Katika ofisi ya utumishi halmashauri ya wilaya ya misungwi kumekuwa na uzembe na kutojali kwa kiwango cha juu kwa baadhi ya watumishi. Nitatolea mfano eneo moja tu kwa leo, nalo ni kuhusu upandishaji wa madaraja kwa watumishi katika halmashauri hii.
Mnamo tarehe 1/4/2018 watumishi wenye sifa walipandishwa vyeo na bodi ya ajira ya halmashauri hiyo. Lakini mpaka leo tunamalizia mwaka [miezi 8] hakuna mabadiliko yoyote katika mshahara wa watumishi hawa.
Wanapofatilia sababu zinazotolewa ni kuwa hakuna mtandao au muhusika hayupo, na kuambiwa uache nakala ya barua yako ya kupandishwa cheo.
Kumekuwa na ufuatiliaji wa bila mafanikio katika ngazi mbalimbali kuhusu suala hili.
Maswali ya kujiuliza ni kwamba;
Wito wangu kwa wenye mamlaka;

- Ni kwanini wawapandishe watu vyeo ilhali wanajua mtandao hautakuwepo kwa miezi minane?
- Ni kwanini wawapandishe watu vyeo ilhali wanajua wahusika hawatakuwepo kwa miezi minane?
- Na kama hizo ndiyo sababu za msingi je kuna uwezekano ofisi ya serikali kusiwe na mtandao au watumishi wenye dhamana na jambo hili kwa miezi minane?
- Kama jambo liko nje ya uwezo wao kwa nini wasiseme ukweli?
Wito wangu kwa wenye mamlaka;
- Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri tunaomba uitishe mafaili yote ya watumishi waliopandishwa vyeo na uombe maelezo ya kutosha kwa wote ambao hawajabadilishiwa mishahara yao.
- Ofisi ya TAKUKURU fuatilieni hapo kuna viashiria vya rushwa, tunaomba mchunguze.
- Katibu tawala wa mkoa wa mwanza, halmashauri hii iko chini yako, tunaomba uwaulize
- Waziri/katibu mkuu haya mambo yanawavunja moyo watumishi uwezo wa kuomba taarifa hizi mnao tunaomba fatilieni.