Obama kaacha uozo mkubwa-D.Trump!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Raisi wa 45 D.Trump amesema (kuanzia ~ dakika 1:00) Raisi aliyepita Barack Obama ameacha uozo mkubwa haijawahi kutokea, amesema Obama ameacha uozo ndani na nje ya USA!

BillionaireBromance.png
 
Na bado amekuwa among the best 12 presidents kati ya 44 presidents wote waliotangulia, are you kidding us? Unemployment level ya 4% na Bush aliacha 7.8%. Ni nzuri ukatoa numbers kujustify shutuma zako.
kuna sehemu wamemuweka katika maraisi
wabovu 10 waliopata kutokea katika nchi hiyo
 
kuna sehemu wamemuweka katika maraisi
wabovu 10 waliopata kutokea katika nchi hiyo
Unatarajia Warepublicans wasemeje kuhusu Obama? Angalia chanzo cha taarifa kina mlengo gani wa kisiasa.
 
kuna sehemu wamemuweka katika maraisi
wabovu 10 waliopata kutokea katika nchi hiyo

Men lie, women lie pia ila numbers don't. Hiyo conclusion yao iko supported na numbers? GOP hawawezi kumkubali Obama hata siku moja lakini hawana facts kusupport hiyo chuki yao may be alternative facts.
 
Siasa za marekani tuwaachie wenyewe wamarekani. Wao ndio vinara wa democrasia duniani lakini vitu vingi vya kidemocrasia wanavifanya katika njia wanayojua wenyewe tofauti na democrasia ya kiafrika. Kwa mfano uchaguaji wa rais wananchi wanapiga kura lakini electroral college ndiyo yenye maamuzi ya mwisho ya nani awe rais.
 
Wamarekani huwa hawaishiwi na vituko.
Hivi Trump anahisi George Bush alimuachia Barack Obama Paradiso??
Ukiwatoa Franklin Roosevelt na Ronald Reagan hakuna raisi wa Marekani aliyewahi kumuachia mwenzake nchi ikiwa kwenye hali nzuri.
Marekani Obama ameacha ushoga,kusagana na ndoa za jinsia zimekithiri,nje ya marekani ameacha vita,huko Libya,Syria na ISIS wakiwa katika ubora wao.Huku Russia ikiichukua Cremea na kuiacha Ukraine kwenye vita.
 
Obama ni Raisi wa kwanza Shoga -Newsweek!

nw_052112_domcvr.jpg

'Wafuasi' wa Obama hawataki kabisa kuona ukweli huu unawekwa hadharani.
Niliwaambia tangu mwanzo kabisa kuwa jambo pekee ambalo Obama amefanikiwa ni kusambaza sera za oshoga duniani.
Watu hawataki kuamini......
 
Raisi wa 45 D.Trump amesema (kuanzia ~ dakika 1:00) Raisi aliyepita Barack Obama ameacha uozo mkubwa haijawahi kutokea, amesema Obama ameacha uozo ndani na nje ya USA!

BillionaireBromance.png

Sasa yeye ndio atauozesha kabisa
 
Marekani Obama ameacha ushoga,kusagana na ndoa za jinsia zimekithiri,nje ya marekani ameacha vita,huko Libya,Syria na ISIS wakiwa katika ubora wao.Huku Russia ikiichukua Cremea na kuiacha Ukraine kwenye vita.

Hebu tukumbushane kidogo ili tuwekane sawa katika hili:
Mosi, Rais George W Bush aliacha vita ngapi nje ya nchi?
Unajua ile vita imeharibu Uchumi wa Marekani kwa kiasi gani?
Ukipata jibu la hili basi huwezi kumrushia mpira Rais Barack Obama peke yake.

Pili,Nguvu ya Urusi hata Rais George W Bush alikutana nayo na wala hakufanya chochote.
Mwaka 2008 Urusi ilivamia Georgia na kuyamega majimbo ya South Ossetia na Abhkazia na Marekani aliishia tu kulalamika na hakufanya kitu mpaka leo. Mbona hili hujalisema na umeishia tu kuzungumzia Crimea?

Tatu, Ugaidi Mashariki ya Kati haukuanza leo na tunaweza kujiaminisha kwamba chanzo cha Radical Islam ni kuvamiwa kwa Iraq, Libya, Afghanistan na Syria. Lakini ukweli ni kwamba hizi ni sababu chochezi na za muda mfupi (The Straw that Breaks the Camel's Back). Nakuhakikishia kwamba tangu kuisha kwa Vita ya Pili ya dunia mwaka 1945 hakuna siku ambayo Mashariki ya kati imewahi kukaa kwa amani bila kuwepo kwa Ugaidi na makundi ya Kigaidi:
Kama ipo itaje tuijue wote ili tuweze kumlaani Rais Barack Obama kwa kutuletea Ugaidi hapa duniani.

Nne, Ushoga na Usagaji hata hapa Tanzania upo na ulishika hatamu sana kipindi cha Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Hili mbona wewe hujaliona?
Kwanini unataka kutoa Kibanzi kwenye jicho la Mwenzio wakati wewe una Mboriti jichoni mwako?
 
Men lie, women lie pia ila numbers don't. Hiyo conclusion yao iko supported na numbers? GOP hawawezi kumkubali Obama hata siku moja lakini hawana facts kusupport hiyo chuki yao may be alternative facts.
ingia google andika worst us president ever
utapata majibu na uzuri wao huwa wanatoa
reason kabisa
 
Na bado amekuwa among the best 12 presidents kati ya 44 presidents wote waliotangulia, are you kidding us? Unemployment level ya 4% na Bush aliacha 7.8%. Ni nzuri ukatoa numbers kujustify shutuma zako.
Ni zaidi ya kusubiri meli ubongo.
 
Back
Top Bottom