Ole Medeye umeamua kumuasi Mungu?

Ole Medeye umeamua kumuasi Mungu?

MwanaHaki

R I P
Joined
Oct 17, 2006
Posts
2,401
Reaction score
710
Ole Medeye umeamua kumuasi Mungu?

Na Msema Kweli

Si kawaida yangu; narudia tena; kunukuu maandiko takatifu katika kazi yangu hii – isiyo rasmi, kwani sijaajiriwa kwayo – ya uandishi. Lakini leo nimelazimika kufanya hivyo kwa “kutimiza wajibu”, kama Mkristo.

Kila ninapolala usiku, kwenye Sala ya Jioni, kuna sala mbili ambazo ni sehemu ya sala hii muhimu. Ninazinukuu hapa kwa faida ya wale wasiozijua au waliozisahau ili wapate kuzikumbuka:
“SALA YA MAPENDO
Mungu wangu, nakupenda kwa nafsi yangu zaidi ya chochote; kwani ndiwe mwenye kupendeza. Nampenda jirani yangu kama nafsi yangu kwa ajili yako. Amina

“KUJUTA DHAMBI
Nakuungamia Mungu Mwenyezi, nanyi ndugu zangu, kwani nimekosa mno kwa mawazo, kwa maneno, kwa vitendo na kwa kutotimiza wajibu...”

Hapa kuna mambo mawili makuu; mosi, kumpenda jirani yangu kama nafsi yangu; na pili, kutenda dhambi kwa kutotimiza wajibu.

Katika mafundisho yake, Biblia inawaonya Wakristo wote na watu wa mataifa, kwamba ole wao waandishi na mafarisayo watakaoshindwa kutimiza wajibu wao kwa kutokemea maovu yanapotokea duniani, kwani, dhahiri, huo ni “uasi” kwa Mungu.

Mimi “sikufundishwa” kuandika; hii ni mojawapo ya talanta zangu nilizopewa na Mungu, kwa hiyo nisipoitumia kuielimisha jamii inayonizunguka, bila kujali itikadi za kisiasa, mifungamano yoyote, imani za kidini, n.k., hakika nitakuwa ninamkosea Mungu kwa kushindwa kutimiza wajibu wangu huo. Mungu hakupi talanta ili ukikalie kitako; anakupa ili uitumie, lakini uitumie kwa makini na uhakikishe unatafakari kabla ya kuitumia.

Kama wewe ni daktari, dereva, rubani, mhandisi, kiongozi wa kitaifa, mwanasiasa, n.k., unapaswa kutimiza wajibu wako ipasavyo bila kukiuka maadili ya kazi yako na, muhimu zaidi, bila kumuasi Mungu.

Ndugu zangu, hivi kuna siku yoyote ile ambayo mlikaa na kutafakari kuhusu nani haswa ni “jirani” yenu? Najua hili ni swali gumu kulijibu; wengi ambao wameulizwa walijibu: Jirani yangu ni mtu yeyote yule ambaye ninaishi naye ama nyumba inayopakana na nyumba yangu, au kwenye mtaa ninaoishi mimi.

Kama ungekuwa ni mtihani, wengi wangefeli, kwa kuwa hiyo ni maana finyu ya neno hilo, ambalo tukiamua kulichambua kikamilifu, tutaandika vitabu lukuki. Lakini kwa leo sitaandika sana, ila, mtaniwia radhi kwa kuamua kunukuu tena Biblia Takatifu.

Katika somo la Jumapili, Julai 14, 2013 (la Kanisa Katoliki), wakati marudio ya uchaguzi wa madiwani katika kata nne za Arusha, yaani, Kimandolu, Olorien, Themi na Kaloleni, ukiendelea kwa amani mpaka sasa pasi na kuwa na vurugu au fujo zozote, ninalazimika kunukuu maandiko haya takatifu ya Injili ya Luka, 10:25-37, kama ifuatavyo:
“Siku ile, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu, akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele? Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje? Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili yako yote; na jirani yako kama nafsi yako. Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi. Naye akitaka kuidai haki, alimwuliza Yesu, Na jirani yangu ni nani? Yesu akamjibu akisema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa. Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipitia kando. Na Mlawi vivo hivyo, alipofika pale akamwona, akapitia kando. Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia, akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza. Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na chochote utakachogharimiwa zaidi, mimii nitakaporudi nitakulipa. Waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake, yule aliyeangukia kati ya wanyang’anyi? Akasema, Ni huyo aliyemwonea huruma. Yesu akamwambia, Enenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo.”


