Nyumba za kupanga uswazi/mkwara? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyumba za kupanga uswazi/mkwara?

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Makaimati, Apr 15, 2011.

 1. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hodi hodi hodi Wanajamii,

  Hiki ni kisa cha kweli kimetokea huku kwetu.

  Endelea kusoma tafadhali:

  Kuna mama mmoja alikuwa na nyumba ya kupangisha karibu na nyumba yake alokuwa anaishi. Wapangaji wake wengi walikuwa Askari Polisi kwa sababu ilikuwa pia jirani na Kituo cha Polisi

  Bahati mbaya hawa wapangaji walikuwa hawadumu kwa sababu huyu mama alikuwa anapenda kutukana tukana sana.

  Akatokea Askari mmoja aliehamishiwa hapa na akitafuta nyumba ya kumtosha na familia yake kubwa. Askari wenzake wakamuelekeza kwa yule bibi huyu wakijiuliza huyu jamaa mpole sana ataweza? Pia walimueleza hio hali lakini kwa shida alokuwa nayo ikabidi aende tu

  Jamaa kufika pale, yule mama akamwambia, "Baba nyumba nnayo lakini utaiweza?

  Askari akauliza, "Kwanini mama?"

  Mama akajieleza, "Baba mimi natukana sana, ndio ila yangu?

  Askari akamwambia, "Nadhani tutawezana mama maana na mimi ila hio nnayo lakini mimi nimekuzidi kidogo"

  Mama kataka kujua, Enhe kwa vipi?"

  Askari akamalizia, "Na kupiga mimi napiga pia"

  Askari huyo ameishi nyumba hio na kuzaa watoto watatu humo ndani na amehama mwenyewe kurudi kijijini kwao baada ya kustaafu kazi hivi karibuni.

  Mkwara unafaa jamani!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 2. Khalifab

  Khalifab Member

  #2
  Jul 8, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duuh kwerrrrrri ma mikwara sometme sana 2
   
 3. grafani11

  grafani11 JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2012
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 15,534
  Likes Received: 342
  Trophy Points: 180
  Isijekuwa huyo bibi ndiyo mama watoto hao watatu. Chezea njini wewe.
   
 4. Mtanzanika

  Mtanzanika JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 2,211
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Nguvu huna ....HERRRRRAAAAAA huna....Hata MIKWARrrrRRRRAAAAAAAAAA!!!!
   
Loading...