NYUMBA INAUZWA - MSONGOLA (Dar Es Salaam)

cashmoney

Member
Joined
Dec 14, 2011
Posts
89
Reaction score
31
Nyumba ya vyumba 10 (kumi) iliyomaliza kujengwa mwaka jana inauzwa. Ipo..Kata : Msongola, Mtaa:Yangeyange, Wilaya: Ilala, Mkoa: Dar Es Salaam, Ina umeme, upatikanaji wa maji, ipo kilomita chache kutoka barabarani, ina eneo la wazi kubwa mbele na nyuma. Pia Ina Leseni ya Makazi. Bei ni Tsh 90,000,000/- (milioni tisini). For interested buyers tuwasiliane kwa namba zifutazo:
Tigo - 0654 743 825, Voda - 0767 633 968, Airtel - 0686 936 444

PP.png MS001.jpg MS002.jpg MS003.jpg MS004.jpg MS005.jpg MS006.jpg MS007.jpg MS008.jpg MS009.jpg MS010.jpg MS011.jpg MS012.jpg MS013.jpg MS014.jpg MS015.jpg MS016.jpg MS017.jpg
 
Dah mbona ilijengwa kama godown vile!! Sema katika hivyo vyumba 10, je kuna vya kawaida, master bed, jiko, sebule, stoo, etc. Kwa ilivyo sijui ni darasa au nini? Maana vyumba 10 si mchezo!!
 
Maskini huwa hamuishiwi maneno ya pumba, dharau, kejeli, matusi na mizaha kwenye mabo muhimu na serious. Hiyo nyumba ya kupanga unayoishi uswahilini ipoje? Usidhalau uischokijua ama usiyemjua, kama huna hela kaa kimya.
 
Hapana ndugu. Ukiangalia hiyo picha ya nyumba hapo juu unaweza kupata shida kutokukubariana na Zogwale. Imejengwa kama shule na hilo halina ubishi na siyo matusi, pumba, dharau, kejeli wala mzaha. Pengine inategemea aliyejenga alitaka aitumie vipi na anayetaka kununua anapanga kuitumia kivipi. Vinginevyo Zogwale yuko sahihi. Ujenzi wa nyumba kama hivi kwa kijana wakileo haukubaliki, labda kama nia ni kupangisha kama kule uswaz chumba hadi chumba. With 90million/=, one is assured of buying a good plot and building a good house of his/her choice. Kuwekeza kwenye banda la shule kama hili kwangu mimi hapana.

Bora kuwa mkweli kuliko kudanganya. Picha zinaelezea nyumba ilivyo!! Sasa unalalamika nini wakati ndivyo ilivyo!! Ondoa picha ili tusiseme ukweli. Mimi sipangi naishi kwangu. Katika matangazo ya biashara kwa nyimba kama hiyo ya vyumba 10 tulitegemea useme kama ni ya familia ambayo inajitosheleza say master and other rooms, na kama ni ya biashara kama gesti au shule/dispensary kama inavyoonekana sema na si kutema mapovu ya hasira.
 
Asante sana Bwaga ya moyoni kwa kumpa ukweli huyu jamaa. Hakika itabidi atueleze matumizi ya hii nyumba na ilivyojengwa ni kwa nini iuzwe mil. 90 tena kwa maeneo hayo. Tatizo tukisema ukweli tunaonekana tunadharau. Mi. 90 is not a joke!! Utanunua kiwanja na utajenga nyumba nzuri ya up to four rooms (family) na visaidizi vyake kama stoo, jiko, public toilet etc.
 
Mnunuzi hawezi kupangiwa matumizi ya anachonunua, na si lazima matumizi yangu yafanane na mwengine. Mnunuzi ndo atajua ataitumiaje, kama ni shule, guest house, madarasa, dispensary etc. Kwako wewe milioni 90 ni kubwa ila kwa mwengine hasa mwenye kujua thamani ya ardhi atanielewa.
 
Ulitegemea wewe na nani?
 
Bei na gharama ya ununuzi wa viwanja na ujenzi wa nyumba hutegemea mambo mengi hasa location na eneo la kiwanja, mazingira na hali ya kiwanja (ardhi tambalale au iliyo kwenye mwinuko au mteremko), aina (design) ya nyumba utakayojenga, vifaa, marighafi utakazotumia, ubora wa vifaa vilivyotumika, upimwaji wa kiwanja, ukuaji wa mji katika eneo husika, upatikanaji wa huduma muhimu kama vile umeme na maji na mengineyo.
 
