ODM Yageuka Joka Kubwa Ndani ya NASA

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,081
2,000
Baada ya kuonyesha tofauti kubwa huko Mombasa kati ya kinara wa ODM Rails Odinga na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka kuhusu wagombeaji wa ugavana wa kutoka chama gani aungwe mkono ni dalili tosha uhai wa muungano wa vyama hivi upo mashakani.
Raila Odinga ameonyesha utaalamu wake wa kisias kwa kutumia vyama vingine vya siasa ili kutimiza azma yake kuwa Rais wa Kenya. Kama hali ya kutoelewana ikiendelea kuna uwezekano chama cha Jubilee kikarudi madarakani.
Hii ni dalili tosha ODM imegeuka kuwa joka kubwa na kuanza kuvimeza vyama vilivopo kwenye muungano wa NASA
 

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
21,194
2,000
Duh ila Kalonzo hapa aliingia cha kike maana hata wabunge wake wanamgomea. Hawa hata wakichukua uongozi itakua malumbano kila siku maana wote wababe wakiwemo Rutto, Mudavadi na Wetangula.
Hakuna kati yao aliyehakikishiwa uungwaji mkono 2022. Juzi nimemwona Rutto anajitapa kwamba wasimwone kama mtu mdogo ndani ya NASA. Kutakua na ushindani baina yao kwamba nani yu karibu na rais.
Hayo ni maoni yangu msinivuruge.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom