"Hate Me Now" By Nas (ft. Puff)
Dah, e bana AshaDii unatishaaaa!!! nakumbuka kulikuwa na ile ki2 Pumps and Bam ya Brand Nubian(cjui kama nimepatia, manake wakti ule english yenyewe ilikuwa bado ya primary school) , ambayo nazani MC Hammer nae akaja kuigonga vilevile!!!! Halafu kuna ile ki2 Jump Around, nazani ya Cyprass Hill wale kama sio House of Pain!!!! Jump! Jump! Jump! Jump!! Jump around! Jump Around!!!! Hiyo ikija mazeyaa disco vumbi ni vurugu mtindo mmoja......joto lote la Dar lakini unakuta bado mtu katinga ndonga moja ina kama kilo tatu hivi huku una bonge la winter jacket ambalo unahakikisha OPP halitoki kichwani!!!! Dah, kweli Hip Hop is Dead!!!! Halafu kuna ngoma moja hivi; ndo vile tena english yenyewe ilikuwa ya shule za uswahilini, kwahiyo sikumbuki ilikuwa inaitwaje na nani waligonga lile dude......ninachokumbuka ni kwamba, washikaji wanachana, halafu kuna mistari inasema WEUSI SHULE na kuna kibao(video yake) kina hayo maandishi!!!! Ilikuwa ni full mzuka, wakati ule kila dent nae ni MC!!!! Na hiyo ilikuwa ndio tiketi ya kuchukulia watoto wa kishua wa Oysterbay na masaki!!! Nakumbuka na mimi nilikuwa na mistari yangu, kuna sehemu inasema
"Mshikaji maskani kawa pusha,
nami nachakarika deal lo kulizungusha,
nahangahika, dar mpaka arusha hakuna jipya,
narudi morogro mpaka dom; kote msoto!
Maskin,
tumekosa nini,
kama hatuchakariki
ndipo natamani kwenye safari
nikutane na osama anipe deal
deal ni-test zali
deal ni deal, usiniulize deal gani choko
ukija zua sokomoko mimi simo,
shauri yako, utavyokumbwa na vipigo
mi n'takupa hi,
wakati upo kwenye mikono ya FBI
kudadeki wallah
kumbe kweli mambo moto
mshikaji mpenda dezo kawa choko
choko kinoma noma hakuna tena
na machizi wamemnunia, nuna nuna
na wengine wanadunda, danda danda
mpaka kwa rais anasema tufunge mkanda
tushafunga mpaka tundu la mwisho,
lakini bado,
mikanda inatupwaya
ingawa mzee mkapa tundu la kwanza
mkanda unambana!
noma, kinoma nom
masela hatuna noma
sela nachakarika
sometime nazungusha ki-uhakika
mbagala mpaka tandika
tmk, mpaka dongo
kote mambo c mambo
sometime nashika midako
nakupambana na masoja wanoko
wanataka nikate mishiko
nami nabaki mweupe mtupu
upuuzi mtupu'
sela nyonga dupu
tembeza kwa washikaji
hoyaa mjuba,
mwenge huvuki kijiji'
piga pafu mbili
pandisha stimu tafuta deal
deal ni deal hata kamali
cheki kwa mbali kuna askari
asilete za kuleta'
mweleze kila mbongo anatafuta
na kama karata tatu, na bingo yote mamoja
akili inanituma kujenga hoja
ya mshike mshike
mzabe mzabe
na masela ndani ya zege
hakuna wanachopata ilimradi njaa wagange
kimbindembinde bora liende
na kifo ni kifo hata cha mende
sasa nini unangoja
beba kideo twende............................................wakti ule TV tulikuwa tunaita video...lol
dah!!!!!!!!!1