Naomba nikushauri siku nyingine ukipita kwenye thread ambayo maudhui yake inafana fanana na hii, jaribu tu na wewe kuji-comouflage ili uonekane kama na wewe unafanana na mashuhuda wa kwenye thread husika. Jaribu kufanya hivyo hata kama ulikulia Ikulu. Mimi nimelelewa na Babu mzaa mama, na alikuwa na ng'ombe kiasi, kiasi kwamba haikuwa shida kunywa maziwa, au kula mboga ambayo maji yaliyotumika kuipika ni maziwa. Still, Babu alitufundisha kuwa ukifika kwenye nyumba ambayo hali yao ya maisha haifanani na ya nyumbani kwenu, na pengine ukakuta wanakula mboga kauzu ambayo haijawekewa viungo ambavyo ulishazoea kula nyumbani, UNATAKIWA ULE NA BILA KUONYESHA DALILI YOYOTE KUWA CHAKULA UNACHOKULA NI TOFAUTI NA KILE ULICHOZOEA KULA SIKU ZOTE. Hiyo ndiyo falsafa Babu yangu aliniachia, na ninaendelea kuitumia hadi leo. Kwa hiyo ukikuta watu wana-share experiences za maisha yao waliyopitia na ukaona kuwa yalikuwa ya shida kidogo, bora upite tu bila kuchangia, kuliko kuchangia katika hali ambayo itaonyesha kuwa unawatambia kuwa wewe maisha yako yalikuwa juu kuliko wao! Wasukuma waliolelewa katika maadili, na hata watu wengine wowote waliolelewa katika maadili, huwa hawako hivyo!