iparamasa
JF-Expert Member
- Nov 14, 2013
- 13,437
- 14,924
URAIS wake alienda kuchukua fomu peke yake......karibu ofisi zote za umma zinaanza "OFISI YA RAIS......"
Zamani Tamisemi ilikuwa chini ya waziri mkuu
Sijui ndio kujilimbikizia madaraka??!!
..,........................
....................,.......
Nimekuwa nikitembea maeneo mbalimbali ya nchi yetu mpaka vijijini
Kwa kweli "Ofisi za Rais" ni nyingi,kila mahali ipo, na bango lipo
Kila shule imeandikwa "Ofisi ya Rais" ndipo utambulisho unafuata,nyingine ziko ndani kabisa porini,nyingine shule za awali.
Shule moja imejengwa kwa tope na miti na ingine imepasuka ukuta imebidi iegeshwe kwa mti darasa lisidondoke,nayo eti imeandikwa "ofisi ya rais....wanafunzi waliokaa ndani kama vibwengo ndugu yangu,wamekula vumbi haswa kwa kuwa darasa halina sakafu
Ofisi ya serikali ya mtaa wetu nayo imeanza na utambulisho "Ofisi ya Rais".
Kitongoji naye kaona looooh!! Nibaki nyuma? watajuaje niko ofisi ya rais? Naye kajihimu mapema,katafuta mtaalam wa maandishi kamchorea bango kubwa,Ofisi ya Rais...
Ofisi ya serikali ya kijiji kule mpigamiti nayo imeanza na utambulisho "Ofisi ya Rais"
Katibu Tarafa wetu naye hakubaki nyuma,bango lake linasomeka vizuri kabisa "Ofisi ya Rais"
Mkuu wa wilaya yetu naye kaliweka wazi "Ofisi ya Rais....Tawala za mikoa na serikali sijui za nini nini
Mkuu wa mkoa naye haswaaa " Ofisi ya Rais ....Tawala za nini sijui chai maharage.
Halmashauri za Miji,vijiji,Jiji,Manispaa nazo kwa mikogo kabisa zinaanza utambulisho "Ofisi ya Rais.......
Takukuru hawakuachwa nyuma pamoja na Tume ya Maadili .....mabango yao yanasomeka vizuri. ....." Ofisi ya Rais
Mwenyekiti wetu wa mtaa huwa anatukoga tukienda kuomba Huduma kwake,basi huitambulisha ofisi yake kwa sauti yake ya mikogo huku akishikashika koti lake lililopigwa vumbi na kuchakaa ......."ndugu,karibu ofisi ya rais,Tawala za mikoa,serikali za mitaa....."""anaongea huku ofisi nzima ikitanda harufu ya ugimbi alioutwika jana
Looh! Basi bibi yangu kaniuma sikio aniuliza "eti hapa ndio kwa yule rais wetu...ofisini kwake"
Mmhhh!! Basi mi nkacheka kimoyomoyo nikisema bibi anayatafuta masaa 48 ,yule aliyekuwa kwenye ofisi ya rais akatupigia muhuri,tukaondoka tukichekaa na bibi yangu