Nyumba na makazi ya maofisa wa serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyumba na makazi ya maofisa wa serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtazamaji, Oct 3, 2010.

 1. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kwa nini viongozi wa ngazi za juu serikali nyumba zao zipo sehemu fulani tu ?

  Je usingekuwa ubunifu wa kuwa karibu na wananchi kama kwa mfano serikali ikawa na nyumba mbili za watendaji sinza , nyumba mbili temeke, nyumba mbili ubungo, kigamboni. nk


  • Kwanza hii ingesaidia hawa watendaji wawe karibu zaidi na wanachi waone na waishi kwenye kero ziwe za maji, umeme, foleni, nk
  • Pili kwa kama watendaji walio kwenye nafasi za maamuzi wanaweza kusaidia kuondoa kero haraka katika maeneo wanayoishi . Sababu akikutana bosi fulani anakaa mbagala na mwingine anakaa ubungo waka discus kero labda wanaweza kuelewana zaidi.
  Basi nashauri serikali ijayo ili kuwa karibu zaidi na wanachi waachane na kasumba ya kuwatenga viongozi na jamii . kama ni nyumba zijengwe kila sehemu chache chache. Na hata mikoani iwe hivyo hivyo.

  Nawasilisha kwa mjadala.
   
 2. faithful

  faithful JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kitakachofuata utashauri serikali ijayo viongozi wapande ma daladala ili wajue adha wanazopata wananchi wa mbagala!
  mtazamo wangu space inaleta heshima kidogo.
   
 3. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkubwa heshima gani unaongelea??? Kwani huwezi kujenga nyumba yenye hadhi sinza, mbagala, ubungo mburahati. ?

  Hiyo space inayoleta heshima ndiyo hiyo hiyo inawafanya wasielewe wananchi wakilalamika. Kama waziri wa Umeme hajui maana ya mgao. Kama waziri wa maji hajui wala haoni adha wanayopata wnanchi kuchota maji kichwani dar.

  Mimi nahakika ukiweka nyumba ya waziri fulani mbagala japo yeye hatakuwa na yale matatizo lakini ile kuyaona na kuwaona wanachi kila siku wakiwa na matztizo kutamfanya awajibike zaidi.

  Kwanza haya mambo ya wakubwa kulundakana mi nadhani ni utamaduni enzi za ukoloni. na sababu kubwa ilikuwa ni usalama.

  Hoja yangu yes wapewe nyumba zenye hadhi lakini zitawanywe.
   
 4. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #4
  Oct 4, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280


  Haiwezekani...duniani kote viongozi hukaa kwenye residecy area A and B .......Kwa sababu maalum za kiusalama na kiutawala....ukitaka kuishi nao karibu ni lazima uwe na kiwanja kwenye maeneo hayo ambayo hata watu wa kawaida huuziwa...ndio maana tukapigania nyumba za maeneo ya aina hiyo zilizouzwa hovyo kwa dar zinapatikana ...Oysterbay,mikocheni ,kurasini etc...ndiko walikokuwa wanaishi maafisa wa ngazi za juu.....na hata mpya zilizojengwa zimejengwa huko.....
   
 5. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  pia mbagala na tandika pia
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu ndio maana nakuambia tunahitaji viongozi wabunifu wenye uwezo na akili ya kufanya mambo kwa njia tofauti kuongeza ufanisi. Ebu niambie serikali ikijenga nyumba tatu za maifisa mbagala, tatu tandika tatu ubungo kuna tatizo gani kiusalama? Au kuna tatizo gani kiutawala?

  Na huko duniani kote unaposema ni wapi? Unataka kusema mawaziri wote wa serikali ya UK au USA wanaishi kwenye mtaa mmoja ?

  Just jaribu kuangalia big picture niliyomaanisha. yaani unasema Haiwezekani au unamanisha sio rahisi?
   
 7. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2010
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  Phillemon,

  Inawezekana, ili tuendelee tunahitaji kuwaza kwa uhuru, siyo vizuri kuazima au kuiga mawazo ya watu wengine, kukariri wanayosema au kufanya.
  Kama huko nyuma nyumba za serikali zilijengwa mahali pamoja, sasa hivi ni wakati muafaka wa kuzisambaza maeneo mengine na hii itasaidia kuondoa kero mbali mbali kama traffic jamms na pia miundo mbinu itaboreshwa katika sehemu husika.
  Mojawapo ya matokeo ya ujenzi wa nyumba za serikali sehemu moja ni ufisadi wa kuuziana nyumba za serikali kwani wale waliozoea kukaa maeneo hayo hawakukubali kuondoka na wakabuni utaratibu wa kuuziana.
  Lingine ni ujenzi holela wa miji kwa kuwa watumishi wa uma wenye maamuzi hawatapata kero hyo kwani mazingira wanayoishi hayahusiki.
  Usalama wa viongozi na watumishi wa uma unategemea matendo yao kwa wananchi. Hakuna sababu ya kuhofu kama serikali inawatendea wananchi kwa haki,ila kama inakumbatia ufisadi, dhuluma kwa wanyonge, wizi wa mali za uma n.k, then usalama wao utakuwa mashakani.
   
 8. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,071
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  umesahau manzese, tandale na magomeni
   
 9. LeopoldByongje

  LeopoldByongje JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2010
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 373
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nani kakuambia kuwa hawa watawala au ukipenda viongozi wapo madarakani kwa ajili yenu. Hiyo mantiki unayoitoa ni sawa katika Ideal situation. Katika real life mambo huwa tofauti. Ndio maana baada ya Uchaguzi wale wanaoshinda na kuingia madarakani upenda na ni lazima hivyo kuitwa Mheshimiwa; utumia magari maalum VX Toyota au kwa lugha nyepesi magari ya kifahari. Upatiwa ulinzi makali, walizi huwa na silaha za moto; na Barabara kufungwa ili kuwapisha wanapokuwa matembezini. Nyumba wanazoishi ni Nzuri na ziko maeneo maalum. Vipato vyao ubadirika na kuwa juu mathalani kwa Wabunge posho ya kikao kwa siku ni zaidi ya laki moja!!!!. Kwa maneno mepesi na ya wazi hao si wenzako. kwa hiyo usidanganyike Maisha ndivyo yalivyo. Samaki mkubwa kummeza mdogo. Aliye nacho uongezewa na yule asiyenacho hata hicho kidogo hunyang'anywa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Kufanya Kazi kwa bidii ndio msingi wa maisha bora.
   
Loading...