Nywele kuwa za rangi ya Brown

Nywele kuwa za rangi ya Brown

Wanakuja kukuambia wakijuacho
 
Zikiwa za brown zinauma?
Kama haziumi na hutaki kutumia super black achana nazo manake hakuna kitu utafanya ziwe nyeusi
 
Tatizo sio kuuma, unaonekana nywele chafu wakati muda huo umetoka kuziosha...Kwaiyo hakuna njia nyingine mbadala...

Inawezekana wapo wanaojua,mimi sidhani kama ipo namna nyingine zaidi ya super black
 
Dawa yake ni kunyoa mapema tu, mimi huwa ninazo nywele ambazo si nyeusi kiviile, zikiwa ndogo nyeusi zikirefuka weusi unapotea na huwa sina kawaida ya kupaka mafuta ya nywele, hata haya ya kawaida(ngozi) kupaka ni NTITI(kujisemea wamakonde) kwa ngozi namshukuru mungu nipake wese nisipake swaafi tu, kwa jiji la kwetu mwaka mzima unaweza katika sijapaka wese mwilini.

Ila nywele kidogo tu nyekundu.. Nasogea kwa mr. Kinyozi anazipunguza.
 
Kazi kwake mleta mada kama atakubaliana na wazo la kunyoa
Kama ana mpango wa kufuga afro awe mtu wa superblack au mafuta fulani hivi ya nywele niliwahi kuelekezwa ila sikutilia maanani sababu mie mwilini mwangu vikorombwezo vikorombwezo huwa sivizingatii. Ajaribu kuyasaka hayo.
 
Inawezekana aina ya maji unayo ogea Mkoa ulipo yanaleta hiyo athari , au ni mwili wako na genes / phenotype zake tu ??
 
Hivi nywele kuwa za rangi ya brown ni ugonjwa au ni nini hiki.

Na huwa mnaondokana vipi na hili tatizo maana usipochana unaonekana kama mtu wa jalalani..

Kupaka superblack ndo kitu sitaki hata kujaribu naombeni ushauri
Kwani tatzo ni nini, mie pia nywele zangu ni brown. Tena hadi huwa naulizwa kama nimepaka piko.
 
Worry out, hata mimi nilikuwa hivyo. Ni hali ya kawaida ila wengi hawajui tu.
 
Back
Top Bottom