Injili hii inatufundisha mambo makuu kadhaa kuhusu tafsiri sahihi ya nani unapaswa kumwita jirani yako, lakini yaliyo muhimu zaidi ni haya yafuatayo: Mosi, jirani yako si lazima awe mtu anayeishi jirani nawe au mtu unayemfahamu; kwa kumpenda Mungu wako, jirani yako ni mtu yeyote yule ambaye unakutana naye, haswa yule ambaye yuko katika shida, na kwa mapenzi yako kwa Mungu, unamsaidia bila kujali alikotoka. Kwenye injili hii, Yesu anatufundisha kwamba jirani yako anaweza kuwa hata adui yako. Yule aliyeangukia kwa wanyang’anyi alikuwa Muisraeli, lakini Waisraeli wenzake – ambao wamezishika na kuzifuata amri na sheria za Mungu, ambao wanapaswa kuziishi kwa vitendo, hawakumsaidia – bali alisaidiwa na Msamaria, ambaye alikuwa adui yake. Wakati huo, Wasamaria na Waisraeli walikuwa maadui dhahiri.

Pili, hata katika kumjibu Yesu, yule mwana-sheria Muisraeli alishindwa kusema “Ni huyo Msamaria”, bali “Ni huyo aliyemwonea huruma.” Wangapi kati yetu, walio au wasio Wakristo, huwa wanakubali kusema ukweli na kuwapa heshima zao wale wanaotenda mambo mema?

Tatu, kwa mujibu wa tafsiri pana zaidi ya hili neno “jirani”, ni kwamba, mtu yeyote yule anayeamrisha – kwa nafasi yake kwenye jamii, akiwa kama kiongozi wa kijamii au kiserikali – watu wake kuwabagua watu wengine kutokana na itikadi zao, makabila yao, dini zao, rangi zao, n.k., hakika anakuwa amemuasi Mungu, kwani Mungu ametuamrisha “tupendane kama nanyi nilivyowapenda” na kila siku tunasadiki kuwapenda majirani zetu kama nafsi zetu.

Kwa hili, kama mwandishi, nalazimika kuwajibika – katika kumpenda Mungu wangu – kukemea kwa nguvu zangu zote kitendo kilichofanywa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Mh. Goodluck Ole Medeye (MB-CCM), cha kuwaamrisha “wazawa” wa mkoa wa Arusha kuwabagua wahamiaji “Wachagga”, na kuhakikisha hawapati nafasi yoyote ile ya uongozi, akimlenga mbunge wa CHADEMA, Godbless Lema (MB-CHADEMA), ambaye ni mbunge wa kuchaguliwa wa Jimbo la Uchaguzi la Arusha Mjini, ambaye tangu kuchaguliwa kwake amekuwa akifaniwa mizengwe lukuki ili tu aachie ngazi. Lengo la ubaguzi huu lilikuwa kuhakikisha kwamba Wamaasai, Waarusha na Wameru, katika kile Ole Medeye alichokiita “kuirudisha Arusha kwa wazawa”, ni kutumia mbinu chafu za ubaguzi wa kikabila kwa kuwagawa watu na kuhakikisha kwamba CCM pekee inafanikiwa kwenye uchaguzi huo, ili kiti cha Meya wa Jiji la Arusha kinabaki CCM.

