Nyumba za kulala wageni si salama

Nyumba za kulala wageni si salama

Jambo hili wengi wetu hatulijui, nyumba nyingi Sana za kulala wageni maarufu Kama Guest House si salama, nyingi zimezingirwa na kuwekewa maagano ya nguvu za giza ili wamiliki wajipatie pesa Kwa njia rahisi zaidi.

Zipo nyingine mtu akilala tu haamki anapitiliza kwenye mauti jumla, zingine ukilala, nyota yako inaibwa na kutumiwa na mmiliki, Kama ulikuwa na pesa au hata mafanikio unashangaa mara umeanza kuanguka kimaisha.

Haya yote yanafanyika ktk ulimwengu wa roho ambao huwezi kuuona Kwa macho ya kawaida.

Kitanda, godoro na yale mashuka yanakuwa na maagano maalumu yamewekewa, ndo maana unaweza kukuta mwanaume au mwanamke anayesafiri mara nyingi Sana anabadilika tabia yake ghafla.

Pengine alikuwa mstaarabu akiiheshimu ndoa yake vizuri Sana mara anageuka na kuwa malaya wa kutupwa.

Si yeye, ni zile roho za mapepo zinakuwa zimemvaa Kwa malengo maalumu ya kuzimu ili watu wafanikiwe ya kwao.

Unaweza kumwona mlevi, kumbe kulewa kwake kunamtajirisha mtu flani.

Hata ma Hotel pia ni hatari Sana, ni maagano yale yale ya Guest House, jaribu kuchunguza tabia za watu wengi, walibadilika wakati gani? jibu utalipata kuwa ni baada ya kusafiri safiri Sana.

Hata hizi Nyumba za kawaida si nzuri pia, usipende kununua nyumba, jenga ya kwako, huwa mara nyingi watu wananunua nyumba ambazo tayari zina maagano ya kuzimu yaliyowekwa na wamiliki wa awali.

Tuweni makini Sana, tunaishi ktk dunia ngumu Sana.
Mtu akisafiri anajifunza mengi sana usitegemee atakuwa vile vile travelling ni sehemu ya kujifunza tamaduni mbalimbali, Hii thread ni upotoshaji tu Umeongea assumption kuliko Facts
 
Kwa nini uishi kwa kuogopa ogopa? Yesu ndio kiboko ya hirizi zote, ukiwa nae hata iwe gest ya Mke wa Shetani huwezi pata shida
 
Ingekuwa busara ukaweka utatuzi na angalizo, kuliko kuishia juu juu tu namna hiyo kama tamthilia.

Ni kweli hayo maagano yapo, ila tufanyaje sasa?

Nyumba za wageni hazina tatizo kama unaenda pale kwa matumizi halali, mfano wale wakristo wanajua, hata Bikira Maria na Mumewe Yosefu, walifikia kutaka kupanga nyumba za kulala wageni, ila wakakuta zimejaa, Mama yule akaenda kujifungulia katika zizi la Ng'ombe.
Luka 2:6-7

Hili linathibitisha ya kuwa, hizo nyumba zilikuwepo karne nyingi zilizopita, hata kabla ya Yesu Kuzaliwa.
 
Tunatakiwa kufanya haya, ila tukiwa wasafi kimwili na kiroho;

1. Kuvunja nguvu zote za giza mahala hapo, hii inamaanisha tuwe wenyewe labda wenye uelekeo safi, yaani haiwezekani uvunje nguvu za giza, huku umelewa, una mwanamke kimada na mpo tayari kwa uzinzi, n.k

2. Uliye / utakayekuwa naye hapo ni mkeo ama mumeo, yaweza kuwa ni mfanyabiashara mwenzio, ila hamuingii humo kwa dhumuni la kupumzishana.

3. Hatuwezi kuepuka hila za ibilisi popote pale wakati tupo hai bado, ila tunachofanya ni kuomba tu ulinzi wake Mungu, maana kila unapopajua wewe, ibilisi yupo na wakala wake, hata kwenye nyumba za ibada.

4. Tukae chini tujifunze Ukuu wa Mungu, katika dini yako hiyo uliyopo, na tusiwe watu wa mizuka na kuogopax2, maana hatuna pa kukimbilia tukiwa humu duniani.

