Obama akiri kufanya jitihada za kuibua machafuko Iran

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
5,780
2,000
Obama akiri kufanya jitihada za kuibua machafuko Iran

Rais wa zamani wa Marekani amekiri katika kitabu chake kipya kwamba wakati wa utawala wake aliunga mkono kuibuliwa machafuko nchini Iran.

Rais Mstaafu wa Marekani Barack Obama ameandika katika sehemu moja ya kitabu chacke hicho alichokipa jina la "Nchi ya Ahadi" au A Promised Land kwamba, mwaka 2009 alishadidisha vikwazo vya kimataifa dhidi ya Iran. Katika kitabu chake hicho Obama amekiri kuwa alidhamiria kustafidi na wenzo wa vikwazo ili kushadidisha machafuko hapa nchini na aweze kuungwa mkono.

Kitabu cha "A Promised Land cha Barack Obama"

Kile kilichoandikwa na Obama katika katibu chake hicho kwa jina la "Nchi ya Ahadi" na nyaraka nyingine za uthibitisho ambazo zilichapishwa katika duru za nchi ajinabi kinaonyesha kuwa, serikali yake ilitaraji kuwa ingefanikiwa kutumia machafuko ya ndani ya Iran na kuishawishi nchi hii kufikia mapatano kuhusu miradi yake ya nyuklia.

Obama amebainisha hayo katika hali ambayo licha ya viongozi wa Marekani na nchi za Ulaya waitifaki wa White kutoa vitisho na propaganda za uongo za vyombo vya habari vya Magharibi; wananchi wa Iran walitoa jibu la nguvu kwa wafanya fitina dhidi ya nchi hii na waungaji mkono wao wa kigeni.

Tarehe 9 mwezi Dei mwaka 1388 iliyosadifiana na Disemba 30 mwaka 2009 inakumbushia maandamano ya mamilioni ya wananchi wa Iran katika kutangaza kujitenga kwao na wazushaji machafuko katika jamii; na kutoa jibu la wazi na kali kwa wazushaji machafuko ambao walifuata njia potofu kwa kisingizio cha kufanyika udanganyifu katika duru ya kumi ya uchaguzi wa rais hapa nchini.
 

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
3,146
2,000
Viongozi wengi wakimaliza madaraka yao wanaandika vitabu ambayo walishatenda huku wakijutia R.I.P mkapa
 

Chillah

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
5,631
2,000
Viongozi wengi wakimaliza madaraka yao wanaandika vitabu ambayo walishatenda huku wakijutia R.I.P mkapa
Tamaa walizo nazo na kutojali wengine... Una tenda kosa ukijua ni kosa kisa utakuja kutubu na watu washakufa kwa uzembe au maamuzi yako yasiyo na tija...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom