Nyumba ina mauzauza


Kuna mtu anaitwa mshanajr ni wakala wa mambo hayo mtafute utapata msaada
 
Last edited by a moderator:
Mshanajr njoo huku utoe msaada tafadhali
 
Kwani huyo singasinga hayo matanki ya maji aliwapa au mlipora bila idhini yake? Asije akawa anawatesa kwa hivyo vitu vyake, maana wenye nyumba mnavisa. Vipi lakini sigara kubwa inapanda? usije ukawa umeitandika inakuletea mawenge. ..
 
Kwani huyo singasinga hayo matanki ya maji aliwapa au mlipora bila idhini yake? Asije akawa anawatesa kwa hivyo vitu vyake, maana wenye nyumba mnavisa. Vipi lakini sigara kubwa inapanda? usije ukawa umeitandika inakuletea mawenge. ..

Alituachia na sigara kubwa haipandi mkuu hata hivo hilo tukio lilitokea asubuhi nipo sober
 
Uoga wako tu mkuu. Kama unataka kuamini chukua vijana wa mabange wakavute usiku kucha humo. Huyo singasinga atalewa moshi na harudi tena.
 
Kwamaelezo yako inawezekana singa singa aliweka makafara mengi sana hapo. Hii story inanikumbusha baba wa rafiki zangu alikuwa meneja wa mashamba ya chai miaka ya 70. Walipewa zile nyumba walizokuwa wanaishi wazungu, basi tukiwa shule alikuwa anahadithia vituko kwenye nyumba, watu wote wanaweza kuwa sittingroom, unakwenda kuoga unasikia mtu anapiga mluzi, au unakuta taulo ambalo ni geni kabisa bafuni.
 
Hahaaa Jf raha lol,mkuu hizi stories za kuliwa kiboga zitakua moja ya Vitu unavyoviogopa,ndio maana vinakujia ukiwa subconscious, na pia kinadharia unaogopa uchawi, both combination imekuwa ukiogofya ndio maana unaota ,hamna lolote mkuu...

Ila umenichekesha handazz lol,Ngoja na mie niende handazz lol,nikajionee mambo, sitaki kusimuliwa hahaaa
 
Hayo ni madhara ya bangi handaz unazovuta mpaka saa saba usiku huku unatamani pesa na makochi ya Singasinga, na huku akili iko kwenye wanakonyea, hayo ndo utakayoendelea kuyaona ukiendelea kutumia handaz
Samahani, Handaz ni nini?
 
Hayo mambo yapo sana mkuu, inafikia hatua unayazoea tu, nakumbuka kipindi cha kwanza Kuhamia kwenye Nyumba yetu mama yangu aliniambia niende peke yangu siku ya kwanza, ila usiku ilikuwa balaa mchanga ulikuwa unamwaga kama mvua, na nimekutana na majanga ya namna hiyo sehemu nyingi tu, inafikia hatua unazoea tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…