OBC loliondo yazidi kukabwa koo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

OBC loliondo yazidi kukabwa koo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ngudzu, Aug 31, 2012.

 1. n

  ngudzu Member

  #1
  Aug 31, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MITANDAO MINNE YA WANAHARAKATI WA HAKI ZA BINADAMU INAYOITWA
  FEMACT
  TANZANIA LAND ALIANCE AU TALA
  PINGOS FORUM YA ARUSHA
  NGONET YA LOLIONDO
  wamemaliza kuongea na waandishi wa habari sasa katika hoteli ya LUSH GARDEN na kutoa tamko Kali dhidi ya serikali kwa nia yake ya kutaka kuuza ARDHI ya LOLIONDO kwa kampuni ya OBC kimya kimya. Tamko lina mambo MENGI ila 5 ni haya hapa chini.


  1. SERIKALI Iache maramoja Kuuza ARDHI HIYO ILI kuepusha athari za kimazingira na kwa binadamu wanaoishi Kwenye vijiji husika
  2. mipango shirikishi inayozingatia HAKI, matakwa na maslahi ya wananchi WENYEJI kutumia ARDHI HIYO iandaliwe
  3. Mapendekezo yaliyotolewa na kamati mbalimbali zilizowahi kutembelea eneo hilo kwa nyakati tofauti ikiwemo kamati ya BUNGE ya bwana Ndugai yafanyiwe KAZI maramoja
  4. SERIKALI Iache kutumia MABAVU katika kupata suluhu ya MIGOGORO inayohusu rasilimali wa wananchi
  Nafukuzia full version niitupie hapa mtandaoni kwa mijadala. NCHI hii iko pabaya Kila kitu kinauzwa sasa tusipokuwa makini
   
 2. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Umenikumbusha kifo cha mpiganaji mwandishi wa gazeti la Mfanyakazi kwenye hili sakata akipinga kwa hoja. Kuna petition nyingine ya dunia nzima kwa JK kupinga kuuzwa kwa Serengeti kwa Falme za Kiarabu. Kinana & Co (CCM) at work
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  RIP Stan Katabalo.
   
 4. m

  massai JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  ndio maana mimi napinga kwa kika hali ujenzi wa barabar ya lami kutoka mto wa mbu kwenda loliondo.sasa kwa wale wachache wasiojua kilichopo nyuma ya pazia nafikiri wataanza kuelewa kua lengo lao lilikua kupata unafuu wa kufika huko wanakotaka kuwekeza.lami itapitishwa vipi kwenye mbuga za wanyama!!dunia nzima inapinga alakini kikweete na wezi wenzake wa sisiemu wanansema kukuchekusikuche lazima lami iwekwe.hawa sisisemu wanataka kùza kilakitu kwasababu wao hawatakuwepo pindi wenye mali yaani wananchi watakapo shtuka
   
 5. A

  August JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2012
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Kitu cha msingimikataba yote ambayo ina gusa maslahiau ardhiya mtanzania iwe wazi sio uamuzi wa Raisi ambao hauna manufaa kwa nchi, je hao OBC walilipa nini kuhalalisha wao kuchezea mali zetu namna hiyo? je wanawalipa watanzania au viongozi waliopitisha uamuzi huo? wakati huo huo hao viongozi tunawalipa pensheni na bado wanaendelea kuwepo kwenye tume mbalimbali au mabodi ya mashirika/wabunge nk nk
   
 6. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Yes! Hawa wadau wanaenda vema kabisa!

  Tupe news yoyote yajirio.
   
 7. N

  Naronyo Member

  #7
  Aug 31, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tungeungana tu watanzania wote nchini kuwaondoa wawekezaji wasio na tija kwa taifa letu. Si rahisi kwa walio madarakani kufahamu hilo ila sisi waathirika tunatambua ukweli huo. Go OBC go..............
   