5. Unaweza kusema mf, 'kwa Jina la Yesu, shetani haniwezi', wakati huox2 umetoka kufanya dhambi na mshitaki wako kwa Mungu ni huyo huyo shetani.

Ahsante!
 
Maandiko ya kusimamia ni mengi, ila jambo la busara zaidi, ni sisi kukaa chini na kujifunza kinagaubaga juu ya uwezo wake Mungu.

Siyo lazima tuwe wote Wachungaji, Mashekhe, Waalimu wa Dini, Mapadre, n.k n.k, ila tunaweza kujifunza tu ya kawaida kumuhusu Mungu na tukafaidika.

Unajua wengi wetu hatuna elimu ama uelewa huo, ndiyo maana anaweza kuja mtu humu akatisha watu na watu wakatishika kweli, kama mnavyoona dini nyingi zinavyoanzishwa, ni kwa sababu ya elimu ya matisho na kujitoa muhanga. Elimu elimu elimu ya Dini ndiyo itakayotuokoa.

Ahsante!
 
Kujitoa muhanga, siyo kujilipua ama kujiua ama kulipua na kuua wengine tu, inaweza pia kuwa mnalishwa wadudu, panya, mende, majani na mengine machafu kama hayo na kuhatarisha afya zenu.

Ama mnaaminishwa mkiumwa msiende Hospitali, ama mnaweza kwenda popote duniani bila vibali maalumu, n.k.

POLENI KAMA NIMEHUBIRI SANA, ILA NAPENDA TUWEKANE SAWA, TUSIOGOPE OGOPE HOVYO.

Ahsante!
 
Hizo pepo ni laana ya uzinzi na si kwasababu ya guest house, guest house ni nyumba kama nyumba zingine, hazina tatizo kabisaaaaaaaaaaa, usiwatishe watu, bali waambie ukweli kuwa dhambi ndiyo mbaya, lakini si guest house, ikumbukwe mtu dhaifu ndiyo anaeingiwa na pepo, hayo unayoyasema yote ni nadhalia tu,Napinga kabisa hoja yako...hapo NI SAWA NA KUCHUKIA MAJAGI YOTE KISA KUNA MTU MMOJA ULIMWONA KABEBEA MADAWA YA KULEVYA AMA POMBE,...Ni guest ni chombo tu, inategemea na matumizi yako mkuu, Pepo ni laana, na laana ipo sehehemu yeyote mkuu, na laana ni umauti.
UMAUTI NI NINI?
mauti ni kifo-chaweza kuwa ni kifo cha biashara,mali,n.k, Mauti hutumwa, soma Ufunuo 6:8 ''utagundua yohana aliona KIFO kimepanda farasi" kumbe basi KIFO kinaweza kutumwa, kifo kinaweza kukimbia,Kifo kinaweza mfuata mtu, kwahiyo basi-hapa tunafundishwa kuwa-KIFO kinaweza panda daladala,kifo kinaweza panda basi, kifo kinaweza panda ndege, kifo kinaweza ingia katika nyumba za wageni, kifo kinaweza ingia NYUMBANI UNAPOISHI ...Usiogope KIFO, ogopa Roho zisababishayo kifo/Roho zitumwazo kukuangamiza, Ogopa dhambi,
Ukisoma 2 wafame 40-41 "Basi wakawapakulia hao watu ili wale.ikawa,walipokuwa katika kula chakula.wakapiga kelele,wakasema,Mauti imo sufuriani,Ee mtu wa Mungu. wala hawakuweza kula. lakini yeye akasema,leteni unga. Naye akautupa ndani ya sufuria:akasema wapakulie watu,ili wale.wala hakikuwamo kitu kibaya sufuriani"...Hapo tunajifunza kwamba ROHO YA MAUTI ilikuwamo sufuriani,..WALIONDOA ROHO YA KIFO NA SI SUFURIA ZIMA....Kama una unamwamini Mungu wako, kemea hiyo Roho, usitende dhambi...maana biblia imeandikwa -HAMTA KUFA BALI MTAISHI..MSIOGOPE..Ili ufe lazima kuwe kuna chanzo. kifo cha biashara kina chanzo, kifo cha kazi yako kina chanzo, kifo chochte kina chanzo,Kemea vyanzo vya kifo ambavyo ni dhambi...IKUMBUKWE ..CHANZO CHA KIFO NI HOFU....wewe kama una mke/mme wako wa ndoa Guest unahofu gani? tena nikwambie unaweza piga saana hadi mkanena kwa lugha...Msiogope Guest wapendwa, bali ogopeni ile dhambi nanyi mtaishi. Kama umebarikiwa na hii ebu sema AMINA OOH HALELUYAAAAH.
 
