Katika uhai wake wengi walimuona Mwalimu kuwa msaliti wa tabaka lake (a traitor of his own class), kutokana na hulka yake ya kutotaka makuu, na vile vile kutokana na uwezo wake wa kusimamia kwa kauli na vitendo, imani yake kwamba hapa nchini kwake, hakuna yeyote atakayeruhusiwa kuishi kwenye utajiri wa kutupwa, kabla ya kukidhi mahitaji muimu ya wananchi wote. Kufuatia kifo chake wametokea manyang'au na kujigawia miongoni mwao rasilimali muimu zote za taifa huku wakiwaacha wananchi wengi wakitaabika,. Kila kuchao tabaka hili la walionacho linazidi kujiimarisha kwa kubuni sheria na mifumo ya kuwagandamiza wanyonge. Ni vigumu kufikiria ya kuwa wanyonge hao wanaweza kujikwamua kwenye minyororo hii bila msaada. Itabidi azaliwe msaliti mwingine wa tabaka lake, kutoka miongoni mwa hao wanaofaidika na mfumo wa sasa, ili kuongoza mapambano ya ukombozi wa pili. Kitendo cha uongozi wa chadema cha kuanza kuhoji uhalali wa tabaka hilo la walionacho, kujilundikia marupurupu ya aina mbali mbali, wakati wale wa kipato cha chini wakipwa mishahara ambayo haikidhi haja , ni ishara nzuri ya kuwa saa ya ukombozi imewadia