Sisi Watanzania, kimsingi, hatuna hulka ya kubaguana, wala hatujawahi kuwa na hulka hiyo. Muasisi wa taifa hili, Mwalimu Nyerere, alifanikiwa kutuunganisha tusahau makabila yetu na kuwa wapenda amani na wenye mshikamano na umoja. Kwa kuhakikisha kuwa tuna lugha moja, Kiswahili, amani ilistawi na kushamiri hapa nchini. Mwalimu, ambaye alisikika akisema kuwa, awapo safarini, alitembea na vitabu vitatu tu: Biblia, Mwongozo wa Chama, na Azimio la Arusha; hakika alikuwa mcha Mungu, na kwa kuwa alimpenda Mungu kwa akili yake yote, roho yake yote, nguvu zake zote; vivyo hivyo alimpenda jirani yake kama nafsi yake.

Leo hii tuna kiongozi, wa kitaifa, wa kuchaguliwa na Watanzania, anawafundisha Watanzania walioko katika kundi moja, kuwabagua Watanzania wengine waliopo kwenye kundi lingine, kwa misingi ya kabila lao. Tangu lini Wamaasai, Wameru na Waarusha wamekuwa maadui wa Wachagga? Au siku hizi CHADEMA ni kabila?

Ninamshangaa Mh. Goodluck Ole Medeye, ambaye ukitafsiri jina lake la kwanza kwa lugha ya Kiswahili utapata maana “Bahati Nzuri”, akiwachochea ndugu zake, wawachukie Wachagga, ikiwezekana hata kuwaua kwa kuwawekea sumu kwenye maji au chakula, n.k.

Hii ni sumu mbaya kuliko zote; huu ni uasi; uasi uliovuka mipaka, ambayo ni dhahiri kwamba, sio tu kwamba Mh. Ole Medeye amemuasi Mungu wake, kama Mkristo, bali pia ameliasi Kanisa kwa kumkumbatia Shetani. Kabla ya kwenda kufanya ibada kanisani Jumapili, anapaswa kuungama dhambi zake hizi kwa Paroko au Kasisi wake, na kutubu, kwani matokeo ya uasi huu na madhara yake ni makubwa kuliko anavyofikiria.

Si nia yangu kuchanganya dini na siasa, lakini kwa leo – mtanisamehe – nimelazimika kufanya hivi, kwa kuwa hata Waislam wameamrishwa kukemea mambo maovu kwa nguvu zao zote. Sijawasikia Masheikh wakilaani kitendo cha Ole Medeye kuwashinikiza wazee wa kimila wa Kimaasai kuwabagua Wachagga, alichokifanya kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Arusha Technical College siku chache zilizopita wakati wa maandalizi ya marudio ya uchaguzi huo wa madiwani, huko Arusha, ambao uliahirishwa kutokana na tukio la kulipuliwa kwa bomu kwenye mkutano wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi huo, uliofanyika kwenye viwanja vya Soweto. Bomu hilo liliua Watanzania wanne na kujeruhi wengine zaidi ya 70. Mungu awalaze mahala pema watu wote waliokufa kutokana na bomu hilo; awape ahueni wagonjwa wote ambao bado hawajapata nafuu na wamelazwa hospitalini. Amina.

Watanzania wenzangu, sisi hatuna itikadi za kubaguana. Kama alivyotufundisha Mwalimu Nyerere, ubaguzi ni sawa na dhambi ya kula nyama ya mtu; ukianza huwezi kuacha.

Leo utambagua Mchagga, kesho utambagua Muislam, keshokutwa utawabagua Wahindi na Wazungu; hutaacha. Shetani atakuganda, utapata shida sana kujinasua. Utasababisha machafuko, vurugu, fujo na vita. Hivi mpaka leo hatujajifunza madhara ya ubaguzi kutoka kwa majirani zetu wa Burundi na Rwanda?

Ole Medeye, tafadhali usitupeleke vitani! Usihatarishe amani ya nchi yetu!

Mungu ibariki Tanzania. Wabariki Watanzania wote. Dumisha amani, umoja na upendo wetu daima! Ninaomba haya kwa njia ya Yesu Kristo Bwana Wetu! Amina!
 
Andiko zuri lakini hoja ya msingi ni hearsay and bruit.