 8. N

  Naronyo Member

  #8
  Aug 31, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot]TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI[/FONT]
  [FONT=&quot]TAARIFA HII INATOLEWA NA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KUELEZEA MSIMAMO WAO KATIKA KAMPENI INAYOENDESHWA NA MTANZAO WA AVAAZ KUHUSU KUTAKA SERIKALI KUSIMAMISHA MCHAKATO WOWOTE WA KUUZA ENEO LA LOLIONDO KATIKA MFUMO WA IKOLOJIA YA SERENGETI UPANDE WA MASHARIKI AMBAYO NI ARDHI YA VIJIJI[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]SISI mashirika ya kiraia yanayofanya kazi nchini Tanzania katika masuala ya haki za binadamu, uchumi na kijamii, ikiwa ni pamoja na ardhi, usawa wa kijinsia, mazingira na rasilimali kwa jumla tunaunga mkono kampeni inayoendeshwa na mtandao wa kimataifa wa Avaaz ambao ni ulingo wa kimtandao unaotetea haki za binadamu kwa njia ya matamko mbalimbali. Mtandao huu imetoa wito kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusitisha mpango wowote wa kuuza ama kutoa sehemu ya ikolojia ya mashariki ya hifadhi ya Serengeti ambayo ni makazi ya wafugaji wa Kimaasai katika wilaya ya Ngorongoro, tarafa ya Loliondo kwa kampuni ya uwindaji wa wanyama pori ya OBC. OBC ni kambuni ya uwindaji inayomilikiwa na familia ya kifalme ya Ufalme wa Umoja wa nchi za Kiarabu (United Arabs Emirate-UAE). Itakumbukwa kuwa mitandao ya Tanzania Land Alliance (TALA) na FEMACT imekuwa ikijishughulisha na migogoro ya Loliondo kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kutoa matamko mbalimbali. Hata hivyo, serikali imekuwa ikisita kutekeleza mapendekezo hayo. [/FONT] [FONT=&quot]Mgogoro wa Loliondo umekuwepo kwa takriban miaka 20 tangu mwaka 1992 lakini ilifikia kilele mwaka 2009 ambapo serikali iliwatoa kwa nguvu wafugaji wa kimaasai katika eneo la ikolojia ya Serengeti upande wa mashariki kwa lengo la kuanzisha korido au mapito ya wanyama pori katika eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 1,500 ambalo ni ardhi ya vijiji saba (7) vya Loliondo. Kwa kuanzishwa kwa mapito ya wanyama katika eneo hilo, maisha ya watu takriban 48,000 yataathirika na mifugo mingi pia.[/FONT] [FONT=&quot]HISTORIA FUPI YA UWEKEZAJI KATIKA ENEO LA MGOGORO, LOLIONDO[/FONT] [FONT=&quot]Tangu eneo la Loliondo ambalo ni eneo la ikolojia ya Serengeti kwa upande wa mashariki kupewa mwekezaji wa Kiarabu ambaye ni familia ya Kifalme kutoka nchi za Umoja wa Kifalme za Kiarabu kupitia kampuni ya OBC (Otterlo Business Corporation) mwaka 1992, eneo la Loliondo liliendelea kuwa na mgogoro baina ya vijiji kwa upande mmoja na OBC na serikali kwa upande wa pili. OBC walipewa kibali cha uwindaji katika eneo lote la Tarafa ya Loliondo na Sale wilayani Ngorongoro tangu mwaka 1992. Tangu wakati huo ambapo kampuni ya OBC inapewa kibali cha uwindaji, kulizuka upinzani wa wananchi kutokana na mchakato wa kumpa OBC eneo la kuwindia kutokuwa wazi na pia shirikishi. Kutokana na mapungufu haya baina ya serikali na OBC, ulizuka mgogoro ambao umeishi mpaka leo bila ufumbuzi. Hata hivyo, Mwaka 2008 serikali wakishirikiana na OBC waliandaa mkataba na vijiji, mkataba huo ulitaka vijiji kuondoka kwa hiari katika eneo hilo ambalo OBC wameweka kambi yao ili kuweza kufanya uwindaji wa kibiashara. Katika mchakato huu wa mikataba, vijiji vingine vilikubaliana na vingine vikakataa. Kutokana na kutokubalika kwa mikataba hiyo kwa asilimia zote, serikali mwaka 2009 July ilianzimia kuwatoa wamasai katika eneo hilo kwa nguvu jambo lililopelekea jamii ya wafugaj wa kimaasai kupata hasara kubwa ikiwa ni pamoja na kunyimwa kulisha na kunyesha mifugo yao katika eneo hilo. Tangu kumalizika kwa operesheni hiyo, serikali iliendelea kufanya michakato mbalimbali kuhusiana na eneo hilo yenye malengo ya kufanikisha azma yao ya kuhakikisha kuwa eneo hilo linatengwa kutoka katika ardhi ya vijiji na kuachwa chini ya Kampuni ya Kiarabu, OBC kwa ajili ya utalii wa Uwindaji.