sifi leo
JF-Expert Member
- Mar 30, 2012
- 5,013
- 8,369
Afande OCD mkoa wa Tabora tafadhali naomba unijibu swali hili.
Kama kijana Kisaka baada ya kubaini watoto wake mapacha wamefia mikononi mwa watoa huduma wa afya, kabla ya kukabidhiwa miili alienda kituo cha polisi kilicho karibu na hosptali hiyo na kukutana na askari ambaye hajamtaja kwa vyombo vya habari, amedai alikutana na mpelelezi wa kituo hicho cha polisi akamweleza jinsi wanae walivyo fia mikononi mwa watoa huduma afya.
Akadai kufa sio ishu ila alikuta marehemu wametobolewa macho, zaidi ya hapo alikuta mtoto mmoja amechunwa ngozi na kutobolwe na kutolewa mfupa mmoja.
Kwa majibu ya Kisaka anadai yule afande alimuuliza hivi, "Kwenu hamna mambo ya kishirikina kweli?" Mwisho akamwambia, "We toka hapa nenda hapo Kituo cha Afya mkamalizane na manesi."
Mh. Afande OCD, huyu askari anafanya nini kazini? Halafu ndio mpelelezi anaetegemewa huyo?