Ofisi ya Taifa ya ukaguzi ijitathmini

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,666
3,838
Ndugu zangu,

Tangu kuteuliwa kwa CAG mpya ndugu profesa assad kumeanza kuwa na tuhuma mbalimbali kwa Ofisi yake hali itakayoweza kusababisha ofisi hiyo kutoaminika. Ni muhimu ifahamike kuwa ofisi ya taifa ya ukaguzi (supreme audit unit) duniani kote ni ofisi inayotakiwa sio kutuhumiwa tu bali hata kuwa na fununu za matumizi mabaya.

Kinachomponza Profesa assad ni mambo yafuatayo ambayo ni muhimu ayarekebishe haraka,

1. Anatuhumiwa kujitenga sana na watumishi wa kawaida na kufanya mambo mengi bila kushirikisha watumishi

2.Kutoheshimu seniority ikiwa ni pamoja na kumuachia mtu anayeitwa SELEMAN kuwa kama kiongozi wa Ofisi na ambaye anatuhumiwa kuchonganisha watumishi na CAG na ndiye anasimamia hamisha hamisha ya maofisa kwa upendeleo na majungu.

3. Tuhuma za upendeleo wenye kujificha kwa elements za udini na ukabila (mathalani amemsimamisha kazi accounting officer na ofisa mipango kutokana na tuhuma za ubadhirifu katika fedha za mradi lakini akaacha kumsimamisha mhasibu mkuu wa mradi huo kwa kuwa ni dini na kabila lake)

Ni kwa msingi huo sasa naye kaanza kuchafuliwa kwenye magazeti kila siku kuwa anatumia fedha vibaya kwa safari, ununuzi wa samani na ukarabati. Ofisi ya ukaguzi haitakiwi kuwa na tuhuma hizi zinaishushia kuaminika kwa jamii.

Profesa assad ni muhimu ukatathmini masuala hayo na kujirekebisha.
 
Kila siku huwa najiuliza nani hukagua mahesabu ya ofisi hii, maana mtaan tunawajua kuwa ni wapigaji wa pesa kama walivyo wapigaji wengine.
 
Hivi kuna chombo gani kinachoaminika nchi hii, mahakama haziko huru hivyo wananchi hatuna imani nazo sana, polisi hawaaminiki nao %kubwa wanatumika badala ya kulinda wananchi na mali zao, bunge nalo haminiki kwa sababu linatumika kupitisha mambo muhimu ya Taifa mfano miswada ya gesi, kila kitu kipo hovyo hovyo, labda JWTZ naona wako smart
 
Back
Top Bottom