Nyumba 2500 zimelipwa fidia bonde la Mto Msimbazi

Nyumba 2500 zimelipwa fidia bonde la Mto Msimbazi

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
5,895
Reaction score
11,788
DODOMA; SERIKALI imesema Mradi wa Bonde la Mto Msimbazi, unatarajia kuhamisha nyumba zaidi ya 3,000 na hadi sasa nyumba 2,500 zimeshalipwa fidia na kuhama eneo la mradi.
-
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Reuben Kwagilwa ametoa kauli hiyo bungeni leo Februari 5, 2026 alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba, aliyehoji lini mradi huo utaanza na kukamilika.
-
“Mradi wa Bonde la Mto Msimbazi unalenga kupunguza athari za mafuriko katika eneo la Jangwani na kuboresha mipango miji katika eneo la chini la bonde. Mradi ulianza kutekelezwa rasmi mwezi Februari, 2023 na utatekelezwa kwa muda wa miaka sita.
-
“Mradi unatarajia kupanua na kuongeza kina cha Mto Msimbazi pamoja na kuongeza uwezo wa mawanda ya mafuriko katika eneo la chini la bonde. Udongo utakaotokana na upanuzi huo utatumika kutengeneza maeneo salama kwa makazi na biashara pembezoni mwa bonde. Jumla ya hekta 57 zinatarajiwa kupatikana kwa matumizi hayo.
-
“Mkataba wa ujenzi huu unatarajiwa kusainiwa mwezi Februari, 2026 na kazi kuanza rasmi ifikapo mwezi Mei, 2026.
-
“Mradi wa Bonde la Mto Msimbazi unajenga daraja jipya eneo la Jangwani lenye urefu wa mita 390 chini ya usimamizi wa TANROADS, kazi hii imeanza tangu mwezi Mei, 2025 na ujenzi umefikia asilimia 15.
-
“Mradi utajenga karakana mpya ya mabasi ya mwendokasi katika eneo la Ubungo Maziwa, mkataba wa kazi hii unatarajiwa kusainiwa mwezi Februari, 2026.
-
“Vilevile, mradi unatarajiwa kuboresha maeneo korofi katika eneo la juu la Bonde pamoja na kuratibu shughuli za kibinadamu ili kudhibiti mmomonyoko wa udongo unaotuama eneo la chini na kusababisha mafuriko,” amesema Naibu Waziri huyo.

1770355517434.jpg


Source: HabariLeo
 
Back
Top Bottom