Nyumba inapangishwa mbezi beach | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyumba inapangishwa mbezi beach

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Kitomai, Jun 1, 2011.

 1. Kitomai

  Kitomai JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,032
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Ipo eneo la Samaki. Ina vyumba vitatu vya kulala, sebure, jiko. kodi shs 600,000 kwa mwezi. ruksa kulipa kodi ya miezi sita. Kwa maelezo zaidi piga simu 0717114409
   

  Attached Files:

 2. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kwanini mtu alipe kodi ya miezi sita?

  Hii kitu siielewi kwa tabia ya kiafrica

  Sasa ukipata miezi sita iweje?
  Ukichukua deposit ya mwezi mmoja inakaaje?

  Nadhani ni bora kuweka min contract ndio miezi 6.

  Na je utadai pesa ya miezi 6 baada ya 6 months kuisha?

  Ndio maana hongo hazitaisha
   
 3. Kitomai

  Kitomai JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,032
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kwanini mtu alipe kodi ya miezi sita?

  Hili swali ungekua katika nafasi nzuri ya kulipatia majibu mazuri kama ungekua na wewe ni mpangishaji. Una nyumba ya kupangisha wewe? Kama hauna utakuja kupata majibu mazuri utakapokua na nyumba ya kupanga.

  Nitakupatia jibu lingine la kudhani. Nadhani ''demand'' is higher than ''supply''.
  Si unajua tena, the higher the demand the lower the supply the higher the price.

  Mimi ningependa mtu awe analipa kodi mwisho wa mwezi baada kupata mshahara

  Hii kitu siielewi kwa tabia ya kiafrica

  Sasa ukipata miezi sita iweje?

  Tafuta mkopo ofisini kwako au Benk au kwa ndugu na jamaa au kama vipi panga hotelini wao wanachukua kodi ya siku moja. Hacha kulalamika sana tafuta njia mbadara hii ndiyo Africa zaidi ya uijuavyo.
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu, ukali huu hautakufukizia wateja kweli?
   
 5. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Na mimi ndo nimeshangaa mkuu Mpita Njia, jamaa kawa mbogo! anyway napita tu kwa sasa!
   
 6. Kitomai

  Kitomai JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,032
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hapana sitawafukuzia. Mimi ni mtu ambaye nipo wazi sana na nadhani hayo ndio maumbile yangu ya asili.
  Naomba yeyote ambaye amekwazika kutokana na maoni yangu anisamehe.
   
 7. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  <br />
  Bongo bwana mtu ana poor customer service badala ya kujirekebisha analeta visingizio ndio maumbile yake. Km maumbile yapo hivyo na unajitambue kwanini usifanye kazi nyingine? Kazi ni combination ya skills.
  Lakini mkuu kwa udadisi; hiyo law ni ya demand au ni law ya nini ulioweka pake kuzungumzia pricing za property? Halafu hata ingekuwa law ya demand; mbona wewe vitu vyako vyote huwa vipo overpriced? Au ni law ya comission. Am sure yr r nt doing good to yrself through overprice. Why nt trying selling many goods and increase turnover. Hata hao unaowafanyia hiyo biashara mali inakaa sokoni muda mrefu kisa overpricing mwisho wa siku unakosa wateja na wao wanaathirika. Kwahiyo, in one hand unapoteza wateja na pia hao wanaokupa vitu. Tunaweza kukushauri kwenye biashara inakuwaje kuliko unavyofanya kwa kuhitaji commission kubwa.
   
 8. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hiyo ndio customer service ya bongo!!
  Sehemu nyingi duniani Mteja siku zote hubembelezwa na hupewa lugha nzuri wakati wa kufanya biashara lakini bongo mteja ananyanyaswa!
   
 9. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Amekuwa mkali for nothing. Tatizo sio mwenye nyumba kwani hata mimi ningekuwa na nyumba ya kupangisha uenda ningependa nilipwe hata kodi ya miaka miwili ili hizo pesa zinisaidie kufanya shughuli nyingine ya maendeleo. Hapa tatizo ni serikali amabayo haijaweka sheria ya kuwalinda wapangaji. Ukienda nchi zenye serikali zenye akili, hicho kitu cha kudai kodi ya zaidi ya mwezi mmoja hakipo. Ni kinyume cha sheria. Kodi inalipwa kila mwezi basi!!! Nchi nyingi za ulaya ndivyo ilivyo. Zaidi utatakiwa kulipa deposit ya mwezi mmoja au miwili kwa ajili ya guarantee ya vyombo na furniture.

  Umefika wakati serikali ifikirie kuwalinda raia wake wanyonge kwani tabia hii ya kudai kodi kwa miezi kadhaa inasababisha watu wawe wadokozi na kuomba rushwa!!!!!

  Ila nimefurahi kwamba angalau mwenye nyumba anataka kulipwa kwa Tshs. na sio USD kama wengi wanavyofanya. Kwa hilo nampongeza.

  Niko interested kupanga hiyo nyumba, je kodi inaweza kushuka kidogo?

