Nyumba tatu za vigogo kubomolewa ili kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Nyumba za aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Botswana, mmiliki wa Hoteli ya Peacock na Mkurugenzi Mstaafu wa BoT zilizopo Mbezi kubomolewa.

---------
Nyumba tatu za vigogo zilizopo eneo la Mbezi kwa Msuguri na Mbezi kwa Yusufu zimewekewa alama ya X kwa lengo la kubomolewa ili kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro inayoanzia Mbezi hadi Kiluvya.

Vigogo hao ni balozi mstaafu wa Tanzania nchini Botswana, Gracian Rutha, mmiliki wa Hoteli ya Peacock iliyopo eneo la Mnazi Mmoja jijini hapa, Joseph Mfugale pamoja na mkurugenzi mstaafu katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mukola Nkulu.

Hizo ni miongoni mwa nyumba nyingi zinazotakiwa kubomolewa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kutokana na kuwa ndani ya hifadhi ya barabara ya mita 121.5 kila upande.

“Hakuna nyumba ya mkubwa katika nchi hii, ambaye nyumba yake iko kwenye hifadhi ya barabara itaachwa, itabomolewa tu,” ni kauli ya mhandisi mkuu Tanroads Mkoa wa Kimara, Jonson Lutechura.

Waandishi wetu walifika nyumabani kwa Balozi Rutha na kupokewa na Ombeni, kijana aliyejitambulisha kuwa ni mtoto wa balozi huyo.

“Ni kweli hapa ni nyumbani kwa Balozi lakini alishastaafu. Nyumba yake kweli itavunjwa lakini Balozi ametoka muda kidogo,” alisema kisha akatoa namba za simu za Balozi huyo ili atafutwe kwa maelezo zaidi.

Alipotafutwa balozi huyo alisema, “Ni kweli nyumba yangu inavunjwa lakini siwezi kuongea chochote kwa sasa kwani nipo kwenye kikao, mnaweza kunitafuta kesho,” alisema.

Waandishi wetu pia walifika nyumbani kwa Mfugale na kukuta ukimya ukiwa umetawala kana kwamba hakuna mtu.

Nyumba nzuri ya ghorofa moja iliyopakwa rangi nyeupe na kupambwa na madirisha ya vioo, huku ikizungushiwa uzio mkubwa, nayo imechorwa alama kubwa ya X na maandishi ya rangi nyekundu yaliyosomeka, “Bomoa Tanroads DSM” kila upande wa nyumba hiyo.

“Hodi” waandishi walibisha lakini ukimya ulizidi kutawala kiasi cha kudhani kwamba huenda hakuna mtu, mara sauti ya kukaribishwa ilisikika.

“Karibuni, tuwasidie nini? Alikaribisha na kuhoji mama mmoja ambaye baadaye waandishi walielezwa kuwa ni mtoto wa kigogo akitaka kujua wageni hao kina nani na wametoka wapi.

Baada ya kujitambulisha, mama huyo alisema baba yake hayupo na kwamba hawezi kuzungumza chochote mpaka awasiliane naye.

“Baba hayupo naomba kwanza tuongee naye,” alisema kisha akatoa simu na kupiga, “Baba kuna waandishi wametoka gazeti la Mwananchi wamekuja hapa wanaulizia kuhusu bomoabomoa.”

Baada ya dakika moja alimpa simu hiyo mwandishi ili azungumze na na baba yake.

“Samahani baba tunafuatilia kuhusu nyumba yako kuwekewa alama X,” alisema mwandishi aliyepokea simu hiyo.

Mfugale alijibu, “Kwanza niseme mimi siwezi kubomoa nyumba yangu mpaka nilipwe.”

Alisema alijenga nyumba yake hiyo tangu mwaka 1996 akisema kipindi hicho, sheria ilikuwa ni mita 30 na nyumba yake ilikuwa mbali kabisa na umbali huo na kulikuwa na mawe ya mpaka wa barabara.

“Baadaye tukaletewa hiyo sheria ya mita 121 ambayo hatujui ilitoka wapi, kiukweli mimi nasema tena siwezi kubomoa mpaka nilipwe na wala siwezi kuhamisha familia yangu mpaka siku watakapokuja wao kunibomolea,” alisema.

Mfugale alisema nyumba yake ina vyumba vitatu na ni ghorofa moja.

“Kiukweli inaumiza sana kuona nyumba nzuri inataka kubomolewa, lakini utafanyaje ndiyo maendeleo, ninachoomba tu Serikali iwaangalie watu waliojenga wakati wa mita 30 kwani walijua wako nje ya barabara hivyo iwafikirie kuwalipa fidia,” alisema.

Tulifika Mbezi kwa Msuguri, Nyumbani kwa Nkulu ambaye alistaafu BoT tangu mwaka 1992, na tulipomkuta alieleza alivyonunua kiwanja katika eneo hilo tangu mwaka 1976 na kujenga mwaka 1980 akisema kuwa kipindi hicho eneo hilo lilikuwa pori.