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]MADHARA YATOKANAYO NA WANANCHI KUONDOLEWA KWA NGUVU LOLINDO MWAKA 2009[/FONT] [FONT=&quot]Kutokana na operesheni ya kuwaondoa wananchi, wafugaji wa kimaasai katika ikolojia ya Serengeti ili kupisha biashara ya uwindaji kwa Kampuni ya OBC, wananchi waliathirika kwa kiasi kikubwa na yafuatayo ni baadhi tu ya madhara walioyapata;[/FONT] [FONT=&quot]1. [/FONT][FONT=&quot]Usumbufu kwa wananchi;[/FONT] [FONT=&quot]2. [/FONT][FONT=&quot]Zaidi ya nyumba za wamasai 350 zilichomwa moto na kuteketea kabisa;[/FONT] [FONT=&quot]3. [/FONT][FONT=&quot]Zaidi ya watu 20,000 walikumbwa na mkasa huo na kuondolewa kwa nguvu,[/FONT] [FONT=&quot]4. [/FONT][FONT=&quot]Zaidi ya asilima hamisini (50%) ya mifugo iliyokuwepo katika eneo hilo ilikufa kutokana na kukosa malisho ya kutosha na maji;[/FONT] [FONT=&quot]5. [/FONT][FONT=&quot]Baadhi wa watoto walipotea wakati wa operesheni;[/FONT] [FONT=&quot]6. [/FONT][FONT=&quot]Kuharibika kwa mimba za akina mama kutokana na hofu na mstuko;[/FONT] [FONT=&quot]7. [/FONT][FONT=&quot]Watu wengi kuchapwa na kudhalilishwa, na kijana mmoja Ngodidyo Roriken alipigwa risasi ya jicho na kusababishiwa ulemavu wa jicho moja;[/FONT] [FONT=&quot]8. [/FONT][FONT=&quot]Watu wengi walishtakiwa na kubambikiziwa kesi ya kuingia eneo la liliodaiwa laOBC angali ni eneo la vijiji.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]HATUA ZILIZO CHUKULIWA NA SERIKALI BAADA YA OPERESHENI[/FONT] [FONT=&quot]Pamoja na operesheni kushindwa kuwaondoa wananchi katika eneo hilo, serikali iliendelea kuhakikisha kuwa inatimiza azma yake ya kutenga eneo hilo, kwa manufaa ya OBC. Baadhi ya michakato ambayo serikali iliendelea nayo baada ya opereshi ni pamoja na;[/FONT] · [FONT=&quot]Kutuma tume mbalimbali kuchunguza mgogoro bila kutoa wala kueleza matokea ya uchunguzi wa tume hizo kwa umma wala kwa mamlaka husika.[/FONT] · [FONT=&quot]Mwaka 2010, serikali kupitia kwa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro iliandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya wilaya, mpango ambao ulilenga kutenganisha ardhi ya vijiji na eneo hilo la ikolojia ya Serengeti na kuanzisha korido ya wanyama ambayo itakuwa ikitumiwa na OBC kuwinda wanyama. Mpango huu ulikataliwa na wananchi kupitia baraza la Madiwani, kwani haukuwa shirikishi na ulikuwa vigumu kuanzisha mpango wa matumizi bora ya ardhi ya wilaya kabla ya mipango ya vijiji kutengenezwa.[/FONT] · [FONT=&quot]Mwaka 2011, serikali iliandikia vijiji vyenye vyeti vya ardhi ya vijiji, vya Ololosokwan na Ngaresero barua na kuzitaka kurudisha vyeti vyao ili kuvibatilisha kwa lengo la kufanikisha na kurahisisha uundaji wa korido ya wanyama.[/FONT] · [FONT=&quot]Kuanzishwa kwa mpango wa kuwatumia viongozi ndani ya jamii kuahamasisha jamii kuondoka ili kupisha serikali kuanzisha korido ya wanyama. Jamii kupitia mikutano yao vijiji vilikataa mpango huu baadhi ya viongozi kutumika na serikali na OBC kutaka kuwahamisha wananchi katika eneo hilo la ikolojia ambalo ndilo eneo la malisho ya mifugo kwa miaka mingi.[/FONT] · [FONT=&quot]Kutokana na michakato hiyo yote kuonekana kushindikana, bado serikali haijatolea uamuzi mgogoro huu, jambo linalosababisha wananchi kuishi kwa hofu kubwa bila kufahamu hatima ya maisha yao.[/FONT] [FONT=&quot]MAPENDEKEZO[/FONT] [FONT=&quot]Kutokana na hayo, sisi mashirika yanayojishughulisha na utetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania tunaunga mkono kampeni za mtandao wa kimataifa wa Avaaz na kuitaka serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya yafuatayo:- [/FONT] [FONT=&quot]1. [/FONT][FONT=&quot]Kuacha mara moja mpango wa kuigawa ardhi ya vijiji kwa ajili ya kuanzisha korido ya wanyama kwa malengo ya kuwanufaisha wawekezaji wa OBC.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]2. [/FONT][FONT=&quot]Serikali iandae mpango shirikishi wa matumizi bora ya ardhi utakao zingatia maslahi na mahitaji ya wanaviijiji wote. [/FONT] [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]3. [/FONT][FONT=&quot]Mikataba yote inayohusu shughuli za uwindaji katika eneo husika iangaliwe na kuridhiwa upya ili kuzingatia haki, matakwa na maslahi ya wananchi juu ya rasilimali husika. [/FONT] [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]4. [/FONT][FONT=&quot]Mapendekezo ya Kamati na Tume mbalimbali ziliyotembelea eneo hilo yawekwe wazi na kutekelezwa ili tija ya matumizi ya kodi za wananchi ionekane.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]5. [/FONT][FONT=&quot]Serikali iache tabia ya kutumia nguvu kila wakati kunapokuwa na mvutano ama mgongano wa maslahi kati ya wananchi na wawekezaji. [/FONT] [FONT=&quot] [/FONT]
   
Loading...