Nyumbani kwa shujaa haviishi vilio

kofia ya plastiki

JF-Expert Member
Jun 9, 2019
416
404
Leo nitaongelea dhana hii katika approach ifuatayo, mara nyingi kwenye himaya ya shujaa vilio huwa ni vya mara kwa mara maana yeye mara nyingi anawindwa na maadui wa hapa na pale.

Tuje sasa kwenye kiini ya mada. Kijana umemaliza chuo umeenda kwa wazazi ukaona kwa kipindi hiki ambacho ajira zimesimama, bora ujichanganye town. Huu ni uamuzi wa kishujaa kwa maana wako wengine wale wa kupenda kugombea vitafunwa na wadogo zetu; hawajaondoka wapo tu nyumbani kwa wazazi wana-enjoy na free basics, or free of charge.

Lakini wewe shujaa umetoka ukiwa na nauli tu kwenda town ukafikia let say kwa mjomba ama rafiki lakini badae ukapata ya chumba, lakini sasa unapambana na bili za umeme maji kodi na ya kula bado usikate tamaa hata kama unadaiwa hela ya umeme, na hujui utaipata vipi wacha kukumbuka kurudi kugombea maandazi na madogo kwa wazazi endelea kupambana kesho yako ni tofauti na leo hivyo ndivyo vilio vyenyewe vya kudaiwa kodi ya chumba umeme, maji hela ya msosi usijali wewe ni shujaa. Vilio ni kawaida.
 
Asante Mkuu kwa thread nzuri. Lakini mbona dhana ya kuwa shujaa kama umeizungumza kuwa ni rahisi kuliko inavyostahili.

Au wachangiaji wengine watatuambia nini maana ya neno Shujaa.

Ila kama lengo ni kupeana moyo sio vibaya Mkuu.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu kujitosa mjini wakati umeacha nyumbani ulikua unakula na kulala bure ni dhana nyepes? Hasa kwa usawa huu? Au urahisi uko wapi?
 
mkuu kujitosa mjini wakati umeacha nyumbani ulikua unakula na kulala bure ni dhana nyepes? Hasa kwa usawa huu? Au urahisi uko wapi?

Basi Mkuu nilidhani ushujaa utakuwa na hadhi kubwa zaidi kuliko kukimbia chakula cha bure nyumbani. Kwa tafsirj nzuri uliyotuwekea, namshukuru Mungu mashujaa tuko wengi sana.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Basi Mkuu nilidhani ushujaa utakuwa na hadhi kubwa zaidi kuliko kukimbia chakula cha bure nyumbani. Kwa tafsirj nzuri uliyotuwekea, namshukuru Mungu mashujaa tuko wengi sana.

Sent from my iPhone using JamiiForums
ndo hivyo mkuu
 
Back
Top Bottom