua hiyo ya kuwavua uwanachama vijana hao itatekelezwa itazidi kuchochea na kupanua mgogoro huo ambao ungeweza kutatuliwa kwa njia za kidiplomasia na kupunguza ufa ndani ya chama hicho.

Lakini kundi lingine linatoa matamshi mazito dhidi ya makada hao na kueleza kuwa wanapaswa kuwajibika kwa tuhuma zinazowakabili na kwenda mbali zaidi na kumtaja Bi. Chatanda ni lulu ya chama mkoani hapa na hapaswi kuondoka.

GAZETI HURU LA KILA SIKU:: Ole Millya kuvuliwa uanachama CCM
 
Back
Top Bottom