Nyumba inauzwa kariakoo

Nyumba inauzwa kariakoo

Yani mtu uweke bilion 2 sehemu ambapo hakuna mfumo wa Fire , Mitaa mibovu! Sewage system mbovu.

Tembeeni muone , Marekani unanunua Majumba kwa hiyo hela miji mizuri unakula Kodi vizazi na vizazi.
Ishu sio kununua nyumba ,ishu hiyo nyumba iko wapi,unafahamu bei fremu za biashara kariakoo kiasi gani?
 
2bil bei ya kawaida sana kwa kariakoo, tena bei hiyo ni nafuu sana,
Bila kukoaea utakapoinunua Leo hii,ukaihifadhi tu,kwa jinsi uchumi unavyofunguka kwa kasi baada ya miaka miwili tu,utaiuza bil 3.5
#Yule Jamaa aliua kabisa uchumi wa taifa hili.
Kinachofanya nyumba/viwanja Kariakoo ziwe ghali ni biashara ya maduka. Tangu waanze mtindo wa kununua viwanja na kuweka frem za maduka bei imekuwa iko juu sana kulinganisha na quality ya viwanja/nyumba. Swali muhimu la kujiuliza: Je, Kariakoo itaendelea kuwa center ya maduka ya bidhaa mpaka lini? Haya mambo ni kama kamari. Inawezekana kabisa kwa muda wa mwaka mmoja tu mfumo wa biashara ukabadilika, na tukajikuta maduka yamehamia sehemu nyingine kabisa yenye nafasi zaidi. Hili linanikumbusha mambo yaliyotokea Manzese siku za nyuma. Kwenye miaka ya 2000 mwanzoni Manzese ilikuwa ina maduka mengi sana ya nguo. Kipindi hicho Kariakoo ilikuwa haijapata umaarufu wa sasa. Ghafla, kwa muda wa miezi sita tu wenye maduka wakahamia Kariakoo wote. Wenye nyumba waliokuwa na maringo ya kufa mtu, huku wakipandisha bei na kuzidisha vituko kila siku wakajikuta wamebakiwa na frem zisizo na thamani. Hakuna anayezitaka.
 
Ishu sio kununua nyumba ,ishu hiyo nyumba iko wapi,unafahamu bei fremu za biashara kariakoo kiasi gani?
Ni ghali, kwa sababu ya frem za maduka. Lakini hii haitoi guarantee kuwa Kariakoo itaendelea kuwa eneo maarufu kwa biashara kwa muda mrefu. Dunia ya sasa mambo ynabadilika kwa kasi sana. Miaka michache ijayo unaweza kukuta umaarufu umehamia sehemu nyingi, hata Bagamoyo.
 
Hata kama ishu ni sehemu ya biashara lakini bado bei ipo juu sana kwa sababu kwa kiasi hicho zipo sehemu za biashara pia unaweza kununua nyumba na kujenga jengo kubwa na kupangisha fremu kwa hela nyingi tu.
 
Pia nahisi Kuna shida mahali,mpaka imefikia kutangazwa humu,kwa maeneo ya kkoo nyumba nyingi zinauzwa kimya kimya na pia wengi miaka hii hawakubali kuuza zaidi wanapendelea ujenzi wa ubia
 
Watu siku hizi wapo kwenye Tec.......
haya mambo ya manual market yanaanza kupitwa na wakati.....
 
Pia nahisi Kuna shida mahali,mpaka imefikia kutangazwa humu,kwa maeneo ya kkoo nyumba nyingi zinauzwa kimya kimya na pia wengi miaka hii hawakubali kuuza zaidi wanapendelea ujenzi wa ubia

sijawahi kuamini kwenye hii siasa ya ujenzi wa ubia wa namna kama hiyo, yani nyumba yenyewe ya urithi badala ya kutia bei mukagawana mnjaiingiza kwenye mambo ya ubia muje kukorogana mbeleni.
Kwa muekezaji kwake hua sio hasara, mana pengine angelihitaji kutumia 5 b kwa full project lakini atatumia 2.5 na zitakazobakia atatumia kwa uekezaji mwengine. Lakini kwa wewe mmiliki na akili zako za kimaskini ni kujizonga tu.
Kuna rafiki yangu mmoja waliwahi kuingia kwenye huo mtego huku vichwa vyao vikibeba mzigo wa sifa za kijinga kuwa wao hawawezi hama mjini, mwisho wa siku wameishia kupigana ndumba kwa kugombeana hela ya kodi za milango.
 
Ni kweli unapozungumzia imani ni swala lingine na linatofautiana kati ya mtu na mtu

Mtaa huo huo wa Pemba ilipo hiyo nyumba ukivuka mtaa sikukuu Kama unaelekea Livingston Kuna nyumba imejengwa kwa ubia na warithi wamefaidika na hakuna dalili ya wao kurogana

Shida ya huyo uliemchukulia km kielelezo kwako ni kwamba hakufuata utaratibu mzuri wa uingiaji wa mkataba na aina ya mkataba,kwani Kuna mikataba ya Aina mbili.Mosi ni mbia ajenge na baada ya kipindi fulani atakabidhi nyumba kwa wenyewe na pili mbia atajenga halafu atagawana na wenyewe kwa mafungu watakayokubaliana na itakuwa kwa daima na kila mmoja atakuwa na hati miliki yake kwa sehemu atakayopewa

Kwa hilo la kurogana watu huwa wanarogana hata ikiwa hamchangii mali na hamhusiani ila kwa upande wangu ni bora kuingia mkataba wenye manufaa kuliko kuuza
 
Unaijua billion we we? Au unataja tyuu? [emoji23]
 
Kwa hilo la kurogana watu huwa wanarogana hata ikiwa hamchangii mali na hamhusiani ila kwa upande wangu ni bora kuingia mkataba wenye manufaa kuliko kuuza

Mimi naamini Ni fikra za kivuvi na za kimaskini tu, unapouza na kukamata hela ndefu mkononi hapo ndipo maisha yanapoanza.
Ubia halafu usubiri miaka 25 ndio uanze kula matunda!!!!!!!! haileti picha kabisa yani
 
Kweli inawezekana zikawa ni fikra za kivivu na kimaskini ila husemwa kunguru muoga hukimbiza mbawa zake, mfano mtu ameishi kwa ufundi kwa zaidi ya 30,halafu uzeeni ndo aje aanze biashara baada ya kuuza nyumba ya urithi!!!! Kutoboa ni ngumu

Pili si kila mkataba ni wa kusubiri ,mikataba mingi ya Sasa ni kuwa unapewa sehemu yako ya kumiliki pamoja na hati pindi tuu jengo linapokuwa limekamilika kwa hiyo unaanza kula matunda mapema tuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom