fareed uziel
JF-Expert Member
- May 27, 2015
- 665
- 720
Habari wakuu,
Poleni kwa kazi la kulisongesha mbele taifa na natumaini ni wazima wa afya.
Tatizo langu ni hivi,
Tuna nyumba yetu maeneo ya Mwananyamala ambayo hua tunapangisha. Mwaka 2013 mwezi wa kumi tulipata mpangaji singasinga (wale wahindi wanaovaa vilemba) ambaye alipanga.
Sasa mwezi wa nane huu mwishoni alihama na kutuachia nyumba pia alichimba kisima kwahiyo alituachia masimtank pamoja na pump ya maji, sasa mzee wangu alipanga airekebishe nyumba ndo apangishe tena kwahiyo akaniambia mimi niwe nakaa kwenye nyumba hii mpaka hapo atakapotengeneza.
Sasa siku ya kwanza kukaa nilirudi mida kama ya saa 7 usiku,ile nafungua mlango naingia ndani nakutana na baridi la ajabu wakati nilizima kila kitu na hamna AC wala fridge yaani baridi kama kuna AC kuliko nje nilipotoka.
Nikakausha nikajua handaz tu sasa mimi hua navuta sigara nilikaa sitting room yaani hamna upepo lakini nawasha sigara na njiti haiwaki yaani haiwaki kabisa, nikatoka nje ndo ikawaka mi nilipata wasiwasi ila kwakua nilikuwa nipo high (handaz) nikachukulia poa nikarudi kwa akili yangu niliweka godoro chini pale pale sebuleni ili nilale, usiku ule nalala nikawa naota ndoto za ajabu ajabu, nikawa naota kuna mzee mmoja hapa mtaani (ni mlinzi wa mduka duka ya hapa) et anataka kunif**ra yaani naota mzee anataka kunila tigo.
Asubuhi nakumbuka niliamka saa 3 nikawa bado nipo kitandani nachezea simu nikasikia jikoni kama kuna mama anaongea huku akipika tena mpaka kelele za vyombo nazisikia, basi nikaenda jikoni kuangalia nikakuta hamna kitu yaani nikashangaa, basi ile kurudi sebuleni nikakuta yule mzee singasinga pamoja na mwenzake simjui wamekaa kwenye makochi (sijui yalitokea wapi).
Wanaongea aisee! Niliishiwa nguvu hata kukimbia nilishindwa naona sababu ya uzito wa kujinyea nikaanza kupiga kelele huku naelekea mlangoni kufika milango nilifunga nikaanza kusoma madua yaani sala zote niliomba na kutoa shahada mpaka kuna jirani akaja na kuniuliza kunani ndo akili ikarudi sawa.
Tukaja sebuleni kuangalia hakuna kitu, nilichoka ndo nikaondoka hapo kumwambia mzee na yeye akanijibu atalishughulikia, wadau mi mpaka sasa hivi ile picha ya yule singasinga inanijia nikiwaza yaani sina raha na sijui nifanye nini?
Usiombe yakutokee, wadau unaweza ukajua haya mambo hayapo ila yapo nimeamini.