Ofisi ya CUF Zanzibar yavamiwa, watu watembezewa kichapo

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,504
1-5-1.jpg.pagespeed.ce.yiyGwucsmB.jpg


Watu wasiojulikana maarufu kama (mazombi) wameivamia ofisi ya Chama cha Wananchi (CUF) katika Jimbo la Dimani wilaya ya Magharibi B.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo huku CUF wakitaka uchunguzi uanze mara moja kuwabaini wahalifu.

“Ni kweli taarifa tunazo za watu kuvamia ofisi hiyo ya CUF na kuwapiga pamoja na kuwahujumu watu na huo ni uharamia unaoripotiwa mara kwa mara,” alisema Kamanda Ali. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma wa CUF, Salim Abdallah Bimani alisema, “Huu ni uvunjifu wa amani na tunataka Rais John Magufuli iwapo anayo nia ya dhati afuatilie hujuma hiyo ambayo watekelezaji wake wanajulikana lakini hawakamatwi”.

Aliendelea kuzungumza “Mazombi wameshawapiga sana wananchi hasa wafuasi wa CUF ambao hawana hatia, wengine mpaka walipoteza maisha, wameshawapiga watu na kuwajeruhi vibaya na pia kuwaibia watu mali zao na hatuoni hatua yoyote ikichukuliwa”.

Aliongeza “Tunamwambia Rais Magufuli kwa mujibu wa Katiba yeye ndiye mwenye mamlaka ya kuwalinda raia wote wa nchi hii, achukue hatua.” Tukio hilo lililotokea saa 6.30 usiku wa kuamkia jana.
 
Huo muda kuna kuwa na wafanyakazi gani?

Hata mimi nimejiuliza inakuwaje watu wawepo ofisini 6 usiku? Maana siku hiz hapa jukwaani kuna habari zinaletwa kinazi mpaka tunashindwa kujua ukweli ni upi na uongo ni upi.
 
Kafu wanajipiga wenyewe,wanasingizia mazombi.
Huyo Bimani ni lini amemtambua magufuli kiasi cha kumtaka aingilie kati,Zanzibar kuna Valantia amwambie mwenye kikose chake aingilie kati kuzuia uhuni huo kama upo
 
matukio ya upande mmoja haya, kwanin n upande ule tu na sio uhuu wa kijan? yote haya yana mwsho. Maana hakuna marefu yacyo na ncha
 
kwa wale wasiojua, Zombi lipo hivi
upload_2017-1-16_11-27-11.jpeg
 

Attachments

  • upload_2017-1-16_11-26-40.jpeg
    upload_2017-1-16_11-26-40.jpeg
    4.4 KB · Views: 19
Muache kelele kuweni wanaume. Muanzishe antizombi movement na vikundi vya sungusungu.
 
Hawajulikani kivip wakat umesema ni mazombi kwanini hao mazombi wasitiwe mbalon yaan wahalifu munawajua had majina afu mnadai hawajulikan
 
Back
Top Bottom