Oil,Power & War

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2011
Posts
1,237
Reaction score
1,828
Jina la kitabu:OIL POWER AND WAR
Mwandishi:MATTHIEU AUZANNEAU
Mchambuzi: Nanyaro EJ

Utangulizi!
Mwandishi wa kitabu hiki ambacho kwa undani kitaelezea historia adhimu kabisa ya mambo ya nishati,anaanza kuuliza swali kuwa nini maana ya maendeleo? maendeleo ni nini?

Wakati tukijibu swali hili ni wito wangu kwa kila mmoja kujisomea kitabu hiki adhimu ili kupata mwanga wa wapi hasa Dunia na Ulimwengu vinaelekea

Mwandishi anasema kuwa NISHATI ndio msingi mkuu wa maendeleo na ndio maendeleo yenyewe.Hoja yake ni kuwa Nishati ndio ina uwezo wa kubadilisha asili ya vitu vingine,nishati ndio inaendesha vitu vingine,ndio chanzo cha vitu vingine,kwenye kila eneo au hatua utakayopiga au kuchukua lazima utahitaji nishati ili usonge mbele,ni wazi bila nishati dunia ingesimama,kiuchumi,kijamii na kwenye kila nyanja,hakuna teknolojia bila nishati,hakuna ubunifu bila nishati,ndio kusema bila nishati hakuna hatua yoyote ya maendeleo ambayo binadamu anaweza kuichukua

In other words,energy is the ultimate universal currency.As
GeorgesBataillewrotein1949,“Essentially wealth is energy:

bila nishati hakuna uzalishaji,bila uzalishaji hakuna maendeleo na bila maendeleo maisha ya binadamu yasingekuwa na dhamani kuishi


Mwandishi anasema kuwa leo ,fossil fuels inachangia zaidi ya 50% ya nishati tunayotumia kila siku,hakuna mabadiliko makubwa sana tangu enzi za garimoshi la kutumia moshi na makaa,tangu baada ya vita ya pili ya Dunia nishati ya mafuta imebaki miongoni mwa nishati ambazo ni uti wa mgongo na miongoni mwa bidhaa adimi na adhimu sana kwenye uchumi wa Dunia,ni nishati ambayo imeungwa na maisha yetu ya kila siku,ni vigumu au haiwezekani kabisa kutenganisha nishati hii ya mafuta na maisha ya binadamu ya kila siku,imekuwa kama damu kwenye mwili wa binadamu,kuwa huwezi kuishi bila nishati hii!

Kwenye makala zinafuatia tutaangazia mataifa na familia ambazo kwa miaka mingi zimekuwa ndio kinara kwenye nishati hii,na jinsi ambavo zimeadhiri maisha na uchumi wa Dunia kwa ujumla,tutaona muungano na mafungamano ya Familia ya Bush na ile ya Bin Laden,pia tutaangazia familia maarufu ya Rockfeller.Tutaona kwa kina namna ambavo nishati hii imeangusha tawala za Dunia na kuleta madhara kwa mataifa kama Iraq 2003

-----------------Nanyaro EJ-----------------
 
Hicho kitabu kingekuwa mada ya GOD kingenoga sana, au G.O.D Kirefu ni Gold Oil Drugs

In God we trust and obey
 
Vitabu kama hv, soma mwenyewe,ndio utajua utamu wake, hii ya kutafsiliwa, inapunguza utamu.
Kwa bongo, Elvis Musiba, ndio aliweza kuweka hz mada kwenye ki Swahili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…