Imani ya dini isikufanye ukawa na imani kwa kila kile kinachokuja mbele ya masikio yako bila kukifanyia uchambuzi yakinifu na matokeo yake unajikuta unaangukia kwenye maandiko ya Exodus 20:16 which says, "You shall not give false testimony against your neighbour".
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    51 KB · Views: 193
Kaka pole sana kwa maumivu yanayoukabili moya wako hasa wakati huu ulipokuwa ukiandika huu waraka. hao ndio CCM halafu kesho utawasikia kwenye majukwaa wakisema CHADEMA ni wakabila. Ila neno ni Moja tu kutoka kwangu; EE BABA WASAMEHE MAANA HAWAJUI WAFANYALO. Pia Mungu anahuruma sana ndio maana hata mzaburi akamshangaa kwa kuumwambia;KAMA UNGEHESABU MAOVU HAKUNA AMBAYE ANGESIMAMA,Hata yule mwenye kutoa ushahidi mbinguni.
 
huyu ole medeye kweli anaufahamu mdogo sana.
hao anaowaita wazawa pale Arusha wapo wachache sana.
sasa anapotegemea kura za wazawa sijui anatumia utafiti gani alioufanya.
mji wa Arusha una watu mbalimbali hao wenyeji tena kwa Arusha mjini hawafiki hata asilimia ishirini.
 
Andiko zuri lakini hoja ya msingi ni hearsay and bruit.

Imani ya dini isikufanye ukawa na imani kwa kila kile kinachokuja mbele ya masikio yako bila kukifanyia uchambuzi yakinifu na matokeo yake unajikuta unaangukia kwenye maandiko ya Exodus 20:16 which says, "You shall not give false testimony against your neighbour".
MwanaDiwani

False testimony?

Kaka/dada, vyombo vya habari LUKUKI liliripoti kuhusu mkutano ulioitishwa na Ole Medeye wakati wa kampeni za Uchaguzi wa Madiwani, na si jambo la siri. Habari "za kuaminika" kutoka kwa majirani wema wanaoupinga ufisadi, ambao walikuwa ndani ya kikao hicho, waliripoti "word for word" na wengine kurekodi picha za video kuweka ushahidi wa kile alichokisema Ole Medeye, picha ambazo zinapatikana kwenye mtandao wa intaneti wa YouTube.com.

Sasa hili suala la "false testimony" linatoka wapi, ikiwa hata magazeti yenyewe yaliandika kuhusu tukio hili?
 
Last edited by a moderator:
Andiko zuri lakini hoja ya msingi ni hearsay and bruit.

Imani ya dini isikufanye ukawa na imani kwa kila kile kinachokuja mbele ya masikio yako bila kukifanyia uchambuzi yakinifu na matokeo yake unajikuta unaangukia kwenye maandiko ya Exodus 20:16 which says, "You shall not give false testimony against your neighbour".

[The story is totally true "No doubt that Mideye ameongea na malagwanani kuwapandikizia chuki za kikabila. BUT mind you KAMWOA MCHAGA. Huyu mh. kwa jinsi ninavyomfahamu si mkabila hata kidogo. Amewahi kuwaambia waarusha wa jimbo lake (mimi ni mpiga kura wake na mwarusha mwenzake) kwamba kunyweni enamasher (pure chang'aa) sana ikatafsiriwa kwamba anataka waarusha wafe na waishe ili wachaga(shemeji zake) waichukue ardhi ya waarusha.
On the point: ukweli ni kwamba amefanya dhambi kubwa sana hata kama ameshinikizwa na babayake a.k.a. Lowassa (yeye ndiye alihakikisha anapata ubunge kwa umafia na fedha). Kabla ya yeye kuja kuwachochea waarusha tayari mkuu wa mkoa alishaanza hizo kampeni, 'ndo maana nasema amesukumwa si kutoka ndani ya moyo wake. Huyu mzee hajafanya.hafanyi lolote kama mbunge tangu amechaguliwa hafai hata kuwa mjumbe wa nyumba 7 kwahiyo hata kuwapata hao wazee ni mbinde atakuwa ameandaliwa tu kwani yeye hayuko nao karibu.
NAOMBA NICHUKUE NAFASI HII KUMWELEZA (japo nimesikia kwamba hata yeye mwenye hataki tena) KWANZA WANAARUMERUMAGHARIBI WA KABILA ZOTE HATUTAMPA KURA ZETU NA TUKIPIGA KURA TUNALINDA KURA ZETU HADI KIELEWEKE.hakuna cha lowasa wala cha muongo wala nani LAZIMA CDM ichukue jimbo kupitia kwa mtanzania yeyote wa jimbo letu (bila kujali ukabila)
lakini naomba nimuulize maswali haya:
1. Lami ya kutoka ngaramtoni mpaka emaoi iko wapi?
2. maji ya kwenye kata karibu zote za jimbo letu yako wapi?(lowasa alijidai mpeni make atampa maji make Mollel aliyakataa kwa Kata za jirani na Ngaramtoni)
3. Barabara za kila kata ulizotuahidi ziko wapi?
4. Mgao wa msitu wa olmotonyi kwa vijiji jirani unaenda wapi?
5. Umeme ulioimba nao, mpaka kwenye uchaguzi wa mtaa wa Olmuringiringa uko wapi?