  Tiba
   
 10. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hiyo rent ukiangalia hiyo amount imekuwa-pegged to USD!
  Kuhusu landlord kulipwa kodi ya mwaka ama hata akitaka miaka 10 that's ok hakatazwi as long as lugha ya kiungwana na kibiashara inakuwa-involved......sio kama huko nyuma jama anasema " Kama hutaki kaa pembeni/au kama unataka kulipa kila mwezi nenda hotel"
  Kama nilivyosema mteja bongo ni mtu wa kunyanyaswa na kulazimishwa tofauti na sehemu nyingine duniani ambapo mteja ni mfalme. Aaah anyway, ndio bongo yetu hiyo, kila mahali customer service ni zero, banks, kwenye daladala, bar, hotelini, serikalini, clubs, mpaka makanisani....Labda siku moja tutafika
   
 11. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,971
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Mkuu upo sahihi,Ukweli apa Tanzania maswala ya estate bado tupo nyuma,uwezi kulinganisha na Kenya au South Afrika,UK or USA.
  Nnafikiri haya mambo ya kutoa deposit then unalipa kodi kila mwezi apa Tanzania ni baada ya miaka 5 ijayo due to few apartments na uwingi wa wanazoziitaji
  So kwa sas tukubali hali hii
   
 12. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  mbona ghali hivyo? Mbezi beach ilikuwa zamani, sio siku hizi.
   
 13. Kitomai

  Kitomai JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,032
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Binafsi si-encourage taking offense easily, lecturing on mistake of others, chronic fault- finding, nagging or blaming others for things that goes wrong. Nilichokua najaribu kuelezea hapo ni ''Housing supply and demand in Tanzania briefly''. kila ninapotoa tangazo napokea maoni kutoka kwa wadau mbali mbali. Maoni yanatofautiana kulingana na makundi mbali mbali, kutoka kwa ''young singles'', ''adult singles'', ''semiactive retirees'', ''active retirees'', ''double-income porfessionals, no children'', double-income professionals, one to three children'', ''single-parent households, one to three children''.
  Ninayafanyia kazi maoni yenu. Asanteni sana.
   
 14. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sasa unalalamika nini? Watu wanakusaidia kubehave proffesionally wewe unaleta maneno mengi? Ishu si ku-encourage kama unavyotuaminisha, tunakushauri how you can improve business. Kuna watu wanaexposure, skills na wafanyabiashara kwahiyo sikiliza unachoambiwa. Sentensi ya mwisho ilitosha saana bila maelezo mengi. Na wengine hapa ni wateja wako.
   
 15. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #15
  Jun 3, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,131
  Likes Received: 3,320
  Trophy Points: 280
  Awesome crib!
   
 16. e

  emrema JF-Expert Member

  #16
  Jun 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwanza unaonekana hujasomea Estate Agency and Marketing umeona tu kuna potential ukaventure. Umevamia tu fani jua kwamba hiyo ni Profession na inahitaji customer care ya hali ya juu. Nakushauri nipm nikupe free lecture on the practice of Estate Agency and Marketing na pia Estate management as a whole.
   
 17. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #17
  Jun 3, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kitomai ndio watu kama nyie/wewe mtakuwa mnagombana na wateja wenu

  Nimekuuliza maswali unaniuliza maswali? Si lazima kila mtu apangishe nyumba alizonazo extra... mfwuuu kubali umechemsha hata mtoto miaka 7 atajibu vizuri asifukuze wateja.

  Kwa hiyo naomba uelewe kuwa sio kila mwenye kuuliza swali hanakuwa hajui mambo

  Umeandika mengi kunijibu kwa hasira ulitegemea nini kuweka post yako humu na tusijibu?

  Nenda kajifunze mawasiliano na kupunguza asila wakati unategemea ka asilimia fulani ikusaidie na ujifunze kusikiliza ushauri wa wengine

  Sijui mambo ya age limit na status ya mtu inaleta utofauti hao wote lazima wanapata income kutoka mahala
   
 18. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #18
  Jun 3, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  MAra nyingine sisi customers tunacomplicate mambo pasi lazima; Bongo yetu tunaifahamu, na default za wapangishaji tunazifahamu (miezi6, 12, 24), wengi wetu ama tumepanga, ama tumepangisha; iwe nyumba ya kuishi au ya biashara. Hata kama umeishi sana kwa wenzetu kiasi cha kusahau maisha halisi ya bongo, unauliza kwa mpangishaji au dalali kwa Lugha nzuri tu (mf; Je, siwezi kulipa kwa mwezi?) kwa hakika kama mwenye nyumba akitathmini chanzo chako cha pesa akajiridhisha kuwa kweli utalipa kila ifikapo mwisho wa mwezi bila kukosa (Visingizio) hawezi kataa kukupangisha kwa terms unazotaka (biashara maelewano)!
  Ni hayo tu wadau, tunajenga!
   
 19. Kitomai

  Kitomai JF-Expert Member

  #19
  Jun 3, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,032
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Nimewasikia wadau.nipo tayari kujifunza zaidi.
   
 20. Mrbwire

  Mrbwire Senior Member

  #20
  Jun 6, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 197
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kitomai; Nimependa hiii...."Niko tayari kujifunza"...
   
Loading...