Ofisi ya Bunge yakanusha tuhuma mbalimbali zilizoelekezwa kwake, ikiwemo kwamba linaendeshwa kibabe

Wapeleke upuuzi huko wanakanusha nini kwani mambo ya bunge yanafanyika sirini?

Sisi wananchi ni vipofu hatuoni kinacho endelea?

Hili bunge la sasa hivi halina maana yoyote
 
234e69_591fac343be44a229af21684b7685c42%7Emv2.jpg


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai aliunda Kamati Maalumu ya wajunge tisa (wabunge) kuchunguza suala la uchimbaji wa Madini ya Almasi hapa nchini, ripoti ya bunge ilikamilika vizuri na kwa mujibu wa kanuni za bunge ripoti hiyo ilitakiwa ijadiliwe na wabunge, na bunge litoe azimio kuhusiana na ripoti hiyo, maazimio ya bunge ndiyo yapelekwe serikalini kwa utekelezaji.

Kanuni za bunge zilionekana siyo muhimu, jioni hiyo hiyo alipanda ndege hadi Ikulu kwa Rais na kukabidhi ripoti ya bunge bila kujadiliwa na bila ya azimio lolote la bunge.

Tangazo lake kuwa bunge linashambuliwa, siyo sahihi tatizo liko kwake SPIKA na anastahili kuomba msamaha kwanza kwa wabunge na kwa Watanzania.




 
Wapeleke upuuzi huko wanakanusha nini kwani mambo ya bunge yanafanyika sirini?

Sisi wananchi ni vipofu hatuoni kinacho endelea?

Hili bunge la sasa hivi halina maana yoyote
Wanadhani watakuwa madarakani milele.. Wamuulize Sitta yuko wapi
 
Hii nchi inakanuni na sheria za ajabu sijapata kuona!! Spika wa bunge ndo anateua kamati ya bunge ama anachagua kutokana na utashi wake watu anaowaamini katika kamati hiyo! Harafu kanuni zinaelekeza kuwa kama mbunge hajaridhishwa na maamuzi ya spika anatakiwa apeleke malalamiko yake kwenye kamati ambayo wajumbe wake wote wamechaguliwa na spika!!!! Hapo hatakama elimu yangu si kubwa, sidhani kama haki ataipata mlalamikaji!! hii ni sanaa!!
Haya ndo mambo yanayotakiwa kufanyiwa marekebisho lakini watu wanakalia mambo mengine tu!!
Kwa maelezo hayo ya kuwepo kwa kanuni hizo zinazompa madaraka spika kuamua mambo mengi bira hatakupitisha bungeni for approval ni haki bunge haliwezi kuwa huru!!!
Angalia AYA YA SABA NA YA NANE. uniambie huyo mbunge atakuwa kapeleka malalamiko yake wapi?
 
Maelezo mazuri na yamejitosheleza ila wazee wa kupinga kila kitu wapotoshaji tu.

Hongera sana bunge kwa kutoa ufafanuzi mzuri mmeeleweka.
"Mimi ninamamlaka kuzidi yaliyoandikwa, nimepewa mamlaka na Mungu"
 
Hili bunge letu sasa nadhani lijitizame upya anasema katika kutuliza vurugu bungeni mpambe wa speaker aweza kuingilia kati kumtoa nje mbunge sijaona palipoandikwa askari polisi anaweza kuingia bungeni na kumtoa mbunge nje lakini hiyo imeshawahi kutokea.
 
Kushutumiwa tu kunatosha kuonesha ulimwengu kuwa kuna uovyo fulani unaendelea... Unaweza kudanganya ila huwezi jidanganya mwenyewe... sasa kwa barua hii ni kuandika huku unajidanganya... sababu kila kitu kipo wazi hata mtoto mdogo wa shule ya msingi ukimuuliza atasema hafurahishwi na utawala huu... Watanzania tumekuwa hatuna cha kujivunia... Raisi spika wanachukiwa kama mwaka 2015 ccm ilivyokuwa inachukiwa... badilikeni Upinzani sio uadui... ndio dhambi ya ubaguzi mliyonayo Nyerere alishawaonya sana kuwa Ubaguzi ni dhambi hatari sana na huwa inaendelea
 
Hivi ndio lile Bunge ambalo muhimili mwingine ulifanikiwa kuwachagulia watu gani wanfaa kukaa kwenye kamati
 
Mara 100 wangekaa kimya, kuliko wanavyotoa hizo press zao bila hata kutumia akili. Kweli nimeamini Mungu anapotaka kuangusha ufalme huwa anaufitinisha.
 
Hatuna spika pale ...tuna subwoofer. . .yule nae wakiitwa ma spika wa bunge atatoka ....labda spika ya kutangazia madudu ya mafism
 
Hawana jipya,wala sio tuhuma ni ukweli mtupu,Mkulu ni mwenyekiti wa ccm na Nguguboi Jooob ni mwanachama,sasa mtuambie yale maagizo ya wewe washughulikie bungeni wakija nje niachie Mimi,yalimaanisha mini?? Msituone misukule tunajitambua,,,hilo jumba la uwakilishi lishawekwa mfukoni na Baba kitamboooooo
 
Kadiri wanavyojitokeza kumsafisha speaker na bunge ndio kadiri wanazidi kuuchafua huu muhimili.

Bunge ni muhimili unaojitegemea japo siku za karibuni limekuwa kama jumuia ya kile chama cha kijani. Hovyo sana

Limekuwa kama NEC ya CCM
 
Back
Top Bottom