kwa leo niishie hapo japo nina mengi.
USHAURI:
1. acha uchochezi wa kidini hautamsaidia zaidi ya kumwaribia kesho kutwa unakosa ubunge utaishije ukiwa na ugomvi na shemeji zako?
2. acha kuwa kama jini unatumwa tu na wewe unaitikia (kumbuka uliponea chupuchupu kule mlangarini wakati wa uchaguzi mdogo Meru.
3. Tumia akili na nguvu ulizopewa na Mungu kuwasaidia watu uliowaomba kuwaongoza (utalaaniwa)
4. achana na lowasa anakudanganya (mbona yeye anawahudumia watu wake lakini wewe hakushauri hivyo?
5. usiwe na wivu kwa anayeweza, kama wewe huwezi basi mwache mwenye uwezo wala usiwe na uchungu naye make karama ni Mungu ndiye anayezigawa]
 
[The story is totally true "No doubt that Mideye ameongea na malaigwanani kuwapandikizia chuki za kikabila. BUT mind you KAMWOA MCHAGA. Huyu mh. kwa jinsi ninavyomfahamu si mkabila hata kidogo. Amewahi kuwaambia waarusha wa jimbo lake (mimi ni mpiga kura wake na mwarusha mwenzake) kwamba kunyweni enamasher (pure chang'aa) sana ikatafsiriwa kwamba anataka waarusha wafe na waishe ili wachaga(shemeji zake) waichukue ardhi ya waarusha.
On the point: ukweli ni kwamba amefanya dhambi kubwa sana hata kama ameshinikizwa na babayake a.k.a. Lowassa (yeye ndiye alihakikisha anapata ubunge kwa umafia na fedha). Kabla ya yeye kuja kuwachochea waarusha tayari mkuu wa mkoa alishaanza hizo kampeni, 'ndo maana nasema amesukumwa si kutoka ndani ya moyo wake. Huyu mzee hajafanya.hafanyi lolote kama mbunge tangu amechaguliwa hafai hata kuwa mjumbe wa nyumba 7 kwahiyo hata kuwapata hao wazee ni mbinde atakuwa ameandaliwa tu kwani yeye hayuko nao karibu.
NAOMBA NICHUKUE NAFASI HII KUMWELEZA (japo nimesikia kwamba hata yeye mwenye hataki tena) KWANZA WANAARUMERUMAGHARIBI WA KABILA ZOTE HATUTAMPA KURA ZETU NA TUKIPIGA KURA TUNALINDA KURA ZETU HADI KIELEWEKE.hakuna cha lowasa wala cha muongo wala nani LAZIMA CDM ichukue jimbo kupitia kwa mtanzania yeyote wa jimbo letu (bila kujali ukabila)
lakini naomba nimuulize maswali haya:
1. Lami ya kutoka ngaramtoni mpaka emaoi iko wapi?
2. maji ya kwenye kata karibu zote za jimbo letu yako wapi?(lowasa alijidai mpeni make atampa maji make Mollel aliyakataa kwa Kata za jirani na Ngaramtoni)
3. Barabara za kila kata ulizotuahidi ziko wapi?
4. Mgao wa msitu wa olmotonyi kwa vijiji jirani unaenda wapi?
5. Umeme ulioimba nao, mpaka kwenye uchaguzi wa mtaa wa Olmuringiringa uko wapi?