Nilidhani unasema labda wanawake kamera za kurekodi... kama ni maagano tu, watabeba mashuka yao...
 
Nilidhani umeongelea wizi ktk haya maeneo, yena wizi wa kupangwa na receptionist na watu wake au hata mmoliki wa guest na watu wake kuwaibia na kuwatapeli wateja wao, ila kama ni suala la nguvu za giza, ni imani tu!
 
Kila kitu ni hatari siku hizi...haya maisha yanakua magumu kweeli..
 
Kuna wengine wamejenga Nyumba nzuri tu lakini wameshindwa kuhamia kwa sababu ya eneo walilojengea Nyumba zao, eneo la kimaagano ya kishetani au lango la kuzimu nk
Kabla ya kujenga muulize Mungu
A BRAIN/ MIND IS A VERY POWERFUL TOOL, kama umeamua kujiaminisha hivyo, ubongo wako utakuongoza unavyotaka na UTAAMINI HIVYO HIVYO.
 
Kana vile wachangiaji wengi twapishaba ba mtia mada, yawezekana na mimi pia. Maudhui ya mada ni uwepo wa nguvu za giza katika "guest/hotel". Mtoa mada na wachangiaje wengine wameongeza nyumba na hata Mabus, mh! Ukiamini haya hutoamini kuwepo kwa vitu hivyo hata maofisi. Tujiamini kwa kuwa hivi vimeundwa/kujengwa na binadamu. Ukiamini ya mada utaaminina wale kiungo cha albino (na mambo mengine ya kiinani) huleta utajiri.
 
Jambo hili wengi wetu hatulijui, nyumba nyingi Sana za kulala wageni maarufu Kama Guest House si salama, nyingi zimezingirwa na kuwekewa maagano ya nguvu za giza ili wamiliki wajipatie pesa Kwa njia rahisi zaidi.

Zipo nyingine mtu akilala tu haamki anapitiliza kwenye mauti jumla, zingine ukilala, nyota yako inaibwa na kutumiwa na mmiliki, Kama ulikuwa na pesa au hata mafanikio unashangaa mara umeanza kuanguka kimaisha.

Haya yote yanafanyika ktk ulimwengu wa roho ambao huwezi kuuona Kwa macho ya kawaida.

Kitanda, godoro na yale mashuka yanakuwa na maagano maalumu yamewekewa, ndo maana unaweza kukuta mwanaume au mwanamke anayesafiri mara nyingi Sana anabadilika tabia yake ghafla.

Pengine alikuwa mstaarabu akiiheshimu ndoa yake vizuri Sana mara anageuka na kuwa malaya wa kutupwa.

Si yeye, ni zile roho za mapepo zinakuwa zimemvaa Kwa malengo maalumu ya kuzimu ili watu wafanikiwe ya kwao.

Unaweza kumwona mlevi, kumbe kulewa kwake kunamtajirisha mtu flani.

Hata ma Hotel pia ni hatari Sana, ni maagano yale yale ya Guest House, jaribu kuchunguza tabia za watu wengi, walibadilika wakati gani? jibu utalipata kuwa ni baada ya kusafiri safiri Sana.

Hata hizi Nyumba za kawaida si nzuri pia, usipende kununua nyumba, jenga ya kwako, huwa mara nyingi watu wananunua nyumba ambazo tayari zina maagano ya kuzimu yaliyowekwa na wamiliki wa awali.

Tuweni makini Sana, tunaishi ktk dunia ngumu Sana.
😰😢
 
Imani km hz nazo ni ushirikina tu km ilivyo kupaa na ungo tu
 
Back
Top Bottom