Nyumba ya kisasa haitakiwi kukosa vifaa hivi

usalama kwanza

JF-Expert Member
Oct 3, 2012
386
158
Kila mtu anapenda kuwa na nyumba nzuri , ya kisasa na inayopendeza , lakini kuna jambo moja ambalo wamiliki wa nyumba au mafundi wanaohusika kwenye ujenzi huwa hawatilii maanani.

Leo nataka nikukumbushe nyumba ya kisasa au nyumba yoyote ile haitakiwi kukosa mitambo ya kisasa ya ulinzi iwe ni Alarm systems, CCTV cameras , Fire alams , Electric fence au nyinginezo.

Kwanini uweke mitambo ya usalama kwenye nyumba yako.

i) Usalama ni swala la muhimu binadamu yoyote ndio maana watu huweka milango , nondo/ grill na vioo kwenye hii yote ni kujilinda dhidi wezi/vibaka, wanyama.

ii) Nyumba za kisasa hushawishi wahalifu kwani huamini ya kuwa kuna mali za thamani kubwa katika nyumba husika.

iii) Nyumba za kisasa hujengwa kwa gharama kubwa sana hivyo ni muhimu kujikinga dhidi ya majanga yasababishayo hasara kama moto.

iv) Uvamizi au majanga kama moto, husababisha madhara makubwa kama vifo, majeruhi na upotevu mkubwa wa mali.

v) Mitambo ya kisasa kama CCTV cameras hukusaidia mwenye nyumba au mmiliki kutambua hatari zinazokuzunguka na kutambua wezi au matukio hatarishi katika eneo lako

vi) Alarm system zitakupa uwezo wa kugundua uvamizi katika mazingira yako. Alarm system za kisasa huja na mitambo ya mawasiliano jambo ambalo litakuwezesha kufuatilia usalama wa nyumba yako hata utakapokuwa mbali na vyumbani.

vii) Mitambo ya kisasa ya usalam ni nafuu , inayofanya kazi kwa uhakika na hukupa uhakika wa usalama katika nyumba yako.

N.B : Kwa mahitaji ya vifaa vya kisasa vya kiusalama tuwasiliane kwa namba 0714890018

Isecure Technology

0714890018

Justine@isecuretec.com
 
Duh, yani umeanzia mbaaaaaaaali alafu mwisho wa siku unaomba "hela" ok ahsante.
 
Karibuni mjipatie alarm na tracking system bora zaidi tanzania. Hivi karibuni nitatangaza ofa kwa ajili ya vifaa vya usalama majumbani, maofisini na tracking system . Nipigie 0714890018 kwa maelezo zaidi
 
Mm kinacho nishinda kwenye matangazo ya humu JF ni kukosa hata makadirio ya chini au ya juu bei.

Mf, room 2 au 3. Gorofa 2 , 3,4, nk CCTV Cameras angalau tujipange tukuite oneday au kama iko ndani ya uwezo tuwasiliane. Matangazo mnaweka wazi, bei eti piga no hiyo hapoo!! LOOH
 
kweli ni ngumu kumfurahisha kila mtu ,ningepost naweka alarm system, cctv na namba ya simu mngeponda hamna maelezo ya kutosha. Sasa nimeweka maelezo ya kutosha mnaponda kuwa nimeanzia mbaaali
'Mteja ni mfalme', 'daima mteja yuko sahihi'. Umeshaweka tangazo lako, subiri wateja na isiwaoneshe wateja wako kuwa huna subira na watu wanapouliza au kuchangia lolote juu ya tangazo lako hata kama hawaongei kwa uzuri
 
Mm kinacho nishinda kwenye matangazo ya humu JF ni kukosa hata makadirio ya chini au ya juu bei.

Mf, room 2 au 3. Gorofa 2 , 3,4, nk CCTV Cameras angalau tujipange tukuite oneday au kama iko ndani ya uwezo tuwasiliane. Matangazo mnaweka wazi, bei eti piga no hiyo hapoo!! LOOH

Labda niliweke hivi ni ngumu sana kuweka bei ya vyote sababu kama ni cctv inategemea na specification za mteja na eneo , mfano mtu anaweza kukwambia anahitaji kamera moja au mbili lakini ukifika eneo la kazi unagundua kuwa zinahitajika kamera zaidi ili mpangilio wa usalama ukae vizuri . Lakini pia kuna mtu atahitaji kuhifadhi data kwa miezi mitatu , sita , kuna aina ya kamera, dvr ndio maana inakuwa ni vizuri kutembelea eneo la kazi. Muda si mrefu nitatoa ofa zikiwa na makadirio ya bei ya nzuri lakini kwa haraka naweza kukuweke ccctv ya camera nne kwa 1.5m , camera mbili 0.9M unapolipia hiyo ni kuwa utapata kazi iliyo kamilika na kitu kama car tracking system ni laki 3. Karibu ndugu
 
Back
Top Bottom