kwa leo niishie hapo japo nina mengi.
USHAURI:
1. acha uchochezi wa kidini hautamsaidia zaidi ya kumwaribia kesho kutwa unakosa ubunge utaishije ukiwa na ugomvi na shemeji zako?
2. acha kuwa kama jini unatumwa tu na wewe unaitikia (kumbuka uliponea chupuchupu kule mlangarini wakati wa uchaguzi mdogo Meru.
3. Tumia akili na nguvu ulizopewa na Mungu kuwasaidia watu uliowaomba kuwaongoza (utalaaniwa)
4. achana na lowasa anakudanganya (mbona yeye anawahudumia watu wake lakini wewe hakushauri hivyo?
5. usiwe na wivu kwa anayeweza, kama wewe huwezi basi mwache mwenye uwezo wala usiwe na uchungu naye make karama ni Mungu ndiye anayezigawa
 
ole medeye --------, kwanza hawezi kufikiri kuwa hapo kuna mchanganyiko wa makabila, na kuna watu wengi sana wana wazazi ambao mmoja ni mmasai/mwarusha na mwingine ni mchaga, utawabaguaje hao? achilia mbali kuwa tanzania haiishi ubaguzi wa rangi wala wa kabila, dini n.k mbona wabunge wengi au wote ambao sio watz wa asili wako ccm? hajawahi kuwaona aje saa hizi kuwang'ang'ania wachaga ambao wanaotembea kwa miguu kutoka arusha kufika kwao?
 
Kamanda usibabaishwe na gamba lolote kwani historia ni mwalimu mzuri kabisa.Arusha mjini na Arusha kama mkoa ndio chanzo cha mabadiliko katika ukombozi wa taifa hili.Hili gamba liitwalo Medeye linaleta ubaguzi.Uzuri tu ni kwamba Arusha mjini iliwahi kupata mbunge mzawa mwishoni mwa miaka ya1970;tangu hapo kukawa na mseto wa wabunge toka makabila mbalimbali.
 
Ole medeye ana matatizo mengi ila kubwa nadhani kajisahau kwa kiasi kikubwa. Huyu bwn kipindi akiwa na akili zake timamu alishaenda hadi yerusalemu ila kwa sasa sidhani km bd anayo imani ya kweli au ni ya kinafiki. Pili huyu jamaa mkewe mbn ni mchaga wa marangu? Ila inasemekana kuna wkt alitaka kuoa mke mwingine baada ya fedha kumtembelea maana mkewe anaonekana mzee na amechoka ukilinganisha na mwanaume. CCM inatumaliza tukiangalia kwa macho hivi hivi.
 
Medeye ni mmoja wa watu wa hovyo sana

ana abuse sana watu mitaani huko arusha na hili suala la wachagga ngoja tumpatie maana na yeye ana ardhi mikoa mingine, itabidi arudishe yote abaki na ya kwao
 
Ukiwa na akili za sisimizi kama za huyu mtu ndio waweza kusema hayo aliyoyasema, hivi yule diwani wa Arusha mjini nae si ni Mchaga yule? au kuna akina Lyimo Wameru/Waarusha au Wamasai? Kweli akili ndogo inatawala akili kubwa.
 
Tukisema CCM wameishiwa sera wanakuja juu, wanasahau kwamba Mwl.Nyerere alisema tangu zamani, watu walioishiwa sera hukimbilia udini, ukabila na umkoa.Je, hayo hayaonekani kwa vitendo miongoni mwa wanaCCM kama si wote?
 
Back
Top Bottom