Ofisi ya Kamishna Mkuu TRA yavunjwa, Kompyuta mbili zaibwa

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,786
Watu wasiojulikana wamevamia na kuvunja ofisi ya kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuiba kompyuta na vifaa vingine.

Habari tulizozipata ambazo zimethibitishwa na Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam zinasema miongoni mwa kompyuta zilizoibiwa ni ile iliyokuwa inatumiwa na Dr. Philip Mpango alipokaimu nafasi ya Kamishna mkuu wa TRA kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Fedha.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, huenda kompyuta hiyo ikawa na taarifa muhimu kuhusu ukwepaji wa kodi na sakata la makontena Bandarini.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Ya Dar es salaam,Simon Sirro amesema tayari jeshi hilo linawashikilia watu wanne kwa uchunguzi zaidi.

Siro alitaja vitu vilivyoibwa katika ofisi hiyo kuwa ni Kompyuta mbili, Televisheni moja na King'amuzi.
Alisema wanaoshikiliwa ni walinzi wawili kutoka kampuni ya Suma JKT ambao walikuwa zamu usiku huo, Katibu Muhtasi pamoja na Karani wa Ofisi hiyo.

Tangu aingie madarakani, Rais John Magufuli amefanya mabadiliko katika mamlaka hiyo kwa kumwondoa aliyekuwa Kamishna Mkuu, Rished Bade na kumteua Dk Mpango kukaimu nafasi hiyo, kabla ya kumteua kuwa Waziri wa Fedha na nafasi hiyo kuchukuliwa na Alphayo Kidata.

Katika kipindi hicho, baadhi ya wafanyakazi wamewajibishwa kwa kusimamishwa kazi kutokana na tuhuma za ama kushindwa kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato au kushirikiana na wafanyabiashara kukwepa kodi na kulisababishia hasara Taifa.
 
Mmmh kwwli watu wajinga wanafikili kuiba computer ndo solution. Wajue tu kuwa muda wao ushafika tu so watulie watumbuliwe majipu.
 
Hiyo ni mbinu kah!! Mafisadi yana mbinu za kizamani sana karne hiu ya leo utamdanganya nani??? Mbona miaka yote hatukuwahi kusikia Tra kumeibiwa?

Ila ni kipindi hiki cha anselema la Magufuli na Tra.
 
Wezi wamepitwa na wakati . Siku hizi tehama imekua bana. Unaweza kuhifadhi mafaili yako kwenye mtandao ukayafungua ukiwa mahali popote penye internet.
 
Watu wasiojulikana wamevamia na kuvunja ofisi ya kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuiba kompyuta na vifaa vingine.

Habari tulizozipata ambazo zimethibitishwa na Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam zinasema miongoni mwa kompyuta zilizoibiwa ni ile iliyokuwa inatumiwa na Dr. Philip Mpango alipokaimu nafasi ya Kamishna mkuu wa TRA kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Fedha.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, huenda kompyuta hiyo ikawa na taarifa muhimu kuhusu ukwepaji wa kodi na sakata la makontena Bandarini.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Ya Dar es salaam,Simon Sirro amesema tayari jeshi hilo linawashikilia watu wanne kwa uchunguzi zaidi.

Siro alitaja vitu vilivyoibwa katika ofisi hiyo kuwa ni Kompyuta mbili, Televisheni moja na King'amuzi.
Alisema wanaoshikiliwa ni walinzi wawili kutoka kampuni ya Suma JKT ambao walikuwa zamu usiku huo, Katibu Muhtasi pamoja na Karani wa Ofisi hiyo.

Tangu aingie madarakani, Rais John Magufuli amefanya mabadiliko katika mamlaka hiyo kwa kumwondoa aliyekuwa Kamishna Mkuu, Rished Bade na kumteua Dk Mpango kukaimu nafasi hiyo, kabla ya kumteua kuwa Waziri wa Fedha na nafasi hiyo kuchukuliwa na Alphayo Kidata.

Katika kipindi hicho, baadhi ya wafanyakazi wamewajibishwa kwa kusimamishwa kazi kutokana na tuhuma za ama kushindwa kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato au kushirikiana na wafanyabiashara kukwepa kodi na kulisababishia hasara Taifa.
Kitaeleweka tu....!!!!!
 
Back
Top Bottom