Hapana ndugu. Ukiangalia hiyo picha ya nyumba hapo juu unaweza kupata shida kutokukubariana na Zogwale. Imejengwa kama shule na hilo halina ubishi na siyo matusi, pumba, dharau, kejeli wala mzaha. Pengine inategemea aliyejenga alitaka aitumie vipi na anayetaka kununua anapanga kuitumia kivipi. Vinginevyo Zogwale yuko sahihi. Ujenzi wa nyumba kama hivi kwa kijana wakileo haukubaliki, labda kama nia ni kupangisha kama kule uswaz chumba hadi chumba. With 90million/=, one is assured of buying a good plot and building a good house of his/her choice. Kuwekeza kwenye banda la shule kama hili kwangu mimi hapana.

Sio kosa lako...maneno yanajieleza, na hata mimi sitegemei vijana kama wewe ambao ndo kwanza mmeajiriwa mwaka jana huku bodi ya mikopo ikiwadai muweze kununua nyumba kwa pesa zenu. Mwenye uhakika na anachosema hatumi pengione au labda. Usitafute umaarufu kwenye mambo usiyoyajua, hii sio facebook.
 
kwa kifupi stunna aka cash money huo mjengo hauna isssue mtu hawezi toa 90m kununua darasa,hii hata kwa familia hifai labda hostel ya wanafunzi wa chuo.
 
Kwani mi nimekwambia nawauzia wenye familia? Nyumba ipo maeneo ambapo mji unakuwa kwa haraka, hivyo mahitaji ya nyumba kwa ajili ya Hostel, Madarasa, Guest House, Godawn nk ni muhimu na yana uhitaji mkubwa kwa baadhi ya watu, hivyo ukiona biashara haijakulenga wewe ni busara kuwaachia wengine kuliko kupunguza ama kuongeza neno.
 
Kubali kukosolewa usiwe mkali inaonekana hujui ethics za biashara. Kwa muonekano hiyo nyumba inafaa kwa guest house au hostel unapata shida gani kusema hivyo kwenye tangazo lako? Kama huwezi udalali waachie wenye fani zao.
 
Naruhusu kukosolewa pale ninapokosea, na naomba kuelimishwa kwa nisiyoyajua. Naomba utuelekeze hizo ethics za biashara, pili mi sio dalali bali ni mmiliki wa nyumba, na tatu kama nilivyowaeleza vilaza wenzako kuwa matumizi ya nyumba yako katika uamuzi wa mnunuzi hivyo siwezi kutangaza kuwa nauzaq nyumba kwa ajili ya matumizi fulani, mwenye macho anaona, mwenye hela ananunua.
 
Cashmoney ukileta biashara halafu watu wakakuuliza maswali mengi sana jua hukuelezea biashara yako vizuri na ndiyo maana unaulizwa maswali. Sasa wale wanaouliza maswali usiwape majina ya bandia kama ulivyowaita vilaza na nina hakika katika hao ulioita vilaza nami nimo maana nilikuuliza maswali ya msingi na ukanijibu kwa lugha ambayo si nzuri sana. Anyway, watanzania wengi marketing skills zetu ni ndogo sana na tunajifanya mafundi wa maneno ya mitaani!!! Hongera!!
 
Mnunuzi hawezi kupangiwa matumizi ya anachonunua, na si lazima matumizi yangu yafanane na mwengine. Mnunuzi ndo atajua ataitumiaje, kama ni shule, guest house, madarasa, dispensary etc. Kwako wewe milioni 90 ni kubwa ila kwa mwengine hasa mwenye kujua thamani ya ardhi atanielewa.
Acha ukurya wako hapa nyumba umejenga vibaya bado mbishi tu jenga mijengo ya kisasa we uliona wapi nyumba moja tena sio gorofa ni ya chini tu ina vyumba kumi? hiyo gesti, hosteli, bweni au nini? tatizo umekuja mjini na ramani ya babu zako kutoka Mara unataka kutujengea Dar linakudodea hilo toa lipicha lako chafu mtu huendi na wakati? matangazo yenyewe digitali siku hz!!!
 
Mwanzoni nilidhania ni kanisa ila sikuona msalaba. Pili rangi inatisha, tatu bei ni kubwa mno kulingana na maeneo illipo
 
Acha ukurya wako hapa nyumba umejenga vibaya bado mbishi tu jenga mijengo ya kisasa we uliona wapi nyumba moja tena sio gorofa ni ya chini tu ina vyumba kumi? hiyo gesti, hosteli, bweni au nini? tatizo umekuja mjini na ramani ya babu zako kutoka Mara unataka kutujengea Dar linakudodea hilo toa lipicha lako chafu mtu huendi na wakati? matangazo yenyewe digitali siku hz!!!

Acha mambo ya ukabila kwenye biashara za watu, unawatusi wahusika. Sasa mimi na wewe nani wa kuja Dar, wakati hata nyumba ya vyumba 10 hujawahi kuiona? Pole sana kama umekwazika, na kwa kuwa dua la kuku halimpati mwewe, nyumba nimeshauza kwa Mil 80 kwa wenye uelewa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom