PostGE2025 Odemba ambana Faris kauli ya "Tukiwapoteza msiwatafute", Faris aomba radhi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kagera Faris Buruhan amesema kauli yake aliyoitoa katikati ya mwezi Aprili mwaka 2024 ‘Tukiwapoteza wanaomtukana Rais Samia polisi msiwatafute”, ilitafsiriwa tofauti akidai kipande cha video kilichosambaa mitandaoni kilikuwa ni sehemu tu ya mazungumzo yake aliyoyazungumza kwa kirefu

Burhan ameyasema hayo akizungumza na mtangazaji Chief Odemba wa kipindi cha Medani Kuu cha runinga ya Star TV siku ya Jumamosi ambapo hata hivyo ametumia fursa hiyo kuwaomba radhi Watanzania waliokwazika na kauli hiyo na kurejea msemo wa ‘Yaliyopita si ndwele tugange yajayo’


 
Odemba kamuingiza kwenye 18 akajaa akampiga kwenye MSHONO.
 
Baada ya mauaji ya kimbari ya Rwanda, watuhumiwa na washitakiwa walikuwa pia wale waliotoa kauli za shari na chuki zilizopelekea mauaji hayo.
 
Odemba yupo vizuri sana,Huyu jamaa alitaka kukwepa akajikuta anabanwa kwenye kona mpaka akakosa pakutokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…