“Nataka kujua hao watu wa Tanroads wametumia sheria ipi, katika kuweka hizo alama za X kwenye nyumba ambazo wanadai zipo kwenye hifadhi ya barabara,” alihoji.

Alisema kwa mujibu wa taratibu na sheria, Serikali inapotaka kuchukua eneo lolote inatakiwa ikae na wanachi, ijadiliane nao kisha wakubaliane na kuwalipa fidia kwa kuzingatia tathmini iliyofanywa kwa mujibu wa sheria.

“Sasa wanataka sisi tubomoe wakati tumejenga hapa miaka mingi, wanataka twende wapi? Hatukatai mpango wa Serikali, basi itulipe hata fidia ili tujue tutaanzia wapi,” alisema.

Mwananchi
 
hii bomoa bomoa ina mkwara kuliko zote.. nyumba zenyewe hazibomolewi ila zaidi ya miezi 6 ni mikwara tu...

mara mama ana mkapa, mara prof jay, mara balozi, mara mkurugenzi, mara tanesco wamekata umeme kupisha bomoa bomoa.. mara dawasco...

maneno mengi tu ya mkwara.. mbona bomoa bomoa zingine hazinaga mbwembwe
 
Nyumba tatu za vigogo zilizopo eneo la Mbezi kwa Msuguri na Mbezi kwa Yusufu zimewekewa alama ya X kwa lengo la kubomolewa ili kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro inayoanzia Mbezi hadi Kiluvya.

Vigogo hao ni balozi mstaafu wa Tanzania nchini Botswana, Gracian Rutha, mmiliki wa Hoteli ya Peacock iliyopo eneo la Mnazi Mmoja jijini hapa, Joseph Mfugale pamoja na mkurugenzi mstaafu katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mukola Nkulu.

Hizo ni miongoni mwa nyumba nyingi zinazotakiwa kubomolewa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kutokana na kuwa ndani ya hifadhi ya barabara ya mita 121.5 kila upande.

“Hakuna nyumba ya mkubwa katika nchi hii, ambaye nyumba yake iko kwenye hifadhi ya barabara itaachwa, itabomolewa tu,” ni kauli ya mhandisi mkuu Tanroads Mkoa wa Kimara, Jonson Lutechura.

Nyumbani kwa Rutha
Waandishi wetu walifika nyumabani kwa Balozi Rutha na kupokewa na Ombeni, kijana aliyejitambulisha kuwa ni mtoto wa balozi huyo.

“Ni kweli hapa ni nyumbani kwa Balozi lakini alishastaafu. Nyumba yake kweli itavunjwa lakini Balozi ametoka muda kidogo,” alisema kisha akatoa namba za simu za Balozi huyo ili atafutwe kwa maelezo zaidi. Alipotafutwa balozi huyo alisema, “Ni kweli nyumba yangu inavunjwa lakini siwezi kuongea chochote kwa sasa kwani nipo kwenye kikao, mnaweza kunitafuta kesho,” alisema.

Nyumbani kwa Mfugale

Mstaafu wa BoT

mwananchi
 
Msijali bomoeni tu, Mungu atawalipa, mwachieni Mungu tu
 
je na ile iliyojengwa kwenye ufukwe wa bahari ya mama mmoja ambaye ni mchungaji/mwanasiasa/mfanya biashara katika sekta ya elimu;alibomolewa ile penthouse yake???
 
haya mambo uyasikie kwa mwenzio tu, hao tanroads hebu wavae uhusika ingekuwa wao wangejisikiaje
 
Mh,hii serikari haina huruma kabisa,ndo maana jk alitumiaga siasa japokuwa ramani aliiona
 
hii bomoa bomoa ina mkwara kuliko zote.. nyumba zenyewe hazibomolewi ila zaidi ya miezi 6 ni mikwara tu...

mara mama ana mkapa, mara prof jay, mara balozi, mara mkurugenzi, mara tanesco wamekata umeme kupisha bomoa bomoa.. mara dawasco...

maneno mengi tu ya mkwara.. mbona bomoa bomoa zingine hazinaga mbwembwe
We jamaa hata Banda la mabanzi hauna asee, usingeandika maneno haya
 
hii bomoa bomoa ina mkwara kuliko zote.. nyumba zenyewe hazibomolewi ila zaidi ya miezi 6 ni mikwara tu...

mara mama ana mkapa, mara prof jay, mara balozi, mara mkurugenzi, mara tanesco wamekata umeme kupisha bomoa bomoa.. mara dawasco...

maneno mengi tu ya mkwara.. mbona bomoa bomoa zingine hazinaga mbwembwe
Nilichogundua tanroad wanatisha watu kutengeneza mazingira fulani ya watu kutoa rushwa, serikali iingilie kati kama wanabomoa, wabomoe wananchi wajue sehemu iliyobaki wawekeze sio mikwara kila siku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom