Nyumba isiyomalizika inauzwa (Tegeta)

Tanki

JF-Expert Member
Apr 7, 2013
491
189
Nyumba ina vyumba vitatu (kimoja ni master).
Ina sebule na jiko ndani.
Baraza ya kutosha ipo.

Eneo lina ukubwa wa mita 29 kwa 20. Mahali ni Tegeta ( ukipanda daladala unashuka Tegeta Samaki kisha unaifuata barabara ya kwenda goba. Ni KM 3 na nusu kutoka Bagamoyo road hadi nyumba ilipo.)

Nyumba inahitaji umaliziaji tu. Ndani milango bado ila yote tayari ina fremu. Ndani plasta tayari ila nje bado. Chumba kimoja tayari kina tiles. vingine vina vina rough floor kwa ajili ya kuweka tiles.

Upatikanaji wa maji ni wa uhakika. Umeme bado ila wireling tayari na nguzo ipo nje yaani bado kuvuta umeme tu.

Gari inafika hadi barazani bila shida yoyote.

Bei ni mil 70 (maelewano yapo )

Kwa aliye serious tuwasiliane 0715553166
 
Mkuu hio heading utata..., "Nyumba Isiyomalizika.. " ina maana haiwezi kumalizika, kwahio kwenye jamii yenye imani potofu inaweza kudhani kwamba hapo kuna mizimu inayofanya nyumba isimalizike
 
Mkuu hio heading utata..., "Nyumba Isiyomalizika.. " ina maana haiwezi kumalizika, kwahio kwenye jamii yenye imani potofu inaweza kudhani kwamba hapo kuna mizimu inayofanya nyumba isimalizike

Mkuu unaonekana unaamini sana ushirikina aisee.
 
Mkuu unaonekana unaamini sana ushirikina aisee.

Hapana ninakusahihisha..., ndio maana nikasema jamii yenye imani potofu (meaning kupotoka)..., in short umekosea heading, heading yako inamaanisha nyumba yako haimaliziki
 
Labda nisaidiwe upeo wangu unashindwa kulielewa hili..
"Nyumba isiyomalizika"
Sasa itakuaje mtu akiamua kuimalizia..!!
 
Hivi kuna sehemu inaitwa tegeta samaki? Je tegeta kuna njia ya kwenda goba?
 
Umenitisha na title yako kidogo, nilidhani ni a haunted house kwamba kila ikijengwa kwa juhudi zote bado haimaliziki.
 
Back